Madrasa za kufundisha Qurani nchini Tanzania Urithi Takatifu wa Kiislamu

  • | Thursday, 7 March, 2024
Madrasa za kufundisha Qurani nchini Tanzania Urithi Takatifu wa Kiislamu

 

     Tanzania ni Muungano kati ya Tanganyika, lililoko ndani ya bara la Afrika upande wa mashariki, ambalo lilipata uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1961 AD, na kisiwa cha Zanzibar, kilichoko mashariki yake katika Bahari ya Hindi, ambacho kilijiunga na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964 AD, Nayo ni  nchi inayojumuisha majimbo 61, ukubwa wake 947.3 km2, na idadi ya watu wake takriban milioni 61.7. Waislamu Tanzania bara wanawakilisha kati ya asilimia 30 hadi 40 ya idadi ya watu, ilhali wanawakilisha zaidi ya 97% ya wakazi wa Zanzibar[1]. Mji wake mkuu wa kitamaduni ni Dar es Salaam, Pia ulikuwa mji mkuu wa utawala hadi Dodoma ilipoibadilisha mwaka 1974 AD.

Historia ya Uislamu katika nchi hii ni ndefu, ambapo ilianza tangu karne ya kwanza H.j. wakati Waomani walipohamia Afrika Mashariki na kuanzisha falme kadhaa huko, wakabakia Zanzibar hadi mwaka 1964 A.D., Wakati Waafrika wa huko walipompindua sultani wake wa mwisho, Jamshid bin Abdullah Al-Busaidi na serikali yake, Baada ya hapo, uwepo wa Waarabu nchini Tanzania ulipungua, Idadi ya wakazi Waislamu ikaanza kupungua polepole baada ya kuwakilisha asilimia 90 ya idadi ya wakazi[2], ingawa sehemu ya kitamaduni ya Waarabu kwa ujumla na sehemu ya dini ya Kiislamu haswa inawakilisha uwepo muhimu.

Image

 

Mfano mashuhuri wa athari ya kiarabu na ya kiislamu nchini Tanzania ni kuenea kwa Madrasa za kufundisha Qur’an katika maeneo mbalimbali nchini humo, katika mazungumzo na Sheikh Ahmed Sadiq, mkurugenzi wa Madrasa ya Ibnu Abbas mjini Dar es Salaam, kutupa fikra kuhusu hali ya elimu ya Kiislamu nchini humo.

Ni nini hali ya elimu ya Kiislamu nchini Tanzania na hali ya madrasa za kiislamu nchini humo?

Zipo shule za kawaida za Kiislamu, ambazo hutoa huduma sawa sawa na shule za kibinafsi katika nchi za Kiarabu, ambapo ni shule za kiserikali, lakini zinafundisha mitaala ya Kiislamu pamoja na kozi za kawaida, shule ya aina hii naitwa kwa Kiingereza "School", pia zipo Madrasa za kufundisha Qur’an ambazo wanafunzi wa shule za msingi  wanajiunga nazo, nchini Tanzania wanaziita “Madares”  Neno “Madrasa” kwa Kiarabu maana yake hapa ni shule ya kufundisha na kusomesha Qur’an; na ni kama "Al-Khalwah" ambayo imeenea katika nchi zote za Afrika.

Madrasa hizi zinagawanyika katika sehemu mbili; Madrasa za kufundisha Qur’an kwa watoto wadogo, Na taasisi zinazofanana na vituo vya kuandaa walinganiaji wa dini katika nchi za Kiarabu, hizi ni shule za kibinafsi zinazofundisha taaluma za Kiislamu, Wanafunzi hutumia siku nzima huko, wakila, kunywa na kulala, na ni kwa viwango vyote vya elimu. ya msingi, ya kati na ya sekondari.

Nini  kazi za Madrasa za kufundisha Qur’an nchini Tanzania?

Madrasa za kufundisha Qur’an zinaenea nchini Tanzania nzima kadiri Uislamu ulivyoenea huko, unapata kwa uchache Madrasa moja au mbili katika kila kijiji, na idadi ya watoto inatofautiana kutoka wanafunzi 30 hadi 200. Tunaweza kusema kwamba Wastani ni wanafunzi 70 katika kila Madrasa. Nazo ni Madrasa za maskini, majengo yake ni dhaifu, kwa sababu wanakijiji ni maskini, wanafunzi hawawezi kulipa ada zinazosaidia katika kuendeleza shule, inasimamia kusomesha Qur’an pekee, hazifundishi mitaala mingine ya kisheria, ikiwemo lugha ya Kiarabu, kwani hamu ya  kuifundisha ni dhaifu sana, baadhi ya dua husomwa kwa watoto, ambazo ni sehemu ya urithi wa kidini wa watu wa nchi hii.

Kwa Watanzania, lengo kuu la kuanzisha Madrasa hizi ni kubarikiwa na Qur’an na mawaidha mema, inawarithisha watoto tangu wakiwa wadogo tabia ya kuheshimu sana Qur’ani Tukufu na Mtume Muhammad (S.A.W.), wawe na bidii sana katika kuhifadhi shule hizi, aidha wanafunzi husoma asubuhi katika shule za serikali, wanaporudi kupumzika kwa muda wa nusu saa tu, basi huenda kwenye Madrasa hizi, kwao, shule hizi za Qur'ani ni takatifu sana, kama misikiti, ni sehemu muhimu ya maisha ya Mwislamu wa Tanzania.

Kwa kiasi gani Madrasa hizi zinaathiria wanafunzi?

Madrasa za kufundisha Qurani zina athari kubwa katika nafsi za watoto, bila shaka, kwani zinatia ndani yao kushikamana na dini na kuupenda Uislamu, lakini ukweli kuhusu kushikamana na dini hapa bado ni dhaifu; kwani wale wanaosimamia shule hizi - kwa sehemu kubwa - elimu yao ya kisheria ni dhaifu, na kiwango chao cha kujimudu katika lugha ya Kiarabu ni dhaifu mno, kwa hiyo, matokeo huwa dhaifu, na watoto huwa waislamu lakini uelewa wao kwa masuala ya dini huwa dhaifu.

Ni nini cha kufanyika ili kuendeleza Madrasa hizi?

Madrasa hizi zinahitaji kuongeza mitaala ya Sharia na kozi za kitaaluma kwa walimu ili kuzitekeleza, na msaada wa kifedha kwa walimu ili kuendeleza kazi hii, kwani wengi wao hawaendelei kufundisha kwa sababu hali zao za kifedha zinakuwa ngumu, ambapo wanalazimika kufanya kazi nyingine ili wapate riziki, hasa kwa wale waliooa na wana watoto na familiya, mapato kutokana na kufundisha hayakidhi mahitaji yao ya msingi.

Vipi kuhusu Madrasa yako wewe?

Kuhusu Madrasa yangu ni Madrasa ya Ibn Abbas iliyoko jijini Dar es Salaam, wengi wa wanafunzi wake ni watoto wa jamii za kigeni walioishi hapa, miongoni mwao Waarabu wa Yemeni, Wahindi na wengineo, na ni Madrasa ya kufundisha Qurani Tukufu, lugha ya Kiarabu, na taaluma za Kiislamu[3], lakini huwezi kulinganisha Madrasa yangu hiyo kwa Madrasa nyinginezo hapa nchini Tanzania, kwani kiwango chake ni duni kwa mpangilio, utaratibu, usimamizi na usafi, hii ndiyo asilimia kubwa zaidi, na tunajitahidi kuhakikisha kwamba Madrasa zote ziko katika kiwango sawa na Madrasa ya Ibn Abbas.

 

Mahojiano na Sheikh/ Ahmed Sadiq

Mkurugenzi wa Madrasa ya Ibnu Abbas, Dar es Salaam

Imefasiriwa na: Bw. Farid Mohammed

Imepitiwa na Dkt. Alaa Salah Abdulwahed

 

[1] Hakuna takwimu sahihi au yakinifu kuhusu idadi ya Waislamu nchini Tanzania.

[2] Waislamu walio wachache barani Afrika, Sayyed Abdul Majeed Bakr, uk 109.

[3] Madrasa hiyo ina kurasa kwenye mitandao ya kijamii zinazoonyesha jinsi ilivyo nzuri na safi, na jinsi juhudi nzuri zinavyofanywa na wanafunzi, tofauti na ilivyozoeleka katika madrasa nyingine za Qur'ani nchini Tanzania.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.5

Please login or register to post comments.