Uislamu Wakataa Vurugu na Ugaidi wa aina yoyote

Imeandaliwa na Dkt.; Alaa Salah Abdulwahed

  • | Thursday, 11 January, 2024
Uislamu Wakataa Vurugu na Ugaidi wa aina yoyote

     Mtume (S.A.W.) ameashiri kuwa Uislamu itaenea na kufika pembe zote za dunia, na kuingia nyumba zote Mashariki na Magharibi mwa ulimwengu, maneno ya bishara hii ya ushindi na kuimarika na kuenea kwa dini ameyasema Mtume (S.A.W.) wakati maadui wa Uislamu walipokusanya na kuungana kwa lengo la kupigania vita dini hiyo wakidhani kwamba wanaweza kuishinda katika siku ya Al-Ahzaab, maneno haya ya Mtume yalikuwa yanatosha kutuliza nyoyo za maswahaba na kuwatia moyo waumini. Pia, Mtume (S.A.W.) alibashiri kutawala nchi za Ajemi na Rumi na kuangamizwa mamlaka ya Qesraa (Mfalme wa Waajemi) na kugawanya utajiri wake kwa waislamu, haya yote yalitukia kiuhalisia katika siku za baadae katika historia ya kiislamu.

Historia ya kiislamu ilithibitisha kufika kwa waislamu nchi za Asia ya Kati kwa mara ya kwanza kwa mfano; India na nchi nyingine. Haya yote hayakuwa kwa nguvu wala ulazimisho, bali kwa sababu ya tabia njema za waislamu na uzingatio wao kwa Da'awa. Vile vile, historia ya kiislamu kwamba baadhi ya makabila ya Watatari waligeuka waislamu. Kwa kweli wengi wa waliojiunga na Uislami walifanya hivyo kwa sababu ya tabia njema za waislamu na sifa bora na mafundisho mazuri ya dini hii kuliko dini zote. Uislamu haikuenea kwa nguvu wala ulazima wala kupitia ugaidi, bali imeenea kwa sababu imependezwa na nyoyo na nafsi za watu wote wakiwemo wakazi wa maeneo haya.

Inajulikana kwamba anayelazimishwa kufanya kitu huwa hakipendi kitu hicho, na ikawa rahisi akiacha kitu hicho, hivyo divyo watu wanaolazimishwa kuingia katika dini au kugeuka kutoka dini fulani hadi nyingine kwa nguvu, ni rahisi waritadi kwani hawakuwa na imani kwa dini mpya hiyo. Jambo hilo halikutukia kabisa katika historia ndefu ya kiislamu. Ama madai wanayoyatoa maadui wa Uislamu makundi, vyama na hata mataifa maalum, tangu zamani mpaka sasa kwamba Uislamu una uhusiano na ugaidi, basi ni madai yasiyo na maana wala hayakubaliki hata kidogo. Kwani dini hiyo adhimu imeenea kwa usamehevu, rehma na upole na watu wote wakiwa marafiki au maadui.

Ugaidi wa makundi yaliyoenea hapa na huko katika enzi yetu ya kisasa hauna uhusiano wowote na dini yoyote hasa Uislamu ambao ni dini ya amani na usalama, kwa hiyo vitendo vyote vya kinyama na kikatili vinavyofanywa kwa madai ya kutetea Uislamu viko mbali sana na dini hii adhimu. Uislamu ni dini inayokataa kuwatishia watu au kuwafanyia uadui na ukatili wowote. Waislamu wanatakiwa kujiweka mbali na vitendo na wito hizo za kuchocheza moto wa ugaidi na chuki, bali kubainisha kuwa ukweli wa dini hii unathibitisha kuwa dini iko kinyume kabisa na vitendo hivyo. Kwani haikualiki kwa dini iliyoweka misingi ya kuishi pamoja na wengine kwa amani na kutendeana na watu wote kwa msingi wa amani na kuheshimiana iwe msingi wa uadui au vitendo vyovyote vya kiadui.

Pia, waislamu wanatakiwa kueleza kuwa Uislamu imeainisha vidhibiti hata wakati wa kupambana na madui vitani, amabpo dini hii kwa mujibu wa rehma yake imewakataza wapiginaje wake kuua wazee, watoto, wanawake, watawa na wanaojibana kwa ibada, waislamu wamekatazwa pia kukata miti, kuharibu majumba, kufanya ufisadi katika ardhi, kuvunja njia, kuwatishia watu ambao si wapiganaji wala wasiwafanyia khiyana au ukatili wa kinyama na kutangaza haya kwa ajili ya kuwahofisha wengine. Kwa jumla, Uislamu imeweka adabu na vidhibiti hata wakati wa vita, zile adabu na vile vidhibiti zinategemea msingi wa rehma, huruma na heshma kwa ubinadamu.

Kwa kweli, vyombo vya habari vinavyochocheza kutangaza picha za mauaji ya kinyama kwa namna inayochafua Uislamu na waislamu vinachocheza sana fitina na chuki baina ya watu. Wakati huo huo inapaswa kuwaita waislamu waliopotea na kukosa njia iliyo sahihi kwa kushawashika vibaya, na kuwaelekeza kwenye njia iliyo sawa, kwani mwislamu ana jukumu la kuwaongoza watu kwenye heri na kuwasaidia waepukane na shari na maovu kwa kutegemea misingi ya dini hiyo takatifu. Misingi ambayo ni pamoja na rehma, amani, usalama, usamehevu, tabia njema, upendo, kufahamiana, wastani, ukati na kati, kukataa vurugu na ukatili na kupambana na ugaidi na fikra kali.

Inafahamika pia kuwa Uislamu ni dini ambayo sheria yake imekusanya hukumu zahusianazo namna ya kupambana na ugaidi na uadui na kuwapatia adhabu wanaotuhumiwa kuhusika makosa haya. Kwa kuwa dini hii imeasisiwa misingi na malengo ya kuhakikisha amani, usalama, utulivu na ustawi kwa wanadamu wote, wafuasi wake walipaswa kuelewa kuwa ujumbe wa Uislamu ni ujumbe wa amani siyo ukatili na uadui, ni ujumbe wa kuwalinda wanadamu wote kutokana na maovu na shari ya aina yoyote, na kuwaokoa kutoka hatari yoyote kwa nafsi zao, mali zao au heshma zao, jambo lililo wazi kaisa katika Qurani Takatifu na Sunna za Mtume (S.A.W.).

La kuthibitisha hayo kuwa Mwenyezi Mungu Ameharamisha damu ya mwanadamu isimwagike pasipo na haki, Akafanya adhabu ya kumuua mtu bila ya kuwepo saababu ya kisheria na kutokana na vidhibiti maalum vya sheria ni adhabu iliyo kali zaidi na kuwa dhmbi hilo ni dhambi kubwa zaidi kuliko madhambi yote. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa} [An-Nisaa: 93], Amesma pia: {Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini – na atakaye fanya hayo atapata madhara * Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka} [Al-Furqaan: 68-69]. Bali Mwenyezi Mungu Amefanya malipo na adhabu ya anayemuua mmoja ni kama aliyewaua watu wote, Aliposeam: {kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote} [Al-Maidah: 32].

Uislamu ilishadidisha sana uharamu na ukatazo wa kumuua mtu asiye mwislamu anaye ahadi na waislamu, ambapo Mtume (S.A.W.) alisema: "Yeyote atakaemuua mwenye ahadi hatapata harufu ya Pepo hata kidogo" Na katika hadithi nyingine alisema: "Hakika Mwislamu huwa na fursa ya kutubu madamu hajafanya uhalifu wa kumuua mwingine bila ya haki".

Mwenyezi Mungu Amelaani kikali kufanya ufisadi katika nchi na uvamuzi dhidi ya wasio na hatia, Akazingatia jambo hilo ni kati ya sifa mbaya zaidi na makosa mabaya zaidi kuliko maovu mengine. Mwenyezi Mungu Amesema: {Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki} [Al-Araaf: 33]. Bali Uislamu imepitisha adhabu iliyo kali zaidi kabisa kwa wale wanaofanya ufisadi katika nchi kwa kufanya jinai za mauaji na uharibifu, Mwenyezi Mungu Amesema: {Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawa nia kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa} [Al-Maidah: 33]. Hivyo tunaelewa vipi Uislamu imepiga vita ugaidi na vurugu kwa aina mbalimbali na kubainisha kukataa kwa sheria ya kiislamu uadui wa aina yoyote.

Kwa hali hii Uislamu ilitangulia kanuni na sheria zote za kupambana na ugaidi na kulinda jamii kutokana na athari zake mbaya, ikilenga kumlinda mwanadamu wa dini, kabila, rangi, mwelekeo wowote; nafsi yake, mali na heshima zake, dini na akili yake. Na kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi huo kwa mwanadamu sheria ya kiislamu imeleza masharti na vidhibiti maalum na kuweka adabu za kuhifadhi amani na utulivu na rehma baina ya watu wote. Kwa hiyo Uislamu imekataza uadui au uvamuzi wa aina yoyote kwa kisingizio chochote baina ya waislamu wenyewe kwa wenyewe wala baina ya waislamu na wengine wasio waislamu, na kuhatamisha dhulma, ikiwaita wote wawe na rehma, upole ma upendo.

Rehma ndiyo msingi muhimu wa miamala ya watu wenyewe kwa wenyewe, kwa mujiu wa aliyosimulia Ibnu Masoud (R.A.) Mtume (S.A.W.) alisema: "Hamtakuwa na imani iliyo kamili mpaka muweni na rehma nyinyi kwa nyinyi" Maswahaba wakasema: "Ewe Mtume! Sote hivyo ndivyo" Akasema Mtume: "Siyo rehma ya rafiki kwa rafikiye, bali kuwa na rehma kwa watu wote na hata viumbe vyote". Kwa hiyo ifahamike kuwa siyo makusudiyo ya kuwa na rehma ni kuhusisha rehma kwa watu tunaowajua tu, bali kwa wote, mpaka rehma hii ifike viumbe vingine kama vile; wanyama na vinginevyo. Mtume (S.A.W.) alipotaka kueleza kuwa rehma inabidi iwe kwa jumla na kwa viume vyote alisema: "Yeyote asiye na rehma hatatendewa rehma". Na Mwenyezi Mungu (S.W.) Aliyesifika kwa Rehma iliyo juu kabisa, rehma isiyofanana na rehma ya wanadamu, amapo Rehma ya Mwenyezi Mungu ni ya hali ya juu zaidi, Yeye Ndiye Mbora wa wanao rehemu, Anaye Rehma iliyojumuisha kila kitu.          

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.