Uislamu wakataa Uadui, Uharibifu na Ufisadi katika Nchi

Imeandaliwa na: Dkt., Alaa Salah Abdulwahed

  • | Thursday, 22 February, 2024
Uislamu wakataa Uadui, Uharibifu na Ufisadi katika Nchi

    Kimsingi, Uislamu ulipiga vita ufisadi na kupinga sana uharibifu tangu siku ya kwanza ya utume wa Mtume (S.A.W.) ambapo ujio wa Uislamu ni kama mapinduzi yaliyopindulia ufisadi na uovu ulioenea katika jamii ya waarabu wa kabla ya Uislamu. Waarabu walioishi katika enzi ya ujahili walikuwa wanafanya maovu yote, kwa hiyo Uislamu ulikuja kwa ajili ya kumaliza na kutangaza kukataa kwa vitendo vibaya vingi vilikuwa vikifanywa ambavyo haviafikiani na maumbile ya kibinadamu wala havitokani na dini wala itikadi iliyo sahihi.

Kwa hakika vitendo vyote vya uharibifu na ufisadi havifanywi ila na wahalifu wavunjaji wa sheria zote ambao hawajali dini, maumbile wala chochote isipokuwa maslahi yao tu, na wala hawana huruma kwa wengine kwa kuwa tabia zao zimechafuka wakawa wanafanya makosa kwa makusudi wakidhani kuwa hawataadhibiwa duniani wala Akhera. Waharibifu na wafisadi hawa wanasababisha kuvuruga maisha na kupoteza amani na utulivu wa jamii.

Sheria ya kiislamu ni sheria ya msamaha na amani kwa wanadamu wote, imekuja kwa ajili ya kuhakiksha maslahi za watu na kuzuia ufisadi, jambo ambalo ndilo msingi wa ujumbe wa Mitume wote, ambapo kuboresha hali na kutengeneza jamii ilikuwa njia ya Manabii na Mitume (A.S.) tukiangalia aliyoyasema Nabii Shua’ib (A.S.) kwa kaumu wake akiwaita kwa imani: {Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze vipimo na mizani. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni adhabu ya Siku kubwa hiyoitakayo kuzungukeni * Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo na mizani kwauadilifu wala msiwakhini watu vitu vyao; wala msieneze uovu katika nchi mkafanya uharibifu} [11/84-85].

Hivyo, Nabii Shua’ib hakutosheleka kwa kuwakataza kaumu wake kupunguza katika vipimo na kufanya ufisadi katika nchi, bali alisisitiza tena katika aya inayofuata kuwakataza udanganyifu na upungufu katika vipimo na pia alitilia mkazo kuwakataza ufisadi katika nchi, jambo linaloeleza uzingatifu wa Nabii huyu kuwazuia kaumu wake kuwa wafisadi kwa kuwa ufisadi huharibu kila kitu na kugeuza mema yawe shari na maendeleo yawe uharibifu. Pia, Qurani Takatifu imetukumbusha kuwa mtu anatakiwa kujaribu kutengeneza mazingira anakoishi kadri awezekanavyo kama alivyosema Nabii Shua’ib alipokata tamaa kurekebisha hali ya watu wake: {Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninayo dalili wazi inayo tokana na Mola wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayokukatazeni. Sitaki ila kutengeneza kiasi ninavyo weza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye ninategemea, na kwake Yeye naelekea} [11/88].

Kwa kuangalia aina ya ufisadi na uharibifu tunatambua kuwa kuna aina mbalimbali za ufisadi na aina iliyo mbaya zaidi ni ufisadi wa itikadi ambapo itikadi ikiwa mbaya kila kitu huwa baya. Pia, uharibifu unagawanyika katika aina tofauti kama vile; kuharibu mashirika ya umma na kupora mali ya taifa ambayo ni ukiukaji mkubwa unaosababisha maovu makubwa katika nchi na vurugu mbaya katika jamii, kwa hiyo Mwenyezi Mungu Ametangaza adhabu kali mno kwa wanaofanya ufisadi wa aina hii: {Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa} [5/33].

Kwa hakika maovu na mabaya yako katika sura nyingi sana na yanagawanyika katika madhambi makubwa makubwa kama vile kumuua mtu asiye na hatia, zinaa, wizi, kunywa pombe na dawa za kulevya n.k. au madhambi madogo madogo yaliyo mengi, maovu haya yote yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu (S.W.) kwa ajili ya kulinda nchi na kuhifadhi jamii za kibinadamu kutokana na shari ya vurugu na kuuana.

Kutokana na hayo, kukataa kwa Uislamu kwa aina na namna zote za uharibifu, uadui na ufisadi ni jambo la msingi lisilo na shaka hata kidogo, ambapo Uislamu ni dini ya kukuza na kuhuisha nchi na ulimwengu, hivyo haikubaliki kuwa dini hiyo hiyo inayohimiza kujenga na kuendeleza nchi na kuhakikisha ustawi na maendeleo ichocheza uharibifu au uadui au ufisadi, bali ni dini inayopigana na aina zote za kusababisha madhara kwa wanadamu au hata wanyama na vitu visivyo hai.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.