Jinai za Mauaji ya Kimbari nchini Palestina yaharibu Urithi wa Kitamaduni na Kihistoria

Makala imefasiriwa na; Bw. Eslam Ragab Mohammed

  • | Thursday, 29 February, 2024
Jinai za Mauaji ya Kimbari nchini Palestina  yaharibu Urithi wa Kitamaduni na Kihistoria

     Katika vita vyake vinavyoendelea dhidi ya wapalestina, mamlaka ya kizayuni haikutegemea tu njia za kijeshi, mbinu za kisiasa, uhamishaji kwa nguvu, utekaji nyara, na mauaji ya kimbari, lakini pia ilijaribu kuharibu makumbusho ya kitamaduni na kitaifa, na kila kinachokuwa ushahidi juu ya unyakuzi wa ardhi na historia; katika jaribio lililoshindwa, linalenga vipengele vya kibinadamu vya Palestina na huathiri kumbukumbu ya vizazi vyote vilivyofuata.

Hata kabla ya kuikalia Palestina, mamlaka ya kizayuni ilijaribu kufuta na kupotosha utambulisho wake wa kihistoria na kidini wa Palestina kwa njia mbalimbali, miongoni mwa njia hizo ni: kubadilisha hali na tabia ya Kiarabu (ya Kiislamu na Kikristo) kutoka kwa matakatifu ya kidini na maeneo ya kihistoria, na kuweka badala yake sifa za Kiyahudi.

Utambulisho ni "ishara, au elementi ya pamoja ambalo linalowakusanya watu wote wa taifa, katika ushirikiano, kushikamana, uaminifu, na kiburi, na hayo yana utakatifu wake kwa sababu hayatiliwi shaka na mtu yeyote, na pia ni utambulisho unaoshirikiwa na wote, kulingana na asili ya kitamaduni na ya kihistoria, na kuushambulia huathiri taifa nzima, wakati huo huo huathiri kila mtu peke yake, na kukata tamaa katika siku zijazo". (Ahmed Baalbaki na wengine: Utambulisho na Masuala yake katika Ufahamu wa Waarabu wa Kisasa, toleo la kwanza, Kituo cha Masomo ya Umoja wa Waarabu, Beirut, 2013, uk. 25)

Majaribio ya kuijaalia Palestina ni wa kuyahudi yamechukua njia nyingi, na yanahitaji maandishi ili kuhesabiwa na kurekodiwa kwa utaratibu kwa ajili ya kuhifadhi historia na utambulisho wa kipalestina, hasa uzinduzi wa neno "Mlima wa Hekalu" juu ya Msikiti wa Al-Aqsa, na vile vile kuuhusisha "Msikiti wa Bilal" kati ya Jerusalem na Hebroni kwa Bibi "Raheli, mke wa Nabii Yakub." na mama wa Nabii Yusuf” badala ya sahaba “Bilal bin Rabah,” kuutenga na mazingira yake ya Palestina, na kuizunguka kwa kuta na minara ya kijeshi, miongoni mwa Fomu hizi pia ni kuiba makaburi ya kihistoria na kuyaonyesha katika makumbusho ya Kizayuni kwa majina na tarehe za uongo, pamoja na kutoruhusu kurejeshwa maeneo ya kihistoria na kiakiolojia ambayo yameporomoka kwa sababu na wakati, operesheni za uharibifu wa Wazayuni, na kumkamata mtu yeyote anayejaribu kurejesha maeneo haya ya makaburi.

Uvamizi huo umezidisha kasi ya kufutilia mbali utambulisho wa kihistoria wa Wapalestina, katikati ya vita vya sasa vya Ukanda wa Gaza, kwa kulenga na kuharibu maeneo ya kiakiolojia na ya kihistoria ya Wapalestina, pamoja na: Uharibifu wa misikiti: Uvamizi wa Wazayuni uliharibu misikiti mingi huko katika Ukanda wa Gaza. Kwa mujibu wa ofisi ya vyombo vya habari vya serikali huko Gaza, uvamizi wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza kuanzia Oktoba 8, 2023 hadi sasa umeharibu kabisa misikiti (140), na umesababisha uharibifu tofauti kwa misikiti (240).

Video nyingi zilizosambaa kwenye vyombo vya habari zilirekodi shauku ya wanajeshi waliovamia kwa mabomu na kuidhalilisha misikiti, kama vile kupandisha bendera ya Kizayuni juu ya msikiti wa "Moaz bin Jabal" wakati wa kuvamiwa kwa kambi ya "Al-Fawwar", kusini mwa Al- Khalil, na uharibifu wa misikiti ya "Bilal bin Rabah" huko "Deir Al-Balah", na "Al-Awda" katika "Jabalia", na "Al-Omari", ambayo ilianza miaka 1400 iliyopita; ambapo mnara wake pekee uliobakia kutoka msikiti huo, na Msikiti wa “Othman bin Qashqar”, ambao ulikuwa katika mji wa kale katika eneo la “Zaytoun”, mashariki mwa Mji wa Gaza, na ulianza miaka 800 iliyopita, uligeuzwa kwa rundo la kifusi. Uharibifu wa Makanisa: Uvamizi huo haulengi tu maeneo ya kidini na kihistoria kwa Waislamu, kwa sababu lengo lake sio tu kuondoa historia na utambulisho wa Kiislamu, bali ni kuondoa utambulisho wa kihistoria na kidini wa Wapalestina bila kujali madhehebu na imani zao, hivyo ndivyo alivyoashiria kwake kasisi wa Kipalestina Dakta Mitri Al-Raheb aliposema kwamba ukiukaji wa mamlaka ya Kizayuni hauathiri misikiti pekee bali pia makanisa. Akaongeza kwamba kanisa ya Al-Qiama katika siku kuu ya Al-Qiama hujazwa kwa askari na polisi, hata ndani ya kanisa. (Al-Shorouk, Novemba 22, 2023 BK).

Tangu mwanzo wa Vita vya Oktoba 8 hadi leo mamlaka wa Kizayuni wenye uporaji umelenga makanisa matatu ya kihistoria, ambayo ni "Monasteri ya Mtakatifu Hilarion" katika "Nuseirat", "Kanisa la Byzantine Jabalia,” ambalo lina umri wa zaidi ya miaka 1,600, na “Kanisa la Mtakatifu Porphyrius” Nalo ni kanisa la Othodoksi la Ugiriki ambalo lilikuwa kitovu cha kuwahifadhi na kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji, hasa nyakati za migogoro. Maofisa wa kanisa walisema kwamba kuyalenga makanisa na taasisi zake, pamoja na makazi yanayotoa kulinda kwa raia wasio na hatia, haswa watoto na wanawake waliopoteza makazi yao kutokana na shambulio la bomu la Israeli kwenye maeneo ya makazi ... ni uhalifu wa kivita ambao hauwezi kupuuzwa. "Kwa mujibu wa CNN mnamo Oktoba 20, 2023 AD.

Uharibifu wa vituo na taasisi za kitamaduni: Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Palestina "Wafa" mnamo 6 Desemba 2023 AD, uvamizi wa Kizayuni uliharibu wakati wa vita vya sasa vya Ukanda wa Gaza (21) vituo vya utamaduni, pamoja na makumbusho 8, miongoni mwao ni Makumbusho ya Rafah, Makumbusho ya Al-Qarara, Makumbusho ya  Khan Yunis ... na wengine, pamoja na kuharibu zaidi ya nyumba 70 za kiakiolojia, kwa mujibu wa shirika la “Urithi wa Amani”. Jambo linalostahiki kutajwa kwamba makumbusho haya yana mamia ya zana zinazohusiana na urithi wa kale wa Palestina, kutoka mitindo ya kale na zana zinazoonyesha utamaduni wa wabedui, wakulima, na wakazi wa mji huo. Uvamizi wa Wazayuni pia ulishambulia kwa bomu Kituo cha Utamaduni cha Orthodoksi huko Gaza, ambayo ni moja ya taasisi za kitamaduni na michezo zinazohusishwa na Kanisa la Orthodoksi (RT Kiarabu, 31 Oktoba, 2023 BK).

Meya wa Gaza pia alisema kwamba kundi la waporaji liliharibu jengo kuu la kumbukumbu, ambalo lina maelfu ya hati za kihistoria zilizo na umri zaidi ya miaka 150, kulingana na kile kilichochapishwa na tovuti ya Khabargazari Mehr mnamo Novemba 29, 2023. Pia liliharibu Kituo cha Rashad Al-Shawa cha Utamaduni katika Jiji la Gaza, ambacho kinazingatiwa ni kituo maarufu zaidi cha kitamaduni huko, ambapo kilianzishwa mnamo 1985 AD na kilikamilika mnamo 1988 AD katika kitongoji cha Al-Rimal. Uvamizi wa Wazayuni pia uliharibu eneo la kiakiolojia la Al- Balakhiya, na bandari ya kale ya Gaza (bandari ya kiakiolojia ya Anthedon) kaskazini-magharibi mwa Jiji la Gaza, ambayo ujenzi wake una umri wa miaka 800, na unaorodheshwa kwenye Orodha ya Awali ya Urithi wa Dunia na Orodha ya Urithi wa Kiislamu. (Ukurasa wa Wizara ya Utamaduni ya Palestina kwenye Facebook kwa tarehe 12/6/2023 AD), zaidi ya hayo, ndege za kivita za mamlaka ya Kizayuni ziliharibu “Nyumba ya Al-Saqqa” ya kiakiolojia katika kitongoji cha Al-Shuja'iya, mashariki mwa Mji wa Gaza, ambao ujenzi wake ulianza (400) miaka iliyopita kwenye eneo la mita (700).

Jinai hizi dhidi ya urithi wa kiutamaduni na kihistoria wa Wapalestina ambao unabeba thamani na alama za msingi kwa ajili ya kuhifadhi utambulisho wao, si hatari kidogo kuliko jinai za mauaji ya kimbari, na kuwahamisha watu kwa kulazimisha yanayofanywa na Wazayuni katika maeneo yote ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu, na matokeo yake yanatumikia malengo ya uvamizi wa chuki na majaribio yake ya kufuta utambulisho wa Palestina, na kulazimisha ukweli wa uwongo uliojaa uwongo na hadithi za uzushi, wakidhani kwamba vizazi vijavyo vitasahau historia yao kwa kupita wakati na kuamini ukweli wa uwongo, lakini jambo hilo ni mbali sana. Vizazi vya leo huko Palestina na nchi za Kiarabu na Kiislamu, na hata Magharibi baada ya Vita vya 8 Oktoba, vinatambua zaidi kuliko hapo awali, historia ya suala la Palestina.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.