Kwa mujibu wa maelekezo ya Sheikh_wa_Al Azhar.. msafara wa tatu wa misaada wapita bandari kavu ya Rafah ili kuwaunga mkono ndugu zetu wenyeji wa Gaza

  • | Tuesday, 28 November, 2023
Kwa mujibu wa maelekezo ya Sheikh_wa_Al Azhar.. msafara wa tatu wa misaada wapita bandari kavu ya Rafah ili kuwaunga mkono ndugu zetu wenyeji wa Gaza

     Msafara wa tatu wa misaada unaotoka Baiti ya Zaka na Sadaka ya kimisri ulipita leo jumanne bandari kavu ya Rafah ili kuingia ukanda wa Gaza kwa ajili ya kuwaunga mkono na kuwasaidia familia na ndugu zetu huko Gaza, ukiundwa na lori 17 zilizojazwa dawa, chakula na misaada zinazohusiana na siku za baridi.

Inatajwa kuwa huo ni msafara wa tatu wa misaada unaopelekwa na Baiti ya Zaka kwa mujibu wa maelekezo ya Sheikhi wa Al-Azhar, msimamizi mkuu na Mwenyikiti wa baraza la Bait Al-Zaka na Sadaka ya kimisri, na msafara huo ni sehemu ya shughuli za kampeni iliyoanzishwa na Al-Azhar Al-Shareif kwa anuani: "Waokoeni wananchi wa Gaza", ambapo misaada iliyopelekwa na Baiti ya Zaka na Sadaka ya kimisri kwa familia na ndugu zetu huko Gaza ilifika lori 75 zilizojazwa dawa, chakula na misaada kwa wakimbizi.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.