Hekima na Mawaidha Mema ndiyo Misingi ya Hotuba ya Kidini katika Uislamu

Imeandaliwa na: Dkt., Alaa Salah Abdulwahed

  • | Friday, 1 March, 2024
Hekima na Mawaidha Mema ndiyo Misingi ya Hotuba ya Kidini katika Uislamu

     Kwa jumla mbinu nyingi za msini za Da'awa zinatokana na hekima na kutoa mawaidha mema na kujadiliana na watu kwa namna iliyo bora bila ya kupuuza wala kubagua mtu yeyote wala maoni yoyote, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora} [Al-Nahli: 125].

Mbinu za Da'awa na ulinganiaji kwa Mwenyezi Mungu zina nafasi kubwa katika Uislmau, kulingana na umuhimu wake kuwafikisha watu kwenye njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, mbinu hizo zilikuwa za viwango na aina mbalimbali kama vile, ulinganiaji wa kidogo kidogo, mahojiano, maswali na majibu, tashbiha na kutoa mifano, kupendeza na kuhofisha, n. k. Mbinu hizo zote na nyinginezo zimetumiwa na Mtume (S.A.W.) katika kazi yake ya kuwalingania watu kwa Uislamu, ambapo mlinganiaji yeyote hutakiwa kutumia mbinu mbalimbali hizo ili aweze kufanikiwa katika Da'awa yake. Pia, mlinganiaji hupaswa kutambua mbinu hizo na namna ya kuzitumia kuhudumia Da'awa na kufikisha ujumbe.

Kwa hiyo, Mtume (S.A.W.) alipotaka kutuma Mua'adh bin Jabal (R.A.) kwa Yemen kwa ajili ya kuwaita watu wake kwa Uislamu na kuwasaidia wafahamu mambo ya dini yao, alimwelezea hali ya mambo ya wayemen na kuwa wao ni watu wa kitabu, akamwamuru awafahamishe Da'awa kidogo kidog, kwani akiwaombea wote wasilimu mara moja, wakubwa wa watu hawatakubali kwa kuwa wamezoea kuwa na nafasi ya juu zaidi kulio wengine, kwa hiyo afadhali waitwe kwa njia ya mahojiano yaliyo mema na kwa upole, kama Alivyoeleza Mwenyezi Mungu katika kauli yake: {na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora} [Al-Nahli: 125].

Ifahamike kuwa mlinganiaji anatakiwa awe na maarifa ya kutosha kuhusu hali ya watu ambao anataka kuwalingania, maana watu wako tofauti katika kiwango cha imani, wapo wanaoamini kuwepo Mungu Mmoja na wapo wanaoamini kuwepo Miungu Mingi, au ni miongoni mwa wale wanaoshawishiwa na anasa za dunia, au ni wenye elimu na ujuzi wa kiwango fulani kinachohitaji hotuba ya kiwango kinacho sawa na elimu na ujuzi huu kama vile viongozi wa dini nyinginezo na wataalamu wake wanatakiwa kulinganiwa kwa kutumia mbinu maalum yenye kufahamu maelezo ya kutosha ya Qurani Takatifu na Sunna za Mtume pamoja na kufahamu mengi kuhusu dini nyinginezo na mambo ya pamoja baina ya dini hizo na Uislamu na mambo yanayotofautiana na Uislamu. Vile vile, mlinganiaji hutakiwa kuwa na ujuzi na uzoefu wa kujadiliana na wengine wanaopinga Da'awa yake na kutoa hoja za kuthibitisha usahihi wa maoni yake.

Zaidi ya hayo, kwa mlinganiaji kuelewa hali ya wanaolinganiwa ni kazi muhimu inayomsaidia kuchagua njia mwafaka ya kuwahotubia walinganiwa kwa mujibu wa viwango, vyeo na nafasi zao, kwa hiyo Mtume (S.A.W.) alikuwa anawaelekeza maswahaba umuhimu wa kutambua hali ya walinganiwa na kuwahotubia kulingana na hali yao, hata alipokuwa anawatumia wafalme na viongozi wa mataifa mbalimbali kuwalingania kwa Uislamu alikuwa anawaita kwa majina na lakabu wanazozipenda, Al-Bukhariy amesimulia katika kitabu chake kutokana na Ibnu Abbas (R.A.) kwamba Mtume alipotaka kutuma ujumbe kwa Kaisar (Mfalme wa Ruum) aliandika: "Kutoka Mohammed mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa Heraql Mtukufu wa Al-Ruum".

Hayo yote yanakuja miongoni mwa hikima iliyotajwa na Mwenyezi Mungu wakati kumwambia Mtume wake njia bora ya ulinganiaji, kwa hiyo walinganiaji wote wanatakiwa kufuata njia hiyo hiyo. Kama kwamba ulinganiaji kwa kutegemea mawaidha mema huwa na athari kubwa kufanikisha kazi na kufikisha ujumbe, kwani inaziathiria nafsi na kuzivuta kwa kiasi kikubwa kuliko mbinu ya kuhofisha na kutishia.

Wakati huo huo, mbinu ya kuhofisha wakati mwingine mlinganiaji huwa hana budi kuitumia katika Da'awa yake, kama alivyofanya Mtume (S.A.W.) pamoja na watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo) aliposema: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu Anayeshika nafsi yangu mikononi mwake myahudi au mkristo yeyote atakaepata habari ya utume wangu mimi kisha anakufa ilhali hajaamini niliyokuja nayo basi hatima yake ndiyo motoni".

Ama kwa upande wa kutumia mbinu ya kuwapendeza na kuwavuta walinganiwa kupitia kuwaahidi kwa malipo mema na ya haraka duniani na yaliyo mazuri zaidi huko Akhera, iliyokuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu (S.A.W.): {Na lau kuwa Watu wa Kitabu wangeli amini na wakachamngu hapana shaka tungeli wafutia makosa yao,na tungeli waingiza katika Bustani zenye neema* Na lau kuwa wangeli ishika Taurati na Injili nayote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao} [Al-Maidah: 65-66]             

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.