Hatari ya Maneno ya Uchochezi na Nafasi yake kuharibu Amani ya Kijamii

Imeandaliwa na Dkt., Alaa Salah Abdelwahed

  • | Thursday, 4 January, 2024
Hatari ya Maneno ya Uchochezi na Nafasi yake kuharibu Amani ya Kijamii

 

     Kwa hakika mwanadamu atahesabiwa kwa kila alilolitamka na kila alililolifanya wakati wa maisha yake, likiwa jema atalipiwa jema ama likiwa baya atajuta wakati ambapo majuto hayatakuwa na maana. Wengi wanadhani kuwa maneno tunayoyasema usiku na mchana hatutaulizwa kuhusu kwake wakidhani kwamba ni maneno tu hayana athari yoyote, kwa hiyo, hayastahili kuwa sababu ya mtu aadhibiwa au alipiwa mema.

Kwa hao tunasema kwamba dini yetu ya kiislamu imetwelezea kwamba neno moja linaweza kumwokoa mtu kutoka kwa adhabu ilhali neno jingine linaweza kumwangamiza umma. Kwa hakika, neno lina umuhimu mkubwa mno kwa mtazamo wa sheria ya kiislamu, kwa hiyo mwislamu anatakiwa kuyadhibiti maneno yake kwa kuwa anatambua kuwa: {Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari} Qaaf: 18.

Hivyo, imani ya mwislamu inamwelekeza na kumwonya kuwa kila analolitamka huandikwa katika daftari ya vitendo vyake na atahesabiwa maneno yake haya katika Siku ya Mwisho mbele ya Mwenyezi Mungu. Pia, kusema yaliyo mema ni sababu ya mtu kujiokoa kutoka kwa adhabu na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (S.W.) kwa kuwa maneno mema husaidia upendo, amani na utulivu ziimarike katika jamii, hali ambayo inaipeleka jamii kuwa na mshikamano, kwa hiyo Mwenyezi Mungu Ameunganisha kufuzu kwa kuwa na hali hiyo: {Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semenimaneno ya sawasawa * Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu naakusameheni madhambi yenu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwamafanikio makubwa} Al-Ahzaab: 70-71.

Vile vile, tunaambiwa kwamba maneno yako katika aina mbalimbali ambapo kuna maneno yanayomsaidia msemaji wake apate heri na mema pengine kuna maneno mengine yanayompeleka msemaji wake mashakani. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu (S.W.) Ametupa mifano miwili ya maneno mazuri na mabaya na hatima ya kila njia kwa kusema: {Hebu hukuona vipi Mwenyezi Mungu alivyo piga mfano wa neno zuri? Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni * Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka * Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, uliong'olewa juu ya ardhi. Hauna imara * Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo} Ibrahiim: 24-27.

Pia, madhambi makubwa mengi yanatokana na maneno, kwa mfano uwongo, ushawishi, ulaghai na fitina haya maovu yanategemea maneno mabaya yasiyoendana na mafunzo ya dini wala tabia njema zinazotakiwa kuwa nazo na kila mwislamu. Wataalamu waliyagawa madhambi katika madhambi ya kivitendo na madhambi ya kimaneno, na hata yale madhambi ya kivitendo asilimia kubwa yake hutokana na maneo mabapo kwa neno baya inawezekana kuzuka mapigano, mauaji, matusi na matatizo mengine mengi ilhali kwa neno zuri tunaweza kujiokoa kutoka madhara na maovu haya yote na tujikinga na matatizo ya dunia na Akhera.

Mtume (S.A.W.) alipoulizwa kuhusu maneno na athari zake kuainisha hatima ya mtu kama ataingizwa peponi au motoni alishanga sana kutoka kwa muulizaji ambaye ni swahaba Mua’adh bin Jabal (R.A.) alipouliza kwa kusema: “Ewe Mtume! Je sisi tutahesabiwa na kuulizwa kuhusu maneno tunayoyatamka?! Mtume (S.A.W.) akamshtusha na kusema: Ewe Mua’adh ni swali baya mno, kwa hakika sababu ya kwanza na ya kimsingi ya kuwaangamiza watu motoni ni matokeo ya ndimi zao”.

 

 

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.