Al-Azhar yazitakia jamii za kimataifa kuendesha mashtaka dhidi ya utawala wa kigaidi wa kizayuni kwa jinai zake kuhusu Hospitali ya Al-Shifaa

  • | Monday, 13 November, 2023
Al-Azhar yazitakia jamii za kimataifa kuendesha mashtaka dhidi ya utawala wa kigaidi wa kizayuni kwa jinai zake kuhusu Hospitali ya Al-Shifaa

 

     Al-Azhar yatoa wito kwa watu huru wa ulimwengu, mashirika na taasisi za kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuvunja mazingiwa dhidi ya Hospitali za Gaza

Pia, Al-Azhar Al-Sharif inasisitiza kuwa: utawala wa kigaidi wa kizayuni haujui thamani ya ubinadamu na uhai, na kwamba utawala huo ulitoa dalili kwa ukali wake ukijitenga mbali na maana ya rehema

Al-Azhar: kukaa kimya kuhusu  jinai za mamlaka ya kizayuni ni fedheha inayocafua taswira ya ubinadamu na jamii ya kimataifa

Al-Azhar yaeleza heshima yake kwa madaktari na wafanyakazi wote katika Hospitali za Gaza kwa kuwajibikia majukumu yao kwa ujasiri na kuwa katika mstari wa kwanza katika mapambano na juhudi za kuwahudumia majeruhi.

Al-Azhar Al-Sharif yawaita watu huru wa ulimwengu kutouunga mkono utawala huo wa kikatili.

Al-Azhar: utawala wa kigaidi unatumia nguvu yake dhidi ya watoto, majeruhi na wagonjwa, na kutekeleza jinai ambazo wanyama msituni hazifanyi.

Kwa hiyo, Al-Azhar Al-Shareif inazitakia jamii za kimataifa kuendesha mashtaka dhidi ya utawala wa kigaidi wa kizayuni usiojua maana ya ubinadamu na uhai, kwa mauaji ya kimbari na jinai za kivita unazozifanya, na hayo baada ya ugaidi wake kusababisha kuutenga ukanda wa Gaza na kuzuia mafuta na vifaa vya tiba kufikia hospitalini jambo lililopelekea idadi kubwa ya hospitali hizo kushindwa kutoa huduma, na kufa shahidi kwa idadi kubwa ya wagonjwa mahututi na vitalu vya watoto waliozaliwa kabla ya wakati katika kutoka huduma katika hospitali ya Al-Shifaa, aidha mashambulizi ya kikatili ya kizayuni kwa kusini mwa Hospitali hiyo yalisababisha kufa shahidi kwa makumi ya watu, na kuzuia kuwazika, na kushambulia kwa risasi kila anayejaribu kutoka au kuingia Hospitalini.

Pia, Al-Azhar inatoa wito kwa watu huru wa ulimwengu, mashirika na taasisi za kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuvunja mazingiwa "yasiyo ya kibinadamu" yaliyowekwa na "wazayuni wa kigaidi" dhidi ya Hospitali za Gaza na vituo vya afya, ikisisitiza kwamba kukaa kimya mbele ya jinai za hizo ni fedheha juu ya uso wa ubinadamu na jamii za kimataifa, na Al-Azhar inawashikilia wale wanaounga mkono utawala wa kizayuni au wanaonyamaza kuhusianna jinai hizo za kutisha.

Pia, Al-Azhar Al-Shareif inaamkia madaktari na wafanyakazi mashujaa wa Gaza, waliosimama katika mstari wa mbele ili kuwaokoa majeruhi, na waliosimama kutekeleza wajibu zao kwa kufanya kazi yao chini ya mashambulizi ya kinyama ya utawala wa kigaidi wa kizayuni bila ya kuogopa kufa, ikisisitiza kwamba hao wabingwa walitoa mifano ya kujitoa muhanga wakati wa uhaba mkubwa wa vifaa vya msingi vya matibabu, umeme na mafuta, jambo lililowalazimisha kutekeleza operesheni ngumu sana bila ya dawa za kutuliza akili na nje ya vyumba mahususi vya upasuaji, ikimwomba Mwenyezi Mungu awasaidie na awalinde kwa jicho lake ambalo halilali kamwe, na kuwalinda na madhara na uovu wote.

Mwishoni, Al-Azhar Al-Shareif inawaita watu huru wa ulimwengu kutouunga mkono utawala huo wa kikatili uliotoa dalili ya ukali wake na ulijitenga mbali na maana yote ya rehema, na umwagaji damu za wasio na hatia, na ukidhihirisha nguvu zake dhidi ya wanyonge wakiwemo wagonjwa, watoto, wanawake na wazee, na ulitekeleza jinai ambazo wanyama msituni hawafanyi.

 

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.