Kukana Mungu na Hatari yake juu ya Mtu na Jamii Nzima

Imeandaliwa na Dkt.; Alaa Salah Abdelwahed

  • | Monday, 25 December, 2023
Kukana Mungu na Hatari yake juu ya Mtu na Jamii Nzima

     Ukanaji Mungu au kutoamini kuwepo kwa Mungu ni fikra ya kifalsafa inayomaanisha kukana kuwepo kwa Mola Muumbaji (S.W.), fikra hiyo inaifuata yeyote asiyeamini Mwenyezi Mungu (S.W.) na kudai kuwa ulimwengu umejitokeza binafsi bila ya kuumbwa, bali kutokana na nishati zilizotukia sadfa, paispo kuainisha wakati maalumu wa kutokea na kujitokeza ulimwengu huu. Pia, wafuasi wa fikra hiyo hudhani kwamba aliyoyafikia mwanadamu katika maisha yake yote ni matokeo ya maendeleo ya maisha siyo kwa kuwa yameletwa na kuumbwa na Mungu, kwa hivyo, wafuasi wa fikra na madhehebu hiyo ndio watu waliojivunia akili yao, wakadhani kwamba akili zao hizo zinaweza kutambua yote yaliyomo katika ulimwengu, na kuwa yale mambo yasiyoonekana au kutambua kwa viungo vya mwili, basi hayapo kabisa, wakisahau kwamba Mwenyezi Mungu Amewaumba na kuwapa akili hizo na viungo hivyo, na kuainisha kazi ya kila viungo kutambua baadhi ya mambo na kushindwa kutambua mambo mengine, kwani Mwenyezi Mungu (S.W.) Amewataka wanadamu kumwamini pasipo na kumwona au kumtambua kwa viungo vya kimwili.

Mwenyezi Mungu (S.W.) Ameashiria fikra hiyo ya ukanaji Mungu Aliposema: "Hakika wale wanaoupotoa ukweli uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii Sisi. Je! Atakayetupwa Motoni ni bora au atakaye kuja kwa amani Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona mnayoyatenda" [Fussilat: 40]. Kwa hiyo, inaonekana kuwa Mwenyezi Mungu katika aya hii Amethibitisha kuwa fikra hiyo ya kukana kuwepo Mungu ipo, na kueleza kuwa wanaofuata fikra hiyo wanakana ishara Alizozitoa Mwenyezi Mungu ambazo ni alama za kiulimwengu na ishara (muijiza) za kisheria, ambapo alama za kiulimwengu ni zile alama au ishara zinazohusiana na uumbaji, upangaji na uendeshaji wa ulimwengu, ama ishara za ksheria ni zile zinazofungamana na Wahyi na Mitume (Muijiza), na kwamba anayekana alama za kiulimwengu hukadhibisha na kukana muijiza za kisheria kikawaida.

Kwa kweli ukanaji Mungu ni hatari kubwa inayotishia wanadamu na jamii kwa jumla, kwa hiyo inapaswa kujikinga nao na kuwatahadharisha wengine kutokana nao, ambapo wafuasi wa fikra hiyo wanadai kuwa alama za kiulimwengu zilipatikana kwa sadfa wala haziumbwi na Mwenyezi Mungu, mfano wa wale wanaodai kuwa usiku, mchana, jua na mwezi zilijitokeza kwa mazingira na kwamba zote zimejitokeza sadfa. Vile vile, wanakana ishara na muijiza za kisheria kama vile; Malaika, Pepo, Moto, Ufufuo baada ya kufa na kadhailka, hivyo wanakana yote yanayotokana na Whayi, Mitume na miujiza zao na hukumu walizozitoa maana kuwafahamisha watu yapi ni halai na yapi ni haramu.

Kutokana na maana hiyo, kutoamini Mungu ni fikra batili isiyokubalika kiakili, na inatakiwa kuelewa kwamba kuna tofauti kubwa baina ya fikra hii katika zama za kale na katika zama za kisasa, ambapo kutoamini Mungu kwa maana ya kutokiri kuwepo kwa Mwenyezi Mungu ni fikra ambayo haikuwa imeenea hapo zmani, bali ushirikina kwa madai mbalimbali ulioenea wakati ambapo kukiri kuwepo kwa Mungu kulipatikana, lakini shida lilikuwa ni kukiri kuwepo zaidi ya Mungu Mmoja, hali hiyo imeelezwa katika Qurani Takatifu, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: "Sema: Ni ya nani ardhi na viliomo ndani yake, kamanyinyi mnajua? * Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je,hamkumbuki?* Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na MolaMlezi wa A'rshi Kuu?*Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, hamwogopi?* Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kilakitu, naye ndiye anaye linda, wala hakilindwi asichotaka, kama mnajua?*Watasema: (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu. Sema:Basi vipi mnadanganyika?" [Al-Muminuun: 84-89].

Ama ukanaji wa kuwepo Mungu katika maana yake ya kisasa kunamaanisha kutoamini kabisa kuwepo Mungu, ambapo wafuasi wa fikra hiyo wamedai kuwa wamehakikisha usahihi wa fikra yao kupitia elimu ya kisasa na uchunguzi wa kiundani, wakadai kwamba dini haisaidii kufikia matokeo haya, jambo ambalo ni uwongo dhahiri kwani dini na elimu hazipingani hata kidogo kwa upande mmoja na baina yao na kumwamini Mwenyezi Mungu kwa upande wa pili, kwa kuwa elimu huwaita wanadamu kukiri kuwepo Mwenyezi Mungu na kuthibitisha kwamba ulimwengu kama huu hauwezekani kujitokeza sadfa, bali umeumbwa na kuundwa na Mola Muumbaji; Mwenyezi Mungu (S.W.).

Kuhusu kutoa kinga na suluhisho la kupambana na fikra potofu hiyo, basi tungetaka kupambana na fikra hiyo tunatakiwa kuangalia sababu zake na kuvichambua vitenda kazi vya kujitokeza kwa fikra hiyo, miongoni mwa sababu hizo kutojali malezi mema ya watoto yanayotokana na mafundisho ya kiislamu, ambapo familia isiyozingatia malezi ni rahisi kushawishiwa kwa fikra kama hizi, kwa hivyo Abu Daudi amesimulia kuwa Mtume (S.A.W.) amesema: "Mwaagizeni watoto wenu kusali wakifika miaka saba, na mwapigeni wakiipoteza sala wakiwa na miaka kumi". Naye Ibn Al-Qayyim Mungu Amrehemu amesema: "Yeyote anayefanya uzembe kuwalea watoto wake akawaacha walelewa ovyo, huwa amekosa kosa kubwa, ambapo wengi wa watoto waliopoteza njia sahihi ndio sababu ya msingi ya kupotezwa kwao ni wazazi wao maana hawakujali kuwalea ipasavyo, na kutowafundisha nguzo za dini na sunna zake, wakawapoteza wakiwa wadogo, basi wakawa hawana faida kwa nafsi zao wala kwa wazazi wao hao".

Aidha, miongoni mwa sababu za kuwa na fikra za kutoamini Mungu, kuchanganya na marafiki wabaya ambao wanamshawishi mtu aende knyume cha maumbile mema na mafundisho mazuri ya dini na elimu, kwa kawaida mwanadamu huathirika marafiki na watu ambao anaambatana nao, na hata roho zinaungana na kuathiriana, kwa hiyo Maimamu Bukhary na Muslim wamesimulia kuwa Mtume (S.A.W.) amesema: "Mfano wa rafiki mzuri na rafiki mbaya ni kama muuzaji wa uturi (Audi) na mhunzi anaetengeneza chuma, maana muuzaji wa uturi ukiambatana naye ama atakutunika uturi au utanusa harufu mzuri, ilhali mhunzi ukiambatana naye ama nguo zako zitachomoka au utanuka harufu mbaya kutokana na kazi yake".

Kwa hivyo, rafiki mbaya mwenye fikra potovu humwathiria vibaya rafiki yake, na kumshawishi ajiunge na fikra hizo na kujiweka mbali na dini ili afanane naye katika maovu na upotufu wake. Khalifa wa waumini Othman Bin Affaan (R.A.) amesema: "Mzinifu mwanamke angependa wanawake wote wangefanana naye kufanya uovu huu huu". Naye Mwenyezi Mungu (S.W.) amesema: "Makafiri Wanapenda lau kuwa nanyi mngekufuru kama walivyokufuru wao, ili muwe sawa sawa" [An-Nisaa: 89].

Mwishoni; tunaeleza kuwa kutoamini Mungu na ukanaji wa kuwepo kwa Mungu ni fikra hatari sana inayoathiria vibaya dini zote, kwa kuwa fikra hiyo haipingana na Uislamu tu, bali inapingana na dini zote za mbinguni na hata falsafa za kutungwa, hivyo ni kwa sababu ya kwamba wafuasi wa fikra hiyo hawakiri dini yoyote wala hawakiri Mungu kabisa, kwa hivyo, kuenea kwa fikra hiyo ni kama vita mpya dhidi ya dini inayoendeshwa na watu wasioamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu wala hawafuati dini yoyote, bali wanalenga kuharibu imani na itikadi za watu na jamii. Kwa hiyo, inabidi kupambana na vita hiyo ya kifikra na kuzuia hatari inayotokana na fikra na maoni haya, wanajamii wote wanatakiwa kushirikiana kuwakinga vijana kutokana na fikra hizo na kuwaelekeza kwenye fikra zilizo sawa.

Taasisi za kiilemu, familia, viongozi wa dini, vyombo vya habari na mashirika ya kijamii wote wanatakiwa kushirikiana kupambana na fikra hiyo. Pia, tutambue uwanja hatari wa kueneza fikra hiyo ambao ni mitandao ya mawasiliano ya kijamii, ambapo mitandao hiyo inatumika sana kueneza fikra potovu hizi, kwa hiyo inabidi kudhibiti mitandao hiyo na kuzidisha na kuimarisha harakati za kuwaelekeza, kuwaongoza na kuwafahamisha vijana kwenye ukweli wa dini yao kupitia programu za kidini, kitamaduni na kifikra kwa lengo la kuwaokoa vizazi vijazo kutokana na mabaya hayo.

Kwa upande wake, Al-Azhar Al-Shareif imechukua hatua kadhaa kukabiliana na hatari ya kuenea kwa Ukanaji Mungu, ambapo ilitoa taarifa nyingi kutahadharisha hatari hiyo na kuwaelekeza vijana kushikilia imani yao wakitegemea akili zilizoongoka, na maumbile ya kibinadamu, miongoni mwa hatua hizo; kuanzisha kitengo maalumu kujibu tuhuma za kukana Mungu, kutoa ripoti, makala na tafiti kuhusu suala hilo, pamoja na kusimamia mijadala na mikutano inayohusiana na suala hili kwa lengo la kubainisha ukweli wa fikra hiyo potofu na kufafanua hatari za kuenea kwake katika jamii mbalimbali duniani.               

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.