Nafasi ya Ushirikiano wa kijamii katika kupambana na Vurugu na fikra potofu

imeandaliwa na Dkt., Alaa Salah Abdulwahed

  • | Thursday, 7 December, 2023
Nafasi ya Ushirikiano wa kijamii katika kupambana na Vurugu na fikra potofu

     Ushirikiano wa kijamii unamaanisha kuwa wanajamii wote wasiadiane na kukamilishane kwa ajili ya kuondoa na kuyatatua matatizo hasa ya wenye shida, wanyonge, maskini n.k.

Tabia ya kushirikiana na kusaidiana ni msingi mmoja wapo misingi ya jamii imara, kwa hiyo Uislamu wakati wa kugusia suala la kuanzisha jamii ulisisitizia sana tabia hiyo kwa kutambua kwamba jamii imara inatakiwa kuwa na mshikamano baina ya wananchi wake. Pia, Uislamu unasisitiza kuhurumiana na kuheshimiana baina ya watu wote si waislamu tu, bali dini hii inajali sana heshima ya mwanadamu na haki yake ya kuishi kwa amani na utulivu.

Dalili za kuthibitisha uangalifu wa Uislamu kwa ushirikiano wa jamii ziko tele lakini zote zinasisitiza ukweli mmoja nao ni kwamba wanadamu wote wanatakiwa kuwa na umoja na usawa, pia mafunzo ya kiislamu yanawaelekeza waislamu wawe pamoja kupambana na matatizo yao ya kijamii kama ulivyo mwili mmoja kama kiungo kimoja kinaumwa, mwili mzima huwa na maumivu.

Mtume (S.A.W.) alieleza umuhimu wa kushirikiana baina ya wanajmii moja kwa kusema: “Hakika mfano wa waumini kushikamana na kushirikiana na kuwa pamoja ni kama unavyokuwa mwili mmoja ikitukia shida au maumivu kwa kiungo kimoja mwili mzima huumwa”.

Kwa kweli ushirikiano wa kijamii na kusaidiana baina ya wanajamii moja huwa katika sehemu mbili kuu; ushirikiano wa maana na ule wa mada, kwa maneno mengine ni ushirikiano wa kifedha na usio wa kifedha.

Kuhusu ushirikiano usio wa kifedha ni ule msaada ambao mtu anatoa kwa mwenzake katika jamii kwa kumsaidia kwa hisia nzuri na kumdhihirishia heshima na upendo na kuwa naye wakati wa furaha na wakati wa huzuni, kumwunga mkono akiwa mkweli na kumrekebisha akikosa kumsaidia afikie malengo yake na kumrahisishia matamanio yake.

Ama ushirikiano wa kifedha ni ule msaada unaotokana na kumpa hela kwa yule anayehitaji hela hizo na kuwasaidia maskini na wasio na mapato ili wawe na maisha mazuri na ushirikiano wa aina hii unatakiwa kutoka wanao uwezo wa kifedha kuwasaidia wanyonge wasio na uwezo huo, kwa hiyo Zaka ambayo ni nguzo moja wapo nguzo za Uislamu inalengea kuufanya ushirikiano huo wajibu na haki inayotakiwa kutoka matajiri wa jamii kwa maskini wa jamii hiyo.

Mwenyezi Mungu Amewavutia waumini kwa tabia ya kusaidiana kifedha katika aya nyingi za Qurani Takatifu: {Si juu yako wewe kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na kheri yoyote mnayo toa ni kwa nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa kutafuta wajihi wa Mwenyezi Mungu. Na kheri yoyote mtakayo toa mtalipwa kwa ukamilifu, wala hamtadhulumiwa} [2/272].

Vile vile, Uislamu ulihakikisha kuwa mali si milki ya watu maalumu katika jamii ilhali wengine hufa njaa, bali mali zote ni kutoka Mwenyezi Mungu kwa hiyo inatakiwa kuwa na manufaa kwa jamii yote bila ya kumbagua yeyote.

Mpaka mapato na mali ambazo waumini walikuwa wanaishinda katika vita hazikuwa milki hasa kwa wapiganaji tu, bali kwa jamii nzima waliopigania na wasiopigania, hayo yameelezwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu} [59/7].

Kwa kweli tabia ya kusaidiana na kushirikiana katika sheria ya kiislamu imehimiziwa sana kwa kuwa mtu yeyote hawezi kuishi peke yake mbali na watu pasipo na kuwa na haja ya wengine, kimaumbile watu wanahitaji kusaidiana katika mambo yao yote ya maisha, pia shida na matatizo mbalimbali yanatatuliwa kwa njia ya ushirikiano na kusaidiana, ama wale wanaodhani kuwa hawana haja ya watu wamejihumumia vibaya kwa kuwa hakuna yeyote asiye na haja ya wenziwe kwa njia au nyingine.

Kuenea kwa ushirikiano katika jamii husaidia kimarika kwa jamii hiyo na kufikia maendeleo na mkafanaikio tarajiwa, ilhali jamii ya wanaojipenda wenyewe tu ni jamii ambayo haitakuwa na umri wala nguvu tena husambaratika na kuharibika kirahisi sana.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.