Umuhimu wa kushirikiana kuhakikisha Manufaa ya jamii na Ustawi wa Nchi

Imeandaliwa na: Dkt. Alaa Salah Abdulwahed

  • | Monday, 4 March, 2024
Umuhimu wa kushirikiana kuhakikisha Manufaa ya jamii na Ustawi wa Nchi

     Mwenyezi Mungu (S.W.) Amewahimiza wanadamu kushirikiana katika mema na kusaidiana katika juhudi za kuleta mafanikio ya jamii kwa jumla. Ushirikiano ni sifa mojawapo sifa njema ambazo wanadamu wanatakiwa kuwa nazo kwa kuwa huchangia kwa kiasi kikubwa katika kukidhi mahitaji ya maendeleo ya jamii na ustawi wa umma. kwa hivyo, waislamu wanatakiwa kushirikiana na wenzao katika kuendeleza nchi na kuboresha hali ya jamii. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui} [Al-Maidah 2]

Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu Amemwumba mwanadamu kiumbe dhaifu anayehitaji wakati wote kwa msaada wa wengine kwa ajili ya kutekeleza mikakati na matarajio yake, jambo hili liko wazi kuhusiana masuala yote ya dunia ambapo mwanadamu kwa mujibu wa maumbile yake hana uwezo wa kufanya yote anayoyataka binafsi, bali yuko na haja kwa wanaomsaidia kufika malengo yake. Kwa hiyo, maumbile yalimbidi mwanadamu asaidiane na wenzake na kushirikiana nao kuhusu masuala mbalimbali ya maisha.

Waislamu wanatakiwa kusaidiana na kushikamana katika mambo ya dunia na dini, Mwenyezi Mungu Ametoa amri ya kushirikiana na kusaidiana katika aya kadhaa za Qurani Takatifu kama vile: {Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu} [5/2]. Hivyo tunaona kuwa Uislamu umezingatia sana suala hilo la kushikamana na kusaidiana baina ya wafuasi wake wenyewe kwa wenyewe na wao na wengine kwano dini hiyo inazingatia sana uhusiano uliopo baina ya mtu na mtu kama ilivyo uhusiano uliopo baina ya mtu na Mola wake.

Kwa mujibu wa sheria ya kiislamu mwislamu anatakiwa kuhifadhi uhusiano wake na watu wote kwa lengo la kuhakikisha ushirikiano ambao ni msingi muhimu wa mafanikio katika jamii yoyote, tena ni dini inayohimiza kuimarisha misingi ya kujuana, kukamilishana, kushikimana na kusaidiana kwa hiyo mtajiri anatakiwa kumsaidia maskini, mwenye nguvu anatakiwa kumsaidia mnyonge, mwenye elimu anatakiwa kumsaidia asiye na elimu na kadhalika. Kwa jumla dini ya Uislamu unawaelekeza wafuasi wake wawe kama mwili mmoja kuhurumiana na wawe na umoja usiofunguliwa kwa sababu yoyote. Si kusaidiana baina ya waislamu wenyewe kwa wenyewe tu, bali waislamu wanatakiwa kujuana na kukamilishana na wanadamu wote kwa ajili ya kuendeleza jamii na kukuza nchi, Mwenyezi Mungu Anasema: {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliyemchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari} [49/13].

Vile vile, uhusiano baina ya mwislamu na wanadamu wengine sawa ni waislamu au la unaasisiwa kupendana kutokana na hadithi ya Mtume (S.A.W.): “Hakika mmoja wenu hawi mwislamu mwenye imani kamili mpaka amtamani nduguye kama anavyojitamani yeye mwenyewe”. Kwa hiyo mshikamano wa kiislamu unamaanisha kushirikiana na kusaidiana na kufuta tofuti yoyote na sifa yoyote ya kutofautisha baina ya mwislamu na mwingine na kutangaza umoja na undugu katika Uislamu na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (S.W.) Aliyesema: {Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka} [3/103], na kauli yake: {Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi} [21/92].

Naye Mtume (S.A.W.) alifananisha waislamu na mwili mmoja ambapo kiungo kimojawapo vingo vya mwili huu kikiwa na maumivu basi mwili mzima huteseka na kuumwa: “Kwa hakika kila muumini kwa muumini mwenzake ni kama ukuta unaoshikamana vizuri akafubga vidole vyake pamoja”, namna hii tunatambua kuwa umoja na kushikamana ni msingi mojawapo misingi ya dini hii adhimu, wakati ambapo kufarikiana na kugongana au kuzozana huwa kinyume na ukweli wa dini na nje ya mafunzo yake.

Mwenyezi Mungu Anatoa onyo kali kwa waumini wasifarikiana baada ya kuunganishwa mfano wa watu wa kitabu wasipotee kama walivyopotea: {Wala msiwe kama wale walio farikiana na kukhitalifiana baada ya kuwafikia hoja zilizo wazi. Na hao ndio watakao kuwa na adhabu kubwa} [3/105]. Kwa upande wake Mtume (S.A.W.) alikuwa anawatahadharisha maswahaba zake na waislamu wote mara kwa mara kutokana kutofautiana wala kuhitilafiana akibainisha kwamba kufarikiana husababisha maadui waweze kutushinda kwa urahisi ilhali umoja unawapa waislamu nguvu ya kuilinda dini kuihifadhi imani, kwa hiyo Mtume alikuwa anawahimiza waislamu kuwa na umoja katika hali zao zote na kuwatii viongozi wao na kushikamana na nguzo za dini pasipo na kukoseana wala kugombana.

Swahaba Al-Erbadh bin Sariya alisimulia hadithi kuwa siku moja Mtume aliwapa maswahaba zake wasia nzito mpaka maswahaba wengi wao waliathirika sana na kulia wakisema: Ewe Mtume wetu hakika umetuusia anavyofanya aliye yuko karibu na kifo chake kwa hiyo tunaomba mawaidha zaidi tena wasia na nasaha, akasema Mtume (S.A.W.): “Nakuusieni kwa uchamungu na utiifu kwa kiongozi wenu hata akiwa mtumishi, kwa kweli atakaeishi baada ya kifo changu mimi ataona hitilafu na mizozo mingi, basi hapo shikamaneni kwa sunna zangu na watakaokuwa nayo makhalifa wangu walioongoka na epukaneni na mambo yanayojitokeza na kuibushwa katika dini

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.