Matoleo ya Kitengo cha lugha za kiafrika kwenye Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu kwa mwaka 2023

  • | Saturday, 30 December, 2023
Matoleo ya Kitengo cha lugha za kiafrika kwenye Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu kwa mwaka 2023

 

     Kisha tunapenda kukuarifuni kwamba Kituo hicho kilianzishwa mwaka 2015 kwa lengo la kufuatilia waliyoyatoa wafuasi wa makundi ya kigaidi na kuyachambua madai wanayoyatoa wakijaribu kuwashawishi vijana wajiunge nao, pia tunafuatilia kwa makini matoleo ya makundi ya kigaidi hasa Kundi la Al-Shabab, Boko Haram, ISIS na makundi mengineyo kwa ajili ya kutambua na kuainisha fikra potofu na kuandaa majibu ya kuyabatilisha madai haya tukitarajia kuchangia kuwakinga waafrika na walimwengu wote kutokana na fikra hizo mbaya na kuwaelekeza vijana wetu kwenye njia ya kueneza amani badala ya vurugu na utulivu badala ya fujo na ukatili.

Mwaka huu wa 2023, kwa mwaka wake wa nane, kitengo cha lugha za kiafrika kwenye Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu kimeendelea na kazi zake za kufichua fikra potofu na kufuatilia taharuki za makundi ya kigaidi, pamoja na kuchambua sababu za kuenea kwa ugaidi barani Afrika hasa baada ya kuangamizwa kwa wengi wa wafuasi na viongozi wa makundi ya kigaidi kama vile; Daesh na Boko Haram.

Miongoni mwa masuala yaliyoshughulikiwa na watafiti wa kitengo hicho na kituo kwa ujumla ni suala la uadui wa kizayuni dhidi ya ukanda wa Gaza na uvamizi wa kikatili unaoendelea kuwaangamiza watoto, wazee, wanawake na raia wasio na hatia, ambapo makala, ripoti na kampeni za kufahamisha zilitolewa kufichua ukweli wa uadui huo wa kikatili na historia ya ushujaa wa wapalestina kupambana na uadui huo.  

Watafiti wa kitengo hicho walichangia kutoa matoleo mbalimbali kuhudumia lengo kuu lao ambalo ni; kuwakinga vijana waafrika kutokana na fikra potofu na kuelekeza nchi na watawala kwenye mipango ya makundi ya kigaidi na mikakati yao.

Kupitia makala, ripoti, kampeni, jumbe za kufahamisha, kanda za video, mijadala na shughuli mbalimbali kitengo cha lugha za kiafrika kimefanya juhudi kubwa kutekeleza wajibu wao wa kufikisha ujumbe wa Al-Azhar Al-Shareif kwa lugha mbalimbali kuhusiana na masuala nyeti ya siku hizi.

Mnaweza kusoma na kuangalia matoleo yetu kupitia mitandao yetu kwenye mtandao wa Facebook, X, Instagram, pamoja na tovuti ya Al-Azhar Al-Shareif, mbali na kutoa baadhi ya makala kwenye magazeti ya kiswahili nchini Tanzania na mihadhara ya ana kwa ana kwa vijana wa vyuo vikuu vya kimisri.

Kwa kweli, Kituo kinaendelea kueneza ujumbe wa Al-Azhar kuwapa vijana mafunzo mema katika maisha yao na kuhojiana na vijana walioathiriwa na fikra potofu kwa lengo la kuchangia katika kueneza amani na fikra za ukati na kati.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.