Al-Azhar yaamkia juhudi za Misri na Qatari zilizopelekea kusitisha mapigano huko Gaza

  • | Wednesday, 22 November, 2023
Al-Azhar yaamkia juhudi za Misri na Qatari zilizopelekea kusitisha mapigano huko Gaza

     Al-Azhar inatoa wito kwa waadilifu wa Waislamu, Wakristo na Mayahudi ili kuendelea kuwasukuma Viongozi na watawala ili kukomesha uadui wa kizayuni dhidi ya Ghaza.

Pia, Al-Azhar Al-Shareif inathamini juhudi za Misri na Qatari zilizopelekea kusitisha mapigano na uadui dhidi ya ndugu zetu katika Ukanda wa Gaza, na kuhakikisha kuwa misaada ya kibinadamu inafika kwa wakati kwa familia zetu katika Ukanda wa Gaza, ikimwomba Mwenyezi Mungu kwamba hatua hiyo kupelekea kukomesha kabisa uadui wa kikatili dhidi ya wenye ardhi na haki.

Al-Azhar Al-Shareif inathamini msimamo wa watu wote walio huru duniani, wakiwemo Waislamu, Wakristo, Mayahudi na wengineo waliotoka barabarani ili kutangaza kukataa uadui dhidi ya raia wasio na hatia mjini Gaza, wakiunga mkono haki za Palestina na kukemea vitendo vya mamlaka ya kikatili ya kizayuni na unyama wake dhidi ya watoto, wanawake, wazee na wasio na hatia, na kukataa kuzilenga hospitali, makanisa, nyumba na makazi kwa wakimbizi.

Aidha, AL-Azhar Al-Shareif inahimiza sauti zote zilizo huru kwani zilielezea msimamo wao kwa ujasiri mkubwa, na umuhimu wa kuwasukuma na kuwahimiza viongozi na watungaji sera wa kimataifa ili kumaliza kipindi hicho kinachozingatiwa kuwa aibu na fedheha kwa ubinadamu wote.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.