Pembeni mwa Mkutano wa COP28.. Al-Azhar yatoa wito kwa wanadamu kusimamisha mauaji ya kigaidi

  • | Sunday, 3 December, 2023
Pembeni mwa Mkutano wa COP28.. Al-Azhar yatoa wito kwa wanadamu kusimamisha mauaji ya kigaidi

     Kutoka ujumbe wa Imamu Mkuu kupitia mtandao wa X kwa mnasaba wa mkutano wa COP 28 unaofanyika nchini Falme za Kiarabu:

Ninatuma wito, bali kilio kutoka kwa mwislamu wa kawaida, ambaye anaugua uchungu kwa ajili ya wanyonge, masikini, na wasio na msaada, ni kilio cha mwanadamu anayeshangazwa na tishio la mashine ya mauaji ya kigaidi inayotekelezwa na wenye mioyo migumu dhidi ya raia wenye amani wakiwemo wanawake, wanaume, watoto, watoto wachanga, na watoto wachanga waliozaliwa kabla ya wakati, na kwa ajili ya maonyesho ya vurugu, hujuma na uharibifu ambao ardhi ya Palestina iliyoporwa inayashuhudia...

Ninauambia ulimwengu wote: umewadia wakati wa kukomesha vita hivi vya kutisha na vya uhalifu, na ninasisitiza kwamba ikiwa vita vitaendelea kama hayo - Mungu apishe mbali – basi hatutaachwa na mazingira tunayoweza kuyahifadhi, au kuweka safi kwa hali ya hewa kwa ajili ya watoto na vizazi vyetu katika siku zijazo za karibu au mbali.

Kutoka kwa hotuba ya #Sheikh wa Al-Azhar wakati wa kusainiwa kwa "Wito wa Dhamiri": Taarifa ya Pamoja ya Dini Mbalimbali ya Abu Dhabi kwa ajili ya Hali ya Hewa, na ufunguzi wa Banda la Dini Mbalimbali katika #COP28.

 

 

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.