Taarifa ya Al-Azhar kuhusu uadui wa kizayuni mjini Rafah

  • | Wednesday, 14 February, 2024
Taarifa ya Al-Azhar kuhusu uadui wa kizayuni mjini Rafah

 

     Al-Azhar yalaani uadui wa kigaidi wa kizayuni dhidi ya mji wa Rafah na inauonya ulimwengu kuhusu maafa makubwa ya kibinadamu yasiyowahi kutokea kamwe

Al-Azhar yauomba ulimwengu kuungana ili kukabiliana na mpango wa kizayuni unaolenga kuwaondoa Wapalestina nje ya Rafah.

Al-Azhar Al-Shareif inalaani vikali uadui wa kigaidi wa kizayuni uliolenga wapalestina wasio na hatia katika mji wa Rafah unaojaa kwa wakimbizi, na kuwaua zaidi ya watu 100, nusu yao ni watoto, ikiuonya ulimwengu mzima kuhusu maafa ya kibinadamu yasiyowahi kutokea iwapo itabaki kimya kuhusiana na mpango hatari wa wazayuni kuvamia Rafah, inayokusanya wakimbizi milioni moja na nusu walioacha makazi na ardhi zao kaskazini, kati kati na kusini mwa Gaza wakitafuta mahali salama.

Pia, Al-Azhar inatoa wito wa kuungana ili kukabiliana na jinai za mamlaka ya kizayuni dhidi ya Rafah, hasa baada ya kuziba masikio yake mbali na wito wa kimataifa zilizotolewa na pande mbalimbali katika jamii ya kimataifa, ikisisitiza kuwa kushindwa kutoa misaada kwa wapalestina wasio na hatia - leo na sio kesho - kutasababisha vifo vya maelfu ya wasio na hatia wakiwemo - wanawake, wazee, watoto na vijana – waliokimbia mbali na moto wa uadui wa kizayuni, katika jinai mpya ya mauaji ya kimbari inayongozwa kwa historia ya uhalifu wa mauaji ya kimbari uliofanywa na mamlaka hiyo tangu zaidi ya miaka 75.

Wanazuoni wa Al-Azhar wanaitaka jamii ya kimataifa na asasi za kijamii kuwajibika kwa majukumu yake mbele ya ubinadamu wao na dhamiri zao kulingana na tishio hilo la janga maradufu; kupitia mauaji ya kimbari, kuzuia misaada ya kibinadamu inayotosha Ukanda wa Gaza, na kumaliza nyanja zote za maisha katika Ukanda uliotengwa.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.