Ramadhani nchini Somalia

  • | Monday, 18 March, 2024
Ramadhani nchini Somalia

 

     Somalia ni nchi iliyopo Afrika mashariki kwenye eneo linalojulikana kama Pembe ya Afrika, imepakana na Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi kutoka upande wa mashariki, Ethiopia kutoka upande wa magharibi, Djibouti kutoka upande wa kaskazini-magharibi, na Kenya kutoka upande wa kusini-magharibi. Somalia ina eneo la kilomita za mraba 637,540.

Idadi ya Wasomali ni takriban watu milioni kumi. Nchi hiyo inazingatiwa kuwa nchi ya Kiislamu, kwani wengi wa wakazi wake ni Waislamu, na waislamu huko wanafuata shule ya Imamu Al-Shafi'i.

Kama desturi ya waislamu kila mahali, basi Wasomali wanaukaribisha mwezi wa Ramadhani kwa furaha kubwa, na wanapongezana kwa kufika kwake. Kwa sababu ya mgawanyiko wa kisiasa katika maeneo mengi, udhihiri wa mwezi huo unaweza kutofautiana katika baadhi ya sehemu mbalimbali. Kwa hivyo kila sehemu inafunga kwa muono wake wa mwezi wa Ramadhani, na wala haitegemewi kuona kwa wengine!! Baadhi ya watu wanaridhika na kile kinachosemwa na Ufalme wa Saudi Arabia kuhusu suala hili.

Waislamu huko wanadumisha Sunna ya daku (Suhuur), ambayo inajumuisha chakula kiitwacho (Hareez), (pasta), na (wali). Ama mlo wa futari, huanza na (tende), (maji), na baadhi maji ya matunda, kisha chakula kinaanza, kisha watu wanakwenda kuswali Almaghribi msikitini, na baada ya kumaliza Swala wanarudi nyumbani mwao ili kula chakula cha futari pamoja na familia zao, chakula hicho mara nyingi ni (wali) na (nyama). Meza ya futari pia inajumuisha vinywaji maalumu, kama vile kinywaji cha (ndimu) na (maziwa), aidha kuna aina nyingi kama (tende) na (keki).

Baada ya kula futari na baada ya watu kupata nguvu zao, kila mtu huenda misikitini –wanaume, wanawake, wazee, vijana, wadogo na wakubwa – ili kuswali Swala ya Tarawih, ambapo husaliwa rakaa ishirini katika misikiti mingi, katika baadhi ya wakati husemwa khutba nzuri wakati wa Sala ya Tarawih, na Qur'an huhitimishwa katika Sala ya Tarawih usiku wa tarehe ishirini na saba ya Ramadhani.

Masomo mengi ya kisayansi na vikao vya kusoma Qur’an hufanyika misikitini baada ya swala ya Tarawih, na katika misikiti mingine hufanyika kabla ya Swala ya jioni, na wanachuoni wa nchi hizo ndio wanaosimamia masomo na vikao hivyo.

Ama kuhusu Laylatul-Qadr basi Wasomali wanaamini kuwa ni usiku wa ishirini na saba ya Ramadhani, baadhi ya watu wanakaa misikitini hadi alfajiri, kisha wanasali swala ya alfajiri, kisha wanarudi nyumbani mwao.

Wasomali pia wanafanya ziara za kifamilia wakati wa Ramadhani, wakichangamka fursa ya kuwa mwezi huo ni wakati wa kukutana na kurejesha uhusiano kati ya watu.

Moja ya desturi mashuhuri baina ya Wasomalia ni kutangaza kwa pampja nia ya kufunga baada ya Swala ya Al-magharibi kila siku. Wanasema katika kundi: (Nakusudia kufunga kesho ili kutimiza faradhi ya Ramadhani).

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.