Ingawa kupunguza kwa idadi ya mashambulio.. Bara la Afrika na ugaidi katika mwaka wa 2023 vitisho vinaendelea kwa mikakati tofauti

 • | Thursday, 18 January, 2024
Ingawa kupunguza kwa idadi ya mashambulio.. Bara la Afrika na ugaidi katika mwaka wa 2023 vitisho vinaendelea kwa mikakati tofauti

     Mwaka wa 2023 umemalizika na vitisho vya makundi ya kigaidi katika bara la Afrika havijamalizika; ambapo bara la Afrika bado linateseka kutokana na kuendelea kwa ugaidi katika maeneo kadhaa ya ardhi yake, ambapo nchi zake haziko mbali na hatari za makundi ya kigaidi yanayozunguka aina zote za maisha ya kawaida kwa watu wanaotaraji maendeleo, usalama na utulivu, hayo licha ya juhudi zinazotolewa na serikali za nchi za bara hilo kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa, pamoja na waliotumiwa kwa ajili ya kukabiliana na ugaidi.

Kiashirio cha Ugaidi barani Afrika kwa mwaka 2023 kinachoandaliwa na Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu kilifichua kupunguza kwa mashambulizi ya kigaidi kwa mwaka huu katika nchi kadhaa, baada ya wimbi la mapigo ya serekali za kiafrika dhidi ya makundi ya kigaidi, lakini wakati huo huo idadi ya mashambulizi haya yaliongezeka katika baadhi ya nchi zinazoshuhudia migogoro ya ndani na matatizo ya kiuchumi, ambapo makundi ya kigaidi barani Afrika yalidai kuhusika kwa operesheni za kigaidi (361), ambazo zilisababisha vifo vya watu (3,360), kuwajeruhi (913), na utekaji nyara wa (382) wengine, pamoja na kuwalazimisha maelfu ya watu kukimbia na kutoka makazi yao.

Na kupitia takwimu ya kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali kwa mashambulizi yaliyotekelezwa katika mwaka wa 2023, ilibainika kuwa eneo la Afrika Mashariki na Pembe la Afrika lilikuja katika nafasi ya kwanza kwa idadi ya mashambulizi ya kigaidi (140), na katika nafasi ya pili ni eneo la Sahel na Sahara kwa mashambulizi ya kigaidi (121), kisha katika nafasi ya tatu ni eneo la Afrika Magharibi ambapo idadi ya mashambulizi ya kigaidi ilifikia (60), huku katika nafasi ya nne ni eneo la Afrika ya Kati kwa mashambulizi (40).

Ama kwa upande wa idadi ya vifo vilivyosababishwa na mashambulizi ya kigaidi, eneo la Sahel lilikuja katika nafasi ya kwanza kwa vifo (1,393), likifuatiwa na eneo la Afrika Mashariki kwa vifo (1,038), kisha katika nafasi ya tatu eneo la Afrika ya Kati kwa vifo (471), huku eneo la Afrika Magharibi lilikuja katika nafasi ya nne kwa vifo (458).

Kwa upande wa mgawanyiko wa idadi ya wahanga wa ugaidi kwa mujibu wa nchi, basi Burkina Faso ilikuja katika nafasi ya kwanza katika nchi zilizoathiriwa zaidi na mashambulizi ya kigaidi; ambapo ilikabiliwa na mashambulizi ya kigaidi (67), yaliyosababisha vifo (955) kwa kiwango cha (28.4% ya jumla ya wahanga), jambo linaloonyesha umwagaji damu wa mashambulizi licha ya kupunguzwa kwake yakilinganishwa na Somalia; ambapo mashambulizi ya kigaidi nchini Burkina Faso yalipunguza kutoka (70) mwaka 2022 hadi (67) mwaka 2023, lakini viwango vya vifo viliongezeka kutoka (594) mwaka 2022 hadi (955) mwaka 2023.

Nchini Somalia, kuna kitu cha ajabu: ambapo ingawa ilikuja mbele ya eneo la mashambulizi kwa kukabiliwa na mashambulizi ya kigaidi (109) yaliyotofautiana kati ya mauaji, milipuko ya mabomu na mashambulizi ya kujitolea mhanga, lakini ilikuja katika nafasi ya pili kuhusu idadi ya vifo vya mashambulizi , na (929) wahasiriwa, kwa kiwango cha (27.6% ya jumla) idadi ya wahasiriwa wa ugaidi.

Mashambulizi ya kigaidi nchini Somalia yalipunguza kutoka (204) katika mwaka wa 2022 hadi (109) katika mwaka wa 2023, wakati vifo viliongezeka kidogo kutoka (916) mwaka wa 2022 hadi (929) mwaka wa 2023. Hapana shaka kwamba jeshi la Somalia lilipata mafanikio katika kuwafukuza kundi la Al-Shabab kutoka maeneo makuu ya kundi hilo, na utayarifu wa misheni ya mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) wa kujiondoa kwake mwaka 2024 ni dalili ya maendeleo yaliyofikiwa na serikali ya Somalia katika kupambana na ugaidi, lakini hayo hayakuzuia Somalia kuwepo miongoni mwa nchi za kwanza katika kielezo cha mashambulizi ya kigaidi katika bara la Afrika, kutokana na kuzidisha kundi la Al-Shabab kwa mashambulizi yake ya kigaidi, likitumia operesheni ya kujiondoa kwa (ATMIS) na kuvipa udhibiti kwa vikosi vya Muungano wa Kitaifa.

Na Nigeria inayokumbwa na janga la ugaidi wa Boko Haram na kundi la ISIS Afrika Magharibi, linakuja katika nafasi ya tatu; ambapo ilikabiliwa na mashambulizi ya kigaidi (58). Mashambulizi hayo yalisababisha vifo (447), kwa asilimia  (13.3% ya jumla ya wahanga wa ugaidi).

Inaangaliwa kwamba kupunguzwa kwa mashambulizi ya makundi ya "Boko Haram" na "ESWAB" nchini Nigeria yakilinganishwa na mwaka wa 2022, ambapo mashambulizi ya kigaidi yalipunguzwa kutoka (76) mwaka wa 2022, hadi (58) mwaka wa 2023, pia idadi ya wahanga ilipunguzwa kutoka (1043) hadi (447). Na kupungua huko kulisababisha kuwepo hali nzuri na kupunguzwa kwa mashambulizi ya makundi hayo mawili ya kigaidi nchini.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikuja katika nafasi ya nne kwa mashambulizi ya kigaidi (28), na idadi ya vifo ilifikia watu (403), kwa asilimia (11.9% ya jumla ya wahanga wa ugaidi). Na mashambulizi ya kigaidi yalipunguza kwa asilimia (53%) katika mwaka wa 2023, wakati viwango vya vifo vilipunguza kwa asilimia (39%).

Ama nchi ya Mali, ilikuja katika nafasi ya tano, ambapo ilikabiliwa na mashambulizi ya kigaidi (40) yakiwemo mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga, yote yalisababisha wahanga (282), kwa asilimia (8.4% ya jumla ya wahanga wa ugaidi).

Na nchi ya Niger ilikuja katika nafasi ya sita kwa mashambulizi (14), yiliyisababisha vifo (156) kwa asilimia (4.6% ya jumla ya wahanga wa ugaidi).

Na nchi ya Uganda ilikuja katika nafasi ya saba kwa kukabiliwa na mashambulizi (4) yaliyoanzishwa na  kundi la "Muungano wa vikosi vya Kidimokrasia", ambayo yalipelekea vifo vya watu (57), kwa asilimia (1.7% ya jumla ya wahanga wa ugaidi).

Inaangaliwa kwamba Uganda ilishuhudia ongezeko la mashambulizi ya kigaidi mwaka wa 2023 ikilinganishwa na mwaka wa 2022, ambapo ilikumbwa na shambulio moja lililosababisha kifo cha mtu mmoja. Na hiyo inamaanisha kuwa kulifukuza kundi la kigaidi la Al-Shabaab nje ya baadhi ya maeneo lililokuwa linadhibiti nchini Somalia kuliifanya kutekeleza mashambulizi mapya nchini jirani, ikiwemo Uganda.

Kenya ilikuja katika nafasi ya nane, ambapo kundi la Al-Shabaab lilitekeleza mashambulizi (23) ambayo yalisababisha vifo vya watu (40), kwa asilimia (1.1% ya jumla ya wahanga wa ugaidi).

Na nchi za Cameroon na Chad zilikuja katika nafasi ya tisa kwa asilimia sawa sawa, ambapo mashambulizi ya kigaidi haya yalisababisha vifo vya wahanga (34) kutoka nchi hizo mbili, ilhali Msumbiji ilikuja katika nafasi ya kumi kwa mashambulizi ya kigaidi (3), na kusababisha vifo vya watu (12).

Ama kuhusu juhudi za kupambana na makundi ya kigaidi barani Afrika katika mwaka wa 2023, basi takwimu inadhihirisha kuwa idadi ya magaidi waliouawa ilifikia (6,628) na wengine wafungwa (2,576) pamoja na kujisalimisha kwa magaidi (2,381).

Na kwa kuangalia viashirio vya ugaidi barani Afrika katika miaka miwili iliyopita, tunaona kwamba mashambulizi ya kigaidi mwaka 2022 yalifika (550) zilizolenga nchi (16), ambazo ni (Nigeria, Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burkina Faso, Mali, Niger, Chad, Cameroon, Kenya, Msumbiji, Afrika ya Kati, Senegal, Uganda, Ivory Coast, Benin, Togo), mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya wahanga (4,189), wakiwemo kunyongwa kwa (117), pamoja na majeruhi (2,029) , na kuwateka nyara (704). Na idadi ya vifo kutoka kwa makundi ya kigaidi ilifikia watu (5,407) na wafungwa (644) pamoja na kujisalimisha kwa (634).

Na katika mwaka wa 2021, mashambulizi yalifika (735) katika nchi (14), ambazo ni (Nigeria, Somalia, Jumhuri ya Democrasia ya Congo, Burkina Faso, Mali, Niger, Chad, Cameroon, Kenya, Msumbiji, Uganda, Ivory Coast, Benin, Togo), mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya watu (4,318), majeruhi (1,968), na mateka (1,210). Na idadi ya vifo kutoka kwa makundi ya kigaidi ilifikia (4,757) na wafungwa (820), pamoja na kujisalimisha kwa (833).

Na kwa mujibu wa kiashirio hicho kinachopima athari za ugaidi kulingana na idadi ya mashambulizi na wahanga, tunaweza kusema kuwa vifo vinavyotokana na ugaidi katika miaka mitatu vimepunguza kwa kiasi kikubwa; basi kiashirio hicho kilifichua kupunguza kwa jumla ya vifo kwa sababu ya ugaidi barani Afrika kwa watu (3,360) katika mwaka wa 2023, kwa kiwango cha kupunguza cha asilimia (19.9%) kulingana na mwaka wa 2022, ambapo wahanga (4,189) waliuawa, kwa asilimia (22.1%) katika mwaka wa 2021, ambapo wahanga (4318) waliuwawa.

Hapana shaka kuwa hali ya kiusalama barani Afrika bado si shwari, basi mpaka lini hali hiyo itaendelea kuwa mbaya licha ya juhudi za serikali na vikosi vya kimataifa zinazoendelea ili kuweka mipaka kwa mashambulizi ya ugaidi katika bara la Afrika! Je, umefika wakati ili bara hilo kumaliza ugaidi uliowatesa watu wake! Bara la Afrika linakabiliwa na hatari kubwa zinazolitishia katika ngazi mbalimbali, na baadhi ya vielezo vinabainisha kwamba labda kutokea ghasia zaidi na kuimarika kwa makundi ya kigaidi katika hali hiyo inayolikumba bara hilo. Na hiyo ni kutokana na baadhi ya mabadiliko ya ghafla yaliyokuwa na athari za moja kwa moja kwa shughuli za kupambana na ugaidi, yaliyo maarufu zaidi ni yafuatayo:

 • Kukosekana kwa utulivu wa kisiasa na kiuchumi katika nchi nyingi za bara, jambo lililoathiria vibaya maisha ya kijamii.
 • Kuendelea kwa migogoro na vita kadhaa, kama vile vita vya Urusi na Ukraini, mzozo wa ndani wa Sudan, mzozo wa silaha kaskazini mwa Mali, na uadui wa mamlaka ya kizayuni (Israel) dhidi ya Ukanda wa Gaza, na athari zake kwa usalama na uchumi wa kimataifa.
 • Mabadiliko ya tabia nchi na kutokea kwa idadi kadhaa ya majanga yaliyozuia harakati za kijeshi katika baadhi ya nchi, kwa mfano, mafuriko nchini Somalia yalisababisha kudorora kwa operesheni za kijeshi dhidi ya ngome za Al-Shabaab, huku kundi hilo likijitahidi kutumia mafuriko hayo ili kuimarisha uungaji wake kwa kufanya operesheni za uokoaji na kutoa misaada kwa maeneo yaliyoathirika.
 • Kuondoka haraka kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa na wa kitaifa wa kulinda amani kutoka maeneo ya kukabiliana na ugaidi imeongezeka, na kutenganisha kwa baadhi ya miungano ya usalama mwaka huu.
 • Kutekeleza kwa makundi ya kigaidi mashambulizi kwa njia tofauti kulingana na kampeni za kiusalama zilizotekelezwa dhidi ya ngome zao, jambo lililolisaidia kubaki na kuenea.

Kwa hivyo, ukweli wa hali wa nchi zilizoathiriwa - na ambazo zinaweza kuathiriwa –na ugaidi unawajibika kuchukua hatua na kufuata mikakati tofauti inayoziongoza kwa kukabiliana na makundi hayo ya kigaidi katika viwango vyote, na hayo kupitia yafuatayo:

 • Kurekibisha pande za upungufu katika nyanja za kiuchumi na kijamii kwa wenyeji, kukuta mahitaji yote ya maisha, na kukabiliana na umaskini na ukosefu wa ajira, ili vijana wasivutiwi na kupambana na kwani wanahitaji pesa; kwani haiwezekani kutenganisha baina ya hali mbaya ya kiuchumi kwa upande na kuenea na makundi ya kigaidi kwa upande mwingine.
 • Kuimarisha njia za ushirikiano wa kijeshi na uratibu kati ya nchi za mpaka zilizoathiriwa na kuzindua ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na makundi ya kigaidi.
 • Kukausha chemchem na vyanzo vya pesa vya makundi ya kigaidi kwa njia zote zinazowezekana ili kuzuia ununuzi wa silaha na kuwavutia wapiganaji.
 • Kutumia mbinu za kisasa na za kidijitali katika kupambana na shughuli za kigaidi, kwa lengo la kuhifadhi wabinadamu.

Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu

Kitengo cha Lugha za Kiafrika

Jan.2024

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.