Amani na Utulivu ni msingi muhimu wa kufikia maisha bora

Imeandaliwa na Dkt., Alaa Salah Abdulwahed

  • | Monday, 12 February, 2024
Amani na Utulivu ni msingi muhimu wa kufikia maisha bora

     Kwa hakika amani na usalama ndiyo neema muhimu zaidi kwa nchi yoyote duniani, ambapo wananchi wote hukutana na kuishi wakifurahia neema hiyo ambayo inapelekea utulivu kwa jamii mzima, mpaka watu wote hawakuwa na hofu wala wasi wasi kuhusu heshima yao, dini yao wala mali zao. Kwa kuwa neema hiyo ya amani ndiyo neema iliyokubwa na muhimu zaidi ikilinganishwa na mambo mengine, basi Mwenyezi Mungu (S.W.) Akawaneemesha watu wa Makkah na kubainisha umuhimu wa neema hiyo kwao katika aya nyingi katika Qurani Takatifu, kama vile: "Je! Kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui" Al-Qasas: 57, na katika aya nyingine Amesema: " Je! Hawaoni ya kwamba tumeifanya nchi takatifu ina amani, na hali watu wengine wananyakuliwa kote kwa majirani zao? Je! Wanaamini upotovu, na neema za Mwenyezi Mungu wanazikataa? " Al-Ankabout: 67, hali hiyo hiyo katika Sura ya Qureish kwa aya zake zote: " Kwa walivyo zoea Maqureshi* Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto*Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii* Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu".

Kwa Kweli kutaja jambo hilo (amani) lililotajwa wazi wazi katika Qurani Takatifu husisitiza umuhimu na nafasi ya neema hiyo, ambapo maana na hikima na malengo ya maisha hayatafikiwa pasipo na kuwepo kwa neema hiyo, ambapo neema yoyote anayo mwanadamu iko nyuma ya neema ya amani na usalama, kwa hiyo ustawi, utulivu, maendeleo hayafikiki amani ikikoseka, bali tunaweza kusema kuwa kwa kweli bila ya amani maisha haiwi bila ya amani, kwa hiyo Mtume (S.A.W.) alipotaka kuzungumzia neema alizopewa mwanadamu na Mwenyezi Mungu alianza kwa kutaja neema ya amani, kwani ndiyo neema ambayo neema nyinginezo zinaitegemea, Mtume (S.A.W.) alisema katika hadithi iliyosimuliwa na Salamah bin Obeid Allah bin Muhswan Al-Ansaariy, kutoka kwa baba yake kwamba alisema kuwa Mtume (S.A.W.) amesema: "Kwa hakika, yoyote anaeamka akiwa na amani maishani make, ana afya nzuri, anamiliki chakula na nahitaji ya siku yake, badi huwa ni sawa sawa na yule anaemlika dunia nzima" Imesimuliwa na Al-Hamiedy katika kitabu cake cha Musnad na Imamu Ahmed.

Kwa hiyo, inaonekana vipi Mtume (S. A. W.) amezingatia na kubainisha umuhimu wa neema hiyo ya amani kwa kuiweka kabla ya neema nyinginezo kwa kuwa ni neema. Zaidi ya hayo, Mtume Ibrahim (A.S.) alipotaka kumwomba Mwenyezi Mungu kwa mji mtakatifu wa Makkah na watu wake, aliaanza kwa kuomba amani kabla ya kuomba chochote kingine, Mwenyezi Mungu (S.W.) Alieleza hivyo katika Qurani Takatifu: "Na alipo sema Ibrahim: Ee Mola wangu Mlezi!Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wakematunda, wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Akasema: Na mwenye kukufuru pianitamstarehesha kidogo, kisha nitamsukumiza kwenyeadhabu ya Moto, napo ni pahala pabaya mno pa kurejea" Al-Baqarah 126. Aidha tunapata maana hiyo hiyo katika Sura za Ibrahim, An-Nahl na Sura ya Qureish kama tulivyobainisha juu.

Kwa hakika aya hizo zote zinathibitisha kuwa msingi wa neema zote ndiyo neema ya amani, ambapo ustawi wa uchumi wala utulivu wa kijamii hauwezi kupatikana ila ikipatikana amani na usalama nchini, pia inadhihirika kwa wote vipi Qurani Takatifu imepambana na wito na harakati za uharibifu na ufisadi ambazo hulenga kusambaratisha jamii na kuwaangamiza wananchi zikitegemea kupoteza amani na kuwahofisha wanadamu, hali hiyo ilitajwa katika Qurani Takatifu kuwa ni uhalifu mbaya na maovu makubwa ambayo ni ufisadi katika ardhi na kushadidisha Kupambana nayo kikali, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: "Na anapo tawala hufanya juhudi katika nchi kwakufisidi humo na kuteketeza mimea na viumbe. NaMwenyezi Mungu hapendi ufisadi* Na akiambiwa: Mwogope Mwenyezi Mungu, hupandwa namori wa kutenda madhambi. Basi huyo inamtoshaJahannam. Paovu mno hapo kwa mapumziko" Al-Baqarah 205-206.

Aya hizo kwa mujibu wa tafsiri ya Imamu Ibnu Jariir Al-Twabariy zinamaanisha: Ewe Mtume yule mnafiki akitoka kutoka kwako akiwa na ghadhabu hufanya maovu Aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu na kujaribu kumwasi Mwenyezi Mungu kwa maovu hayo ambayo ni kama vile kukata njia, kuharibu nchi, kuwadhuru watu, kama alivyofanya Al-Akhnas bin Shariq Al-Thakafiy aliyeelezwa na Al-Sadiy kuwa aya hii imeteremka kusimulia hali yake na adhabu anayoistahiki kwa vitendo vibaya vyake kuchoma mimea ya waislamu na kuwaua mifuga wao. Hayo ndiyo ufisadi katika ardhi, na maana hiyo hiyo tunaikuta katika Sura ya An-Naml ambapo Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: "Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya ufisadikatika nchi wala hawafanyi la maslaha* Wakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungututamshambulia usiku yeye na ahali zake; kishatutamwambia mrithi wake: Sisi hatukuona maangamizo yawatu wake, na sisi bila ya shaka tunasema kweli* Basi wakapanga mipango yao, na Sisi tukapangamipango yetu, na wao hawatambui" 48-50.

Na aya nyingine ya Sura ya Al-Baqarah inatusimulia kuhusu aina ya watu ambao hudai wema na kauli nzuri kwa ajili ya kutudhihirishia kwamba baadhi ya watu hutumia mema minajili ya kujificha nyuma yake na maovu yao na nia zao mbaya, hawa ndio waliotajwa na Mwenyezi Mungu kuwa ni wafisadi kwa sababu ya machafu na mabaya wanayoyafanya katika jamii na kusababisha kupoteza amani na utulivu wa jamii hiyo, kwa hiyo Mwenyezi Mungu Amewaamrisha waumini wakiongozwa na watawala wao Kupambana na wafisadi hao kikali kwa ajili ya kudhibiti jamii na kuhifadhi utulivu wake kwa sababu ya machafu yao, na wasipate fursa ya kueneza ufisadi wao katika jamii na nchi, Mwenyezi Mungu (S. W.) Ameeleza naman ya Kupambana na watu hao Akisema: "Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Munguna Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katikanchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewanchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katikaAkhera watapata adhabu kubwa* Isipo kuwa wale walio tubu kabla hamjawatianguvuni. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenyemaghfira na Mwenye kurehemu" Al-Maidah 33-34.

Hapana shaka kuwa Qurani Takatifu imeelezea vizuri adhabu kali ya uhalifu huu kwa lengo la kudhibiti jamii na kutoa tahadhrisho wazi kwa hatima ya kazi kama hiyo, jambo hilo hilo lilikaririwa kuhusu adhabu ya kumshutumu mwanamke kwa zinaa iliyobainishwa katika aya ya Sura ya Annuur: "Na wanao wasingizia wanawake mahashumu, kishawasilete mashahidi wane, basi watandikeni bakorathamanini, na msiwakubalie ushahidi wao tena. Na haondio wapotovu* Isipo kuwa wale walio tubu baada ya hayo nawakatengenea; kwani bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu"

Haya yote kwa ajili ya kuwazuia watu wasikose amani katika ardhi waishi kwa amani na utulivu bila ya kuogopa chochote juu ya heshima yao, damu zao na mali zao, wala damu zisifanyiwe ukatili au mali ziibiwe ovyo.

Mwishowe, hapana shaka kuwa uadui na dhuluma wanazozifanya wazayuni dhidi ya wapalestina ni jinai zisizoafikiana na maadili ya kibinadamu hata kidogo, ambapo wavamizi hawa hawana huruma kwa mtoto wala mwanamke wala mzee wala mgonjwa, bali wanabomoa kila kitu kwa madai ya kujitetea, ilhali wanatekeleza mkakati wa kuwaangamiza wananchi wa ukanda wa Gaza wasio na hatia, kwa hiyo tunatangaza upya kukataa na kushutumu uadui huo dhalimu na kutahadharisha kutoka katika kuenea chuki na maovu, licha ya kukosa amani na utulivu duniani kote.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.