Usamehevu wa Uislamu na maadui na haki za mateka wakati wa vita

Imeandaliwa na Dkt.; Alaa Salah Abdelwahed

  • | Thursday, 14 December, 2023
Usamehevu wa Uislamu na maadui na haki za mateka wakati wa vita

     Kwa hakika tuliyoyaona kupitia mitandao siku za hivi karibuni kuhusu namna ya kuamiliana na mateka wa kiyahudi kulingana na ukatili wa kizayuni dhidi ya mateka wa kipalestina na watu wasio na hatia, yanatudhirisha namna Uislamu unavyohimiza wafuasi wake wawe na usamehevu na watu wote mpaka maadui na kutowaruhusu wapiganaji waislamu kufanya khiyana wala ukatili. Uislamu ni dini ya usamehemvu na wanadamu wote, bali na viumbe wote mpaka wanyama na vitu visivyo na uhai.

Sheria ya kiislamu inawatakia waislamu wote walazimika kwa miamala mazuri katika hali zao zote na pamoja na watu wote bila ya kujali tofauti yoyote kidini, kimila, kikabila au yoyote nyingine. Kwa kuwa Uislmau unazingatia sana kueneza tabia njema na kutangaza kuwa ni dini ya msamaha, upendo na amani waislamu wanapaswa kuwa mabalozi wa dini hiyo wakiwajibikia mafundisho yake na tabia zake mabazo zote zinalenga kueneza amani, utulivu na rehma kwa hiyo, Mtume (S.A.W.) alipotaka kufupisha ujumbe wake alisema: “Kwa hakika nimetumwa kwa ajili ya kukamilisha tabia njema” na alijisifu kwamba: “Hakika mimi ni rehma iliyotozwa kwa wanadamu na Mola wao”.

Kwa namna hii tunaona vipi Qurani Takatifu imesisitiza umuhimu wa kushirikiana baina ya wanadamu wote waislamu na wasio waislamu na kuzingatia husiano na mambo ya pamoja yaliyopo baina ya wanadamu kwa jumla. Pia, Qurani ilisisitiza kuwa ni muhimu sana wanadamu waelewana na kukamilishana kuimarisha na kukuza jamii na nchi mpaka ulimwengu mzima. Kueneza amani, usalama, kuheshimiana, kuhurumiana, kubadilishana manufaa, uzoefu na tamaduni yote haya ni mambo yanayotakiwa kuwa msingi wa ushirikiao baina ya watu kwa ajili ya kuhudumia ubinadamu. Uislamu ulihakikisha maana hii na kuthibitisha umuhimu wa kuimarisha mahusiano ya waislamu na ulimwengu kote, kwa kuwa dini hii ni dini ya mwisho na ujumbe wake ni kwa malimwengu yote na Mtume wake ndiye wa mwisho aliyetumwa kwa watu wote.

Kwa mujibu wa mafunzo ya sheria ya kiislamu kuhusu kuwasiliana na kushirikiana na wanadamu wote, waislamu wakiongozwa na Mtume (S.A.W.) walijitahidi sana kuwa na uhusiano mzuri na ulimwengu mzima. Kwa kuhakikisha lengo hili Mtume (S.A.W.) alifanya juhudi nyingi na kachukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kufikia lengo hili. Miongoni mwa juhudi za Mtume kusaini mikataba ya amani na waliokuwa maadui wake washirikina na mayahudi kwa lengo la kuweka misingi ya kuishi pamoja kwa amani na kushirikiana kuendeleza Madinah na kukamilishana kupata mafanikio na ustawi.

Ile mikataba na maazimio yalikuwa katiba na ahadi ambayo Mtume alitoa kwa wasio waislamu ili wawe na matumaini kuhusu maisha yao katika dola ya kiislamu, ambapo aliwapa amani na kukubali masharti yao mpaka waislamu walikuwa wanadhani wakati mwingine kuwa baadhi ya mikataba hiyo inawadhulumu waislamu kama ilivyotukia wakati wa kuafikiana kwa azimio lililoitwa “Suluhu la Al-Hudaybiya” ambayo Mwenyezi Mungu Ameliita “Ushindi mkubwa” Alizungumzia azimio hilo kwa kusema: {Hakika tumekufungulia Ushindi wa dhaahiri * Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika Njia Iliyo Nyooka * Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu} [48/1-3].

Siyo maazimio tu, bali misafara ambayo Mtume (S.A.W.) alikuwa anaituma kwa lengo la kujuana na kubadilishana maarifa na mataifa wengine, ambapo kuanzia mwaka wa saba baada ya Hijra yake Mtume alituma na kupokea misafara kadha wa kadha na alikubali zawadi za mfakme wa Uhabashi “Al-Najashiy” na aliwafanyia wajumbe wake ukarimu mkubwa kwa waliyoyafanya na waislamu waliohamia Uhabashi katika Hijra ya kwanza. Vile vile, Mtume aliku Zaydu bin Thabit ajifunza lugha ya mayahudi kwa lengo la kutambua nia na mipango yao na kwa kuwasiliana nao ikitukia dharurua ya hayo.

Kwa kuangalia historia ya ustaarabu wa kiislamu tunaweza kuelewa namna dini hiyo ilivyokuwa mfano bora wa kushirikiana na wengine na kubadilishana heshima na huruma na manufaa, ambapo wislamu walitoa mifano mizuri kwa hali ya kuishi pamoja na wengine kwa amani, siyo hii tu, bali kukamilishana nao kujenga nchi na kuendeleza jamii. Usama bin Munqidh anasimulia kuwa waislamu walikuwa na harakati za kukamilishana na kusaidiana na wengine bila ya kujali dini wala kabila wala rangi. Dalili nyingine iliyo wazi kwamba kuenea kwa Uislamu kumesababishwa sana na harakati za waislamu wafanyibiashara waliokuwa wakizunguka huko na huko wakilazimika kwa mafundisho na maadili ya Uislamu, jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa kueneza Uislamiu na kuwavuta watu wajiunga nayo.

Pia, historia inatwambia na kutupa sura nyingine ya kuelezea hali ya Uislamu kushirikiana na wengine katika nyanja mbalimbali hasa biashara mpaka wakati wa vita, hali ilivyokuwa baina ya waislamu na wasio waislamu kutoka Ulaya na pengineko ambapo mikataba na biashara zilifanywa baina ya pande mbili japokuwa vita.

Uislamu ulisisitiza katika matini nyingi za Qurani na Sunna kuwa hekima ya kuumbwa kwa wanadamu katika jinsia, mataifa na makabila tofauti tofauti ni kujuana na kutambulikana ili wakamilishana na kubadilishana mawazo, uzoefu na manufaa na kwamba msingi wa kupendeleana baina ya watu ni uchamungu tu. Mwenyezi Mungu (S.W.) Alisema: {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana namwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliyemchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari} [49/13].

Kwa hiyo, tunaona kuwa sheria ya kiislamu imetangaza kuwa watu wote wako sawa ambapo wametoka chanzo kimoja wakaumbwa na Mungu Mmoja watarejea kwake ili wafanyiwa hesabu kwa mema na maovu. Pia, sheria inawakumbusha waislamu kuwa wanatakiwa kuwa na uhusiano mzuri na watu wote na wasiwadharau wengine, bali washirikiane na watu wote kwa ajili ya kuhakikisha matarajio yao na kupata radhi ya Mola wao Mtukufu.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.