Al-Azhar Al-Shareif yalaani mauaji ya shule mbili za Al-Fakhura na Tal Al-Zaatar

  • | Sunday, 19 November, 2023
Al-Azhar Al-Shareif yalaani mauaji ya shule mbili za Al-Fakhura na Tal Al-Zaatar

    Ulimwengu unaonyamaza kimya na umma wa kiarabu na wa kiislamu hazikutoa chochote cha kuwaondoa laumu mbele ya Mwenyezi Mungu kuhusu haki za Wapalestina.

Al-Azhar Al-Shareif kwa Wapalestina: msikate tamaa kwani kisasi chenu kiko kwenye Mwenyezi Mungu naye ndiye mwenye nguvu Asiyeshindwa.

Al-Azhar yatoa wito kwa watu huru duniani kufichua ugaidi wa  Wazayuni na mashambulizi yao ya kikatili dhidi ya Wapalestina.

Pia, Al-Azhar yatoa rambirambi kwa Wapalestina wenye haki na ardhi kuhusu mashahidi wao na mashahidi wetu, ikimwomba Mwenyezi Mungu azitulize nyoyo zao.

Al-Azhar Al-Shareif inasisitiza kwamba mashambulizi yanayofanywa na mamlaka ya kizayuni kwa wakimbizi wasio na hatia katika shule mbili za Al-Fakhura na Tal Al-Zaatar, yaliyosababisha kuhangaika kwa mamia ya mashahidi na majeruhi, ni jinai zisizo za kibinadamu na kimaadili, zinazoongezwa kwa historia za mamlaka hiyo ya umwagaji damu, mamlaka isiyojua maana ya ubinadamu, tabia na maadili, wala kuelewa isipokuwa mauaji, dhuluma, ubakaji na ukiukwaji wa haki za wengine.

Al-Azhar Al-Shareif inatoa wito kwa watu huru duniani kuungana dhidi ya ugaidi wa kizayuni, na wale wanaowasaidia, na ukimya wa jamii za kimataifa na uhaini wa walio karibu na walio mbali, na kusukuma kwa nguvu zao zote ili kukomesha mashambulizi hayo yanayowalenga watoto, wanawake, wazee na vijana, na kufichua jinai na mauaji haya yanayoendelea dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.

Pia, Al-Azhar Al-Shareif inatoa rambirambi zake za dhati kwa wenye haki, ardhi na suala la uadilifu, na kwa umma wa Kiarabu na wa Kiislamu na kwa ulimwengu unaokaa kimya, ambazo hazikufanya chochote na kushindwa kuwaokoa ndugu zetu katika Palestina, na hazikutoa chochote kinachowaondoa laumu mbele ya Mwenyezi Mungu na historia, ikimwomba Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi na awasamehe, na Azitulie nyoyo za Wapalestina wa uhuru, na awanusuru dhidi ya adui yao, adui yetu na adui ya ubinadamu, ikisisitiza kwamba kila ukoloni utaondoshwa, na kwamba ukoloni wa kigaidi wa kizayuni utaondoka mbali na ardhi ya Palestina, sasa hivi au baadaye, na kuwahotubia Wapalestina wasikate tamaa kwani kisasi chao kiko kwa Mwenyezi Mungu, naye ndiye mwenye nguvu asiyeshindwa.

 

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.