Uadui wa Kizayuni mjini Ghaza na vigezo visivyo na uadilifu

Imeandaliwa na Bw., Eslam Ragab Mohammed

  • | Friday, 17 November, 2023
Uadui wa Kizayuni mjini Ghaza na vigezo visivyo na uadilifu

 

      Kwa hakika, uadui wa kizayuni unaoendelea mjini Ghaza umeonyesha uhuru wa uwongo na viwango visivyo na uadilifu, ambapo Ulaya na nchi za kimagharibi zimetutaabisha kwa kusema mengi na kuzungumza kila wakati juu ya uhuru, sio hii tu, bali wametumia nguvu ya kiaskari kwa ajili ya kutekeleza uhuru wanaoudai katika baadhi ya maeneo katika bara la Afrika na Asia, lakini siku zimebainisha upotofu wa  madai ya Magharibi kuhusu maadili na uhuru, na hivyo katika wakati wa vita vya Ghaza

Maneno haya ya Magharibi kuhusu maadili na uhuru uliwashangaza wengi miongoni mwa wale wanaotafuta heshima na uhuru, wakati wengine wanadai kuwa ni lazima kutumia kanuni ya uhuru wa kuunga mkono haki za binadamu na kuziendeleza bila kutawanyika au ubaguzi, hivi karibuni maneno yake yamevunja, yamebadilishwa, na umeanguka kwenye ubaguzi, kwa kuunga mkono uhuru huu ikiwa kwa ajili ya faida ya kikundi Fulani tu, watu maalumu, au suala fulani, na sio wengine.

Kwa kweli, ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na nchi ya kiyahudi dhidi ya Wapalestina, kuwalenga raia wenye salama na nyumba zao, kuchukua bila haki ardhi na mali zao, kupanua ujenzi wa makazi, na kubadilisha ukweli wa kihistoria na kisheria kwa miji ya Palestina ni jambo la kuaibikia na jambo linalotia doa kwenye paji la uso wa jumuiya ya kimataifa na ubinadamu, na ukurasa mpya ya uhalifu ulioongezwa kwa kurasa nyeusi za nchi ya kiyahudi.

Kwa hivyo, Kituo cha Al- Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu kinasisitiza ulazima wa umoja wa Waarabu na Waislamu kuwaunga mkono Wapalestina na kuunga mkono suala lao na suala letu lenye haki na mapambano yao ya kisheria.

Al-Azhar Al-Sharief ina jukumu kubwa kuhusu suala la Ghaza na Al- Kudsu tangu miaka mingi yaliyopita, na wakati hivi sasa Al-Azhar Al-Sharif ilikuwa na msimamo mzuri kama kawaida dhidi ya matukio ya mwisho ya Ghaza, Ambapo Al-Azhar imelaani vikali ugaidi wa nchi ya kiyahudi dhidi ya Ghaza, kuwaua raia wa Palestina, kuwajeruhia makumi miongoni mwao, na kuwalenga watoto na wanawake wao. Al-Azhar inalaani ukimya huu wa kimataifa usio na maana na usiokubalika, ambao unailipa nchi ya kiyahudi usukumizi usio na maadili wala  ustaarabu, ili kuendelea na ukiukaji wake katika haki ya binadamu na ubinadamu, na mashambulizi yake ya mara kwa mara dhidi ya ndugu zetu wasio na hatia wa Palestina.

Na pia mfano bora wa viwango viwili vya Magharibi ni yale yaliyotokea wakati wa mgogoro wa katuni zinazoweka ubaya kwa wema wa viumbe vya Mwenyezi Mungu, Muhammad (S.A.W) pale baadhi wakaona kwamba mwandishi wa habari na gazeti lililochapisha katuni hizo wana uhuru wa kutoa maoni yao, na hawakuzingatia kuwa katuni hizo zinaweza kuwa za kibaguzi na kuwabagua Umma wa Kiislamu unaomcha mtume wake na hisia zao zinapata maumivu na udhi kwa ajili ya mtume wao! Mkanganyiko huu katika misimamo miwili iliyopita sio pekee, bali historia na ukweli wa sasa una mifano mingi inayoonyesha ukubwa wa mkanganyiko huu katika misimamo na kanuni za kundi Fulani katika nchi za Magharibi, na katika ngazi zote, zikiwemo za kisiasa. , kijeshi, kisanii, vyombo vya habari na vingine... Uchokozi unaofanywa na Mayahudi ni halali kwa sababu - kwa mtazamo wao - haki iliyopatikana na ulinzi wa ulimwengu, lakini jibu la Wapalestina ni fikra kali, ugaidi na chuki dhidi ya Mayahudi

Vilevile, kuwazuia wanawake wa Kiislamu kuvaa hijabu katika baadhi ya nchi ni haki inayolenga kupata ushindi kwa maadili ya kibinadamu ya Magharibi, kutobaguliwa kwa misingi ya dini, na uimarishaji wa misingi ya usawa baina ya watu wa nchi mmoja, na kukataliwa kwa tamaduni zinazokuja kwa nchi za Magharibi, lakini kuwajibisha walio nje ya mfumo wa maadili ya mashariki, kama vile mashoga na watu wenye fikra kali, ni uvunjifu wa maadili ya binadamu, kurudisha nyuma demokrasia na uhuru wa maoni na itikadi!

Kuna mifano mingi inayoonyesha kiwango cha kupingana maadili na kanuni za Magharibi inayojaribu kueneza nguvu zake na maadili yake juu ya wengine, bila ya kujali kiwango cha kufaa kwao kwa mujibu wa muktadha wao wa Kihistoria, kidini, kitamaduni, kisiasa na kijamii.

Kwa hivyo, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali siku zote kinasisitiza kwamba uhuru ni haki kwa wote, lakini ina mipaka. Kwani kila uhuru ina mipaka ambayo ni mila na desturi, na bila ya mipaka hizi ulimwengu utageuka kwa pori ambalo mwenye nguvu atamdhulumu mnyonge, na uhuru unatumiwa kupitisha ajenda za uharibifu zinazolenga kuharibu ulimwengu, sio kuujenga upya, na kuharibu ubinadamu, sio kuuboresha. Na kituo cha Uangalizi pia kinasisitiza kwamba ukali na kutumia nguvu katika kufaradhisha uhuru ndio ni kilele cha "Udikteta

Al-Azhar Al-Sharif inatoa rambirambi zake za dhati na kufariji kweli kwa familia za mashahidi na raia wa Palestina, akiomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape rehema na msamaha wake mashahidi wa Palestina, azizipe nguvu nyoyo za familia zao na  awape subira na faraja, na awape uponyaji na afya waliojeruhiwa, ikisisitiza umuhimu wa kueneza Amani ulimwenguni, na hivyo inabainshwa sana katika maneno ya Mheshimiwa Imamu Dk. Ahmed Al-Tayeb, Sheikh Al-Azhar Al-Sharif wakati wa Kongamano la mwisho la Bahrain, ambapo amesema kwamba Sababu ya misiba ya Mashariki na Magharibi ni kutokuwepo msingi wa haki ya kijamii, pia ameongeza akisema: "Misiba ya wanadamu inaungwa mkono na nadharia za mgongano wa ustaarabu na mwisho wa historia na utandawazi", na katika mwishao wa neno lake akatoa wito kwa ulimwengu kuweka utamaduni badala ya siasa katika uhusiano wa kimataifa.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.