Wanadai .. Tunasahihisha

5

  • | Friday, 10 June, 2016

• Hawakuchukua shauri la ye yote isipokuwa kikundi cha jamaa zao wasiowakilishi kabisa maoni ya umma ambao idadi yake ilikaribia bilioni mbili katika ulimwengu kote, kisha tukikubali kwamba walichukua shauri la wakuu wa umma basi jambo hilo halitukia ila katika maeneo maalum nchini Iraqi na Syria sio katika nchi zote, vile vile makundi ya kiislamu wanaokuwepo nchini hizo mbili yanapigana wenyewe kwa wenyewe, je ukhalifa gani huo tena?
• Zaidi ya hayo, watu hawa waliotoa Baiyaa wakihofia kuuawa au kuadhibiwa au kutiwa mashakani maishani mwao basi Bayaa yao haizingatiwi kwa sababu ya wametoa Bayaa kwa ulazimisho sio kwa hiari, jambo lililotokea katika maeneo mengi miongoni mwa maeneo yaliyokaliwa na wapiganaji wa kundi hilo.
• Kwa kweli wale madaesh hawatambui dini ya Uislamu japokuwa wanajinasibisha kwake na kuzungumzia kwa jina lake wakificha maovu yao nyuma yake wakafedhehewa na Mwenyezi Mungu (S.W.) ambapo Alibainisha ujinga n auwongo wao kwani Mwenyezi Mungu hukataa kwa nuru yake izimwe.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.