Nafasi ya Mwanamke katika Kujenga Jamii

Imeandaliwa na Dkt.; Alaa Salah Abdulwahed

  • | Thursday, 23 November, 2023
Nafasi ya Mwanamke katika Kujenga Jamii

    Mwenyezi Mungu Amewaumba wanadamu katika jinsia mbili; wanaume na wanawake kwa hekima ya kukamilishana na kuungana, ambapo kila mmoja wao huwa na wajibu na majukumu maalumu katika jamii huku mwenzake anawajibika wajibu na majukumu yannayokamilisha jukumu la kujenga jamii na kuunda umma.
Inafahamika kwamba mwanamke ana nafasi kubwa katika jamii, mpaka huitwa "Nusu ya Jamii", ambapo mwanamke amepewa nafasi, majukumu na cheo anachoshirikiana na mwanamme kutakeleza wajibu wake, kwani mwanamke anamsaidia mwanamme maishani. Kwa hiyo, Uislamu inamheshimu mwanamke na kumpa nafasi ya juu, kwa kuwa huwa sehemu ya maisha samabamba na mwanamme.
Kwa kuangalia hali ya mwanamke enzi za Jahiliya kabla ya ujio wa Uislamu na hata katika enzi za Warumi na Wayunani tunaona namna watu wa enzi hizi walikuwa wanamzingatia mwanamke kati ya vitu vya anasa na vifaa vinavyotumika nyumbani, kwa hiyo hakuwa na haki yoyote, ambapo mke anayefiwa na mumewe alikuwa halali kwa ukoo wake bila ya kuomba ridhaa yake. Imamu Al-Bukhariy alisimulia kuwa mwanamke wa enzi hizo hakuwa na haki ya kuchagua mumewe na hasa aliyefiwa na mumewe basi ukoo wake walikuwa wanashauriana akitaka mmoja wao kumwoa, au pengine kumwolewa kwa mwingine au kumzuia asioe, maana wao peke yao wanao haki ya kuainisha hatima yake kuliko yeye mwenyewe wala ukoo wake.
Pia, desturi za Waarabu kabla ya Uislamu zilikuwa zinawaruhusu kumshutumu mwanamke ambaye hawamtaki tena kwa zinaa ili aogope fedheha ambayo haipo kabisa na kulipa mahari aliyopewa kwa ajili ya kupata uhuru wake. Mwenyezi Mumgu Amesema kukataza haya: {Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa - isipo kuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake * Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi? * Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?} [An-Nisaa: 19-21].
Uislamu ilipokuja hali ya mwanamke imebadilika, ambapo mwanamke ametukuzwa akapewa haki zake akiwa sawa sawa na mwanamme kuhusu majukumu ya maisha ambapo kwa mtazamo wa Uislamu mwanamke ndiye msaidizi wa mwanamme na mwanamke bora zaidi ni yule anayemsaidia mumewe kuwajibika majukumu ya maisha, kama Mwenyezi Mungu (S.W.) Alivyoeleza sifa za mwanamke bora katika kauli yake: {Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu} [An-Nisaa: 34].
Haya kwa mwanamke ambaye ni mke, ama kuhusu akina mama kweli Uislamu ilimtukuza sana mama ikawaamrisha wanawe wamtii na kuomba radhi yake wala wasimkasirishe na kubainisha kuwa ridhaa ya wazazi na hasa mama ni njia mojawapo njia za kupata radhi ya Mwenyezi Mungu na baraka dunaini na malipo mema Akhera; yaani Pepo. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu,na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapofika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu} [Al-Ahqaf: 15].
Inabainika kutokana na dua hii iliyotajwa katika aya tuliyoitaja kwa wazazi wawili kisha kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu kuitengeneza dhuriya na kuunganisha hii na kumtaja mama peke yake na kumtilia mkazo ni kwa sababu ya kuonyesha kuwa ana nafasi mkubwa mno na taabu anazozipata kuanzia ujauzito kisha kujifungua kisha unyonyaji kisha malezi na anaendelea kuwalea wanawe hata baada ya wafike utu wao mzima. Hayo yanaashiria kuwa Uislamu imemtukuza mama ikikiri fadhila zake na mchango wake ikijikita pia nafasi yake kuwalea wanawe kwa kujibu wa misingi ya malezi mema iliyopitishwa na Uislamu, jambo linalochangia kukiandaa kizazi cha waislamu wanaolazimika kufuata njia iliyonyooka wakishikilia tabia njema kama walivyolelewa na mama zao.
Kwa kutambua nafasi ya mwanamke katika jamii Uislamu umesisitiza umuhimu wa kuchagua mke bora kwa kuwa yeye ndiye nguzo wa msingi wa familiya yote, pia yeye ndiye anayeweza kuathiria sana kizazi kwa malezi, ambapo anatarajiwa kuwa mama mlezi anayewasaidia wana wake kuwa kizazi chema na watoto wenye tabia na maadili mazuri. Kwa kuainisha sifa muhimu za mwanamke, Mtume (S.A.W.) amebainisha kuwa sababu na vidhibiti vya kumchagua mke ni: “Mwanamke huchaguliwa kuolewa kwa kuzingatia utajiri wake ama ukoo wake ama uzuri na urembo wake ama dini yake, basi chagua yenye dini ni bora kwako”. Na katika hadithi nyingine iliyosimuliwa na Abdullah bin Omar bin Al-As (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) amesema: “Dunia ni anasa na anasa bora zaidi katika dunia hii ni mke bora”. Al-Hassan alijiwa na mtu akasema: Ewe Hassan binti yangu ameombwa kuolewa na wanaume wengi, basi ni nani nimkubali awe mumewe?! Akasema: aliye mcha Mungu kwani akimpenda atamkirimu na kumtunza na akimchukia hatamfanyia dhuluma”.
Kutokana na hayo wataalamu wa malezi wanaona kuwa mchango wa mke na nafasi yake kujenga familiya ni kubwa zaidi kuliko mchngo wa mume kwa kuwa yeye ndiye huambatana na mtoto wajati wote tangu alipokuwa mimba tumboni mwake mpaka awe mtoto mchanga kisha mtoto halafu kijalunga halafu kuwa kijana na kuendelea. Mtume (S.A.W.) alipokuwa anawahotubia vijana kuwajimiza kuoa aliwaambia kuwa ndoa ni kutoka Sunna yake akikusudia kumwoa mke bora anayewajibika maamrisho na makatazo ya sheria ya kiislamu, akibinisha faida na umuhimu wa ndoa kwa kusema: “Enyi Vijana! Yeyote anaye uwezo wa kuoa basi aoe kwani hii ni bora kuhifadhi tupu na kulinda macho, ama asiye uwezo huu basi hutakiwa kufunga saumu kwani ni himaya yake kutokana na makosa”
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.