Wanadai .. Tunasahihisha

3

  • | Wednesday, 8 June, 2016

•    Mfumo wa utawala katika Uislamu hutegemea hali ya watu na desturi zao kwa sharti ya kutokuwa na sheria inayopinga sheria ya Mwenyezi Mungu (S.W.) ambapo haikujitokeza matini wazi sahihi hata moja inayowalizimisha waislamu kupitisha mfumo maalum wa kisiasa kwa maelezo yake hasa, bali ilijitokeza ulazima wa uadilifu na kuzichunga maslahi za waja na nchi kwa namna itakayomridhi Mola wa watu.


•   Mifumo yote ya kisiasa iliyokuja baada ya zama za makhalifa waongofu Abu Bakr, Omar, Othman, Ali na Al-Hassan Bin Ali mifumo hiyo haiitwi ukhalifa ila kutokana na mtazamo wa kilugha ama kwa upande wa ukweli wake basi mifumo hiyo ndiyo mifumo mbali mbali ya utawala jambo linalothibitisha kwamba mifumo ya utawala inatofautiana katika Uislamu kutokana na tamaduni, mila na desturi na hali za mambo.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.