Wanadai .. Tunasahihisha

2

  • | Wednesday, 8 June, 2016

•    Hadithi ambayo kundi la Daesh linaitegemea katika kuthibitisha suala la kurudi kwa ukhalifa tena katika kitabu cha Imamu Ahmad Bin Hanbal cha Musnad na katika kitabu cha Musnad cha Al-Tyalisiy kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: "Mtabaki mkifuata mfumo wa utawala wa unabii kama anavyotaka Mwenyezi Mungu, kisha Atauinua  akitaka kuuinua, kisha utakuwa ukhalifa kwa mujibu wa mbinu ya Mtume, basi utadumu kwa muda kama Atakavyotaka Mwenyezi Mungu, kisha Atauinua Akitaka kuuinua, kisha utakuwa ufalme imara, utakaodumu kama Atakavyotaka Mwenyezi Mungu, kisha utakuwa    جَبْرِيَّةً ambapo utadumu kama Atakavyotaka Mwenyezi Mungu, kisha Ataiinua Akitaka kuiinua, kisha utakuwa ulhalifa kwa mujibu wa mbinu ya Mtume", akakaa kimya".


•    Waelezaji wa hadithi hiyo walisema kuwa ukhalifa ambao utafuata mbinu ya Mtume uliotajwa katika hadithi ni ule ukhalifa utakaokuwepo mwishoni mwa zama ambapo Nabii Issa (A.S.) atateremsha pamoja na kujitokeza kwa Mahdiy anayengojewa kwa mujibu wa maoni ya walioeleza hadithi hiyo.


•    Hadithi hiyo haina uagizo wa ukatazo, kwa maana ya kwamba haina makalifisho kwa kitu maalum, bali ni taarifa tu, ambapo ye yote anayedai kwamba kwa kutangaza kusimamisha ukhalifa na matokeo hatari yake ameshatekeleza wajibu alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu, basi je, Mwenyezi Mungu alimkalifisha kufanya hayo? Na alikuja kwa wajibu kutoka wapi hasa? Au atabainika kwamba yeye ni mwongo anayefasirisha matini za kisheria kinyume na ukweli wake.


•   Kundi la Daesh halikuanzisha mfumo wa ukhalifa kutokana na mbinu ya Mtume (S.A.W.), bali walianzisha ukhalifa kutokana na mbinu ya umwagaji damu, vurugu, na ukatili bila ya kujali heshima ya mwanadamu ye yote, hawakuzingatia mkungwe wala mzee wala hawakulazimika kwa mbinu ya Mtume (S.A.W.) kuhusu kutendeana na wasio waislamu, bali walifuata mbinu ya ukafirishaji ambao Mtume (S.A.W.) aliueleza kwa kusema: "Msirudi makafiri baada ya kufariki kwangu mkipigana wenyewe kwa wenyewe". Matini hiyo huwa dalili mojawapo dalili zisizo na mfano zinazothibitisha ukweli wa unabii wake (S.A.W.), basi hayo ndiyo makundi ya kiislamu yanawaita waislamu kuwa ni makafiri yakawaagiza kuuawa, kisha yakajigombana katika mafungu ambayo kila fungu linalikafirisha jingine wakapigana.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.