Wanadai .. Tunasahihisha

15

  • | Monday, 20 June, 2016

Madhehebu ya Maimamu wa waislamu toka enzi ya Mtume Muhammad (S.A.W.) mpaka siku za kisasa inatoa hukumu ya kuwa anayefanya madhambi hata yakiwa ni madhambi makubwa lakini hubaki Mwislamu, tunaombea Mwenyezi Mungu ampe toba na uongofu. Msingi huu ulikubaliwa na wote isipokuwa Al-Khawarij  ambao waliwakafirisha waislamu kwa kufanya madhambi, isitoshe bali waliwakafirisha Maswahaba wa Mtume (S.A.W.) kwa sababu ya madhambi, basi si jambo la ajabu kwamba wafuasi wa kundi hilo waliwakafrirsha wanajamii wote wa kiislamu bali pia ulimwenguni kote katika siku hizi za kisasa, inakumbukwa kwamba wazo la ukafirishaji kwa sababu ya kufanya madhambi linarejea kihistoria enzi ya kundi la Al-Khawarij waliomwasi Bwana wetu Imamu Ali bin Abi Twalib, wakamkafirisha yeye na maswahaba wengi kwa kudai kwamba maswahaba hao wamefanya madhambi na hatia, tunabidi kukumbuka kwamba Mtume (S.A.W.) ameonya sana kutoka Ukafirishaji kwa ujumla ambapo alisema katika hadithi yake iliyo sahihi: “Mtu ye yote anayemwita nduguye kuwa ni mkafiri basi mmoja miongoni mwao huwa ni mkafiri” na hiyo ni onyo kali kutoka ukafirishaji na hatima yake.
Kwa hakika wito hiyo ni dalili ya kuwa makundi yenye mawazo makali yanachagua mifano mibaya au mifano isiyo sawa katika historia ya kiislamu yote kisha wanaizalisha mifano hiyo upya wakakosa na hupatwa na hasara kama walivyofanywa waliotangulia wakapotea.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.