Ugaidi wa Kifikra .. Dhana yake, Chanzo chake na Namna ya Kujikinga nao

Imeandaliwa na Dkt.; Alaa Salah Abdulwahed

  • | Friday, 1 December, 2023
Ugaidi wa Kifikra .. Dhana yake, Chanzo chake na Namna ya Kujikinga nao

     Ugaidi wa kifikra inamaanisha kuwa mtu mmoja au zaidi au makundi kujaribu kuwalazimisha watu au mataifa au nchi fikra, maoni au madhehbu maalumu kwa nguvu, na kwa kutegemea mbinu kali badala ya kutumia mbinu zinazokubalika kama vile; mazungumzo na njia nyinginezo za kistaarabu. Watu hao au makundi hayo wanajaribu kuwalazimisha wengine kufuata fikra maalumu kwa nguvu kwani wanadai kwamba wapo wengi wanaokuja na ukweli na haki, na kuwa wengine wanaopinga maoni yao hawapo sawa hata wakiwa wengi kuliko wao. Makundi haya wanajidai haki ya kuwaongoza na kuwatawala wengine pasipo na sababu au mantiki yoyote. Kwa hakika ugaidi wa kifikra au wa kiitikadi ulianza hapo zamani sambamba na kuumbwa kwa mwanadamu, ambapo tangu mwanadamu alipoanza kuishi ardhini, hali hiyo ilijitokeza ikiambatana na mwenendo wa baadhi ya wanadamu na itikadi zao, hata hivyo kuwepo kwa wanadamu kumepita kiasi cha miaka maelfu, ugaidi huo ungalipata mashabiki wake japokuwa hatari na maovu yanayosababishwa na hali hii na madhara yanayoziathiria vibya ustaarabu wa kibinadamu.

Kwa hakika ugaidi wa kifikra na wa kiitikadi hauhusiani na dini mmalumu, bali magaidi wapo katika wafuasi wa dini tatu za mbinguni ambazo ni pamoja na Uyahudi, Ukristo na Uislamu, isitoshe, bali ugaidi wa aina hii upo katika dini zilizotungwa na mwanadamu. Kwa hivyo, haikubaliki kuituhumu dini moja kuwa ni msingi wa ugaidi bila ya kuangalia hali ya mambo katika dini nyinginezo, ambapo kila dini ina baadhi ya wafuasi wake walioshawishiwa kuwa magaidi wakajiunga na fikra hizo. Mafundisho ya kiislamu yaanpingana kabisa na ugaidi wa kifikraUislamu ndio dini ya rehma, usamehevu na ukati na kati, kwa hiyo umma wa waislamu wa Mtume Mohammed (S.A.W.) umesifika kuwa mbinu yake ni ya ukati na kati, jambo Alilolisisitiza Mwenyezi Mungu (S.W.) Aliposema: "Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wawasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume aweni shahidi juu yenu" [Al-Baqarah: 143]. Kwa hivyo, Uislamu ndiyo dini ya ukati na kati katika mambo yote ya dini na hata dunia, dini hiyo haikutambua wala kujua ugaidi hata kidogo, vurugu au ulazimisho wa kifikra au kimadhehbu. Mtume (S.A.W.) amekataza ushadidi, kufuata siasa kali kuhusu masuala ya dini, ambapo alisema katika hadithi iliyosimuliwa na Ahmad na wengine, kuwa Mtume (S.A.W.) amesema: "Tahadhareni wala msishadidisha katika dini, kwani waliokuwa kabla yenu waliangamizwa kwa sababu ya kufanya hivyo".

Kwa kutaka kueleza zaidi tena kwa uwazi na uadilifu, tunabidi kutafautisha baina ya mwenye fikra sawa na mwenye fikra kali, kanuni na vidhibiti vya kutafautisha baina ya mwenye fikra kali na asiye na fikra hizo ni kwamba mwenye fikra zilizo sawa na za ukati na kati hukubali maoni mbali mblai bila ya kukataa mitazamo inayotofautiana na maoni yake, wala hadai kuwa yuko sahihi wakati wote, bali husema: maoni yangu ni sahihi na pengine huwa kosa wakati ambapo maoni ya wengine ni kosa inayoweza kuwa sahihi, ama mwenye fikra na misimamo mikali hukataa maoni na mitazamo ya wengine, akidai kuwa maoni yake yako sahihi wakti wote, na kuona kuwa maoni yake ni sahihi yasiyo na shaka hata kidogo, na kwamba maoni ya wanaotofautiana na maoni yake ni kosa kabisa.

Tukiangalia chanzo kilicho muhimu zaidi cha ugaidi wa kifikra tutatambua kuwa ujinga ndio chanzo cha msingi cha ugaidi wa aina hiyo, na sio ujinga kwa jumla, bali ujinga kwa mambo, hukumu na masuala ya dini, pamoja na kutotafautisha baina ya matini Alizoziteremsha Mwenyezi Mungu na matini zilizotungwa na maulamaa, jambo linalosababisha kukosa kuelewa ukweli wa mambo yalivyo, zaidi ya hayo kutofahamu vyema baadhi ya istilahi za sheria kama vile; Jihad, Ukufurishaji, Shahada, Walaa na Baraa, Kutii na Kuasi na kadhalika. Ufahamu mbaya wa istilahi hizo na nyinginezo huwapelekea kuwa na makosa mengi na kutoa hukumu hatari zisizoambatana na sheria hata kidogo, hivyo wakazitegemea hukumu hizo kufanya jinai, maovu na halifu kwa kudai kuwa wako sawa, licha ya kuzingatia jitihada za baadhi ya maulamaa ni matini ambazo hazikubali shaka wakivuka mipaka na kuzifanya matini na hukumu hizo ni sawa sawa na matini takatifu za Mwenyezi Mungu, na kwamba jitihada hizo ni dini isiyokubali kujadiliwa.

Watu hao wanaofuata ugaidi na upendeleo wa kifikra bila ya kuwa na msingi wa elimu yoyote, wanatetea maoni ya maulamaa kama wanavyotetea matini ya Mwenyezi Mungu, jambo linalosababisha vurugu na upendeleo kwa madhehebu au kwa dini, kisha mambo yanazidi kuwa tishio kwa kufanya uadui au kufanya kabisa dhidi ya nchi na taasisi zake na hata dhidi jamii, hali iliyopo katika nchi kadhaa za kiislamu. Kwa kweli vitendo hivyo haviafikiani na Uislamu kabisa, kwani dini hiyo takatifu inategemea uadilifu, usawa, uwiano na ukati na kati, wala haitegemei ugaidi, ukabila, vurugu wala uchochezi wa fitina na kuungana na ubatilifu. Mtume (S.A.W.) ametutahadharisha kutokana na watu hao akisema: "Mwishoni wa zama, watajitokeza watu, wengi wao ni vijana, hawana malengo ya kuhudumia dini, wanasema maneno mazuri kama ninayoyasema, wanasoma Qurani bila ya kuelewa chochote, bali wanasoma tu pasipo na kutambua hata kidogo, wanatoka kutoka dini kama unavyotoka mshale kutoka mnyama anayewindwa, basi mkiwakuteni muwaueni, kwa hakika kuwaua watu hao ni jambo la lazima na lenye thawabu kwa yule atakaewaua" Imesimuliwa na Ahmed na An-Nasaiy na wengine.

Ama kuhusu namna ya kujikinga na ugaidi wa kifikra, basi huwa kwa njia ya kudhihirisha na kushikimana na uwastani wa Uislamu na uwiano wake, na kujitahidi sana kuimarisha na kueneza hisia za kujifungamana na dini na nchi kwa vijana. Aidha, kuzitambua fikra kali na kuwaokoa vijana kutokana na misimamo mikali na maoni maovu, kwani vijana wangeelewa na kufuata fikra na maoni yaliyo sawa wangeshughulikia yanayowanufaisha wao na jamii zao, na kuepukana na yaletayo madhara, haya yote yafanywe kupitia kwa familia, taasisi za kiilemu, misikiti, kazi, vyombo vya habari kwa aina zake zote. Inakumbukwa kwamba kuwakinga vijana kutokana na fikra kali hakufikiki ila baada ya kufahamu vyema dhana ya upotofu wa kifikra na misingi ya ugaidi na sababu zake namna inayofaa kupambana nao.

Na shughuli ya kupambana na ugaidi wa kifikra ingalianza mapema, ingalikuwa na manufaa makubwa, pamoja na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo na kushauriana kama ni suluhisho lenye athari kubwa kumaliza hali hiyo, ambapo mazungumzo ni mtindo na mbinu unaofaa kuunda dhana sahihi na kubainisha haki na kudhihirisha ufisadi wa baadhi ya itikadi, tuhuma na fikra, pamoja na kunufaika na wanavyuoni wa sheria, wataalamu wa kisaikolojia na kijamii, kwani wana elimu, maarifa na uzoefu.

Kwa hiyo, wanaweza kuwakinaisha wale walioathirika kwa fikra za kigaidi, na kurekebisha istilahi potofu na maoni mabaya waliyo nayo kuhusiana na familia, jamii na nchi nzima. Mashirika, Taasisi na mamlaka watakiwa kupambana na magaidi hawa, kwa lengo la kufanya hivyo ili wale ambao wameshawishiwa kuharibu nchi, kufanya vurugu na mauaji, kusababisha ghasia na uharibifu wa aina yoyote waelewe kuwa wanafanya hatia kubwa zilizokatazwa katika sheria ya kiislamu.

  

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.