Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu matukio huko Gaza

  • | Monday, 30 October, 2023
Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu matukio huko Gaza

     Maamkizi ya baraka na amani ya Mwenyezi Mungu kwa wapiganaji wa kipalestina, na kwa wananchi wa Gaza wasio na hatia ambao ndio alama ya enzi na uvumilivu, na kwa watoto na wanawake wenye subira kubwa, maamkizi mazuri kwenu mkiwa mnakabiliana kwa miili yenu dhaifu isiyo na kinga moto ya mashambulizi, yanayopelekwa na jeshi la kigaidi lisilo na huruma wala rehema, na lililojitenga mbali na maana yote ya maadili na ubinadamu, likatekeleza jinai zote za kikatili; kama vile kuzishambulia hospitali, kuharibu misikiti na makanisa, kuwaua watoto, wanawake, waandishi wa habari na raia wasio na hatia ambao hawana uwezo wala nguvu ya kujiteta.

 Al-Azhar Al-Shareif inapeleka Maamkizi yake mema kwenu enyi mashujaa, wakati ambapo mnakabiliana kwa imani yenu meli zinazobeba ndege za kivita na vifaa vya kurusha makombora ya kuangamiza halaika, na mnakabiliana nazo mkishikiliana na imani yenu kwa Mwenyezi Mungu, bila ya kuogopa au kunyenyekea.

Enyi mashujaa: jimudu nguvu zenu kutoka kwa Qur'ani tukufu, na tegemeeni kauli ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: "Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini".

Pia, Al-azhar Al-Shareif inathamini kwa heshima na shukrani kubwa msimamo mshujaa wa Bwana Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, aliyetoa wito wazi wa kusitisha mashambulizi dhidi ya wanyonge na wasio na hatia huko Gaza bila ya kuogopa wala kunyenyekea, maamkizi kwako ewe mtu mshujaa unayesema maneno ya haki na uadilifu.

Aidha Al-Azhar inashukuru msimamo wa watu huru popote walipo ulimwenguni ambao hawakunyamaza kimya, bali walitoka barabarani kulaani mauaji ya kikatili yanayofanywa dhidi ya wanyonge mjini Gaza, wakitoa wito wa kuyasitisha mashambulizi ya kizayuni na kuweka ukomo kwa mauaji dhidi ya watoto na wasio na hatia.

Vile vile, Al-Azhar Al-Shreif inazitaka serikali za nchi za Kiarabu na Kiislamu kuwasaidia ndugu zao huko Palestina kwa haraka, na kutumia uwezo wao, utajiri wao, na vyanzo vyao vya nguvu kwa ajili ya kuwanusuru na kuwaunga mkono na kukomesha ukandamizaji wa utawala huu wa kikoloni.

 

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.