Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu mauaji ya Beit Jabalya yaliyofanywa na mamlaka ya kigaidi ya kizayuni

  • | Wednesday, 1 November, 2023
Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kuhusu mauaji ya Beit Jabalya yaliyofanywa na mamlaka ya kigaidi ya kizayuni
     Kwa hakika hivi karibuni mamlaka ya kizayuni imegeuka kuwa kali kama mbwa mwitu mwenye njaa aliyeambukizwa na tamaa ya kuwaua watoto, wanawake na wasio na hatia, na kufurahia kula nyama zao na kunywa damu zao pasipo na anayeweza kuwazuia kufanya hivyo wala anayethibitisha jinai hzio, bali magaidi hawa wanasaidiwa na kimya ya ulimwengu ambayo ni kama kimya cha wafu waliomo makaburini mwao, na kubana uwezo wake wa kuzuia mamlaka hiyo ya kigaidi na kuweka mwisho wa milo zao ya kila siku kutoka damu ya watoto, wanawake, wazee na vijana wa Gaza.
Hakika Al-Azhar Al-Shareif inamwomba Mwenyezi Mungu Awalinde wananchi wa Gaza kwa enzi yake na utawala wake, na awaangamizze maadui na kuwazuia kuuingia na kukalia ukanda huo, na Atuonyeshe katika madhalimu, wauwaji na wanaowasaidia miujiza ya uwezo wake wa kuwaangamiza madhalimu.
Na wewe ewe mwislamu popote ulipo, omba dua baada ya swala zako kwa dua ya Mtume wako aliyejikinga nayo katika wakati kama hizo, "Ewe uliyeteremsha Qurani, unayeendesha mawingu, uliyewashinda makundi, uwashinde na tunusuru dhidi yao" ...
Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.