Taarifa ya Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra potofu kuhusu maelezo ya mwandishi wa habari mzayuni anayechocheza kuwaangamiza wapalestina

  • | Wednesday, 27 December, 2023
Taarifa ya Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra potofu kuhusu maelezo ya mwandishi wa habari mzayuni anayechocheza kuwaangamiza wapalestina

     Mwandishi wa habari wa Kizayuni mwenye fikra potofu: anatoa wito hadharani kuangamizwa kwa watu wa Palestina kwenye skrini za televisheni ya uvamizi.. Na #Kituo cha Al-Azhar: Taarifa hizi za Nazi za kifashisti zinaonyesha kushindwa wazi kwa vita vyao vya umwagaji damu vya kudumu kwa muda mrefu pamoja na kuendelea hasara zao za kijeshi na kiuchumi.

 

Wakati wa mahojiano ya televisheni, "Tsvi Yehezkeli", mleta habari wa masuala ya Kiarabu na mkuu wa sehemu ya Kiarabu kwenye Kituo cha 13 cha televisheni ya Kiebrania, alisema kwamba vikosi vya uvamizi vilipaswa kupeleka pigo la kufungua kwenye Ukanda wa Gaza ili kuua Wapalestina laki moja kwa wakati mmoja, bila ya kutofautisha baina ya raia na wanajeshi, kisha baada ya hayo kuchukua maamuzi ya kusimamisha kufyatua risasi na kubadilishana mateka, sawa na shambulio la kushtukiza la Operesheni ya "Risasi inayomiminika" dhidi ya Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza mwaka 2008, ambalo lilisababisha kuuawa shahidi kwa Wapalestina 1,417, wakiwemo raia 926, watoto 412 na wanawake 111

 

Jambo linalostahiki kutajwa kwamba vita vya mauaji ya kimbari vinavyojulikana kwa jina la Operesheni ya "panga za kichuma, ambayo jina lake lilichaguliwa na uvamizi huo kama ni anuani inayoashiria uadui na ukatili wake wa kigaidi dhidi ya Wapalestina, vinataka kubadilisha jina lake -kwa sababu ya kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa- kwa jina la Vita vya “Mwanzo; kitabu cha kwanza cha Agano la Kale” au vita vya “Simhat Taorah” ili kubeba mwelekeo wa kidini na Kiitikadi, ambapo tangu Oktoba 7, mauaji (1,700) yamefanywa, yakisabibisha shahidi (20,258), wakiwemo (8,000) Watoto, (6,200) wanawake, (310) wahudumu wa matibabu, (35) walena rai ana (101) kutoka kwa waandishi wa habari.

 

Kwa upande wake, Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu kinathibitisha kwamba taarifa hizi za nazi na fashisti siyo tu ila kitu kimoja miongoni mwa vitu vingi na zinaonyesha kushindwa wazi kwa vita vyao vya umwagaji damu, vya muda mrefu, pamoja na kuendelea kwa hasara kati ya safu za askari wao wa kigaidi, pamoja na upotevu wa zana za kijeshi na migogoro ya kiuchumi iliyoikumba mamlaka ya ukoloni, na kwa uhalisia taarifa hizi ni sawa na kauli ya waziri wa Kizayuni "Amihai Eliaho" aliyetoa wito wa kutupa bomu la nyuklia dhidi ya Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza, na mjumbe wa Knesset "Tali Gottlief", ambaye alitoa wito wa matumizi ya silaha za nyuklia kuwaangamiza kabisa watu wa Palestina, na taarifa zingine zenye fikra potofu za kibaguzi ambazo hujaza majukwaa ya mitandao ya kijamii na majukwaa ya vyombo vya habari, ambazo zinaakisi mtazamo wa Kiburi ya kikabila na ubaguzi wa rangi wa chuki kwa kila kitu cha Kiarabu na kukiangamia bila ya kuwepo hisia ya dhamiri ya mwanadamu.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.