Al-Azhar Al-Shareif yatoa Misaada ya Haraka kwa Wapalestina wa Gaza

  • | Tuesday, 24 October, 2023
Al-Azhar Al-Shareif yatoa Misaada ya Haraka kwa Wapalestina wa Gaza

       Mheshimiwa Imamu mkuu aamuru kupeleka msafara kutoka wa Baiti ya Zaka na Sadaka kwa Ukanda wa Gaza, unaoundwa na lori 18 zinazojazwa na Dawa, vyakula, na misaada.

Jumanne jioni msafara wa Baiti ya Zaka na Sadaka ya kimisri ulifikia bandari kavu ya Rafah kwenye mpaka wa Misri na Palestina, uliopelekwa na Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa/ Ahmad Al Tayyeb, Shekhi wa Al Azhar, msimamizi mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Baiti ya Zaka na Sadaka ya kimisri, kwa ajili ya kuunga mkono na kuwaokoa wadugu wetu kwenye Ukanda wa Gaza.

Msafara huo unakusanya lori 18 zinazojazwa na Dawa, vyakula, na misaada mbalimbali, kama maji, vyakula na nguo kwa mujibu wa kampeni ya "waokoeni Gaza" kwa ajili ya kuunga mkono wadugu wetu kwenye Ukanda wa Gaza.

Msafara huo ulipelekwa kwa amri ya Mheshimiwa Imamu Mkuu wakati ambapo wakazi wa Gaza wanateseka sana na hali mbaya wa kibinadamu, kutokana na mzunguko mkubwa unaopigwa na ukoloni dhidi ya Ukanda wa Gaza, na kufa shahidi maelfu ya watoto, wanawake na wazee wasio na hatia.

Na msafara huo unazingatiwa kuwa kubwa zaidi unaopelekwa na Al-Azhar, na unakuja kutokana na jukumu la kihistoria la Al-Azhar katika kuutetea suala la Palestina na kuwasaidia wadugu wetu Wapalestina. Nao ni kuendelea kwa misafara ya matibabu na misaada ambao Al-Azhar inashughulika kuipeleka kutokana na jukumu lake la kibinadamu na kimataifa.

Na msafara huo uliongozwa na profesa/ Sahar Nasr, mkurugenzi mtendaji wa Baiti ya Zaka na Sadaka ya kimisri, pamoja na idadi ya wafanyakazi wa Al-Azhar na Baiti ya Zaka, pamoja na kuendelea kampeni ya "waokoeni Gaza", ili kuendelea kuunga mkono na kutetea suala la Palestina na kuwasaidia watu wetu huko Gaza.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.