Ramadhani nchini Nigeria

  • | Wednesday, 20 March, 2024
Ramadhani nchini Nigeria

 

Nigeria ni nchi iliyopo Afrika magharibi, inapakana na Nigar kwa upande wa kaskazini, Chad kwa upande wa kaskazini mashariki, Cameron kwa upande wa mashariki, Binin kwa upande wa magharibi, pwani yake ya kusini iko kwenye Ghuba ya Guinea kwenye Bahari ya Atlantiki.

Mji mkuu wake wa zamani ni Lagos, lakini sasa hivi Abuja ni mji mkuu wake wa kisiasa na Lagos ni mji mkuu wake wa kibiashara, Nigeria ilipata uhuru wake tarehe 1 Oktoba 1960 kutoka kwa ukoloni wa Kingereza.

Kwa upande wa Lugha, zipo lugha nyingi za kinyeji nchini Nigeria kama vile Hausa ambayo ni lugha ya kwanza ya watu milioni 50, na lugha ya pili ya milioni 30 Pia, lugha ya Fulfulde ni lugha ya kinyeji ya pili ya milioni 24. Pia kuna lugha nyingine nyingi za kinyeji zinazofikia 500 lakini lugha rasmi nchini Nigeria ni kiingereza. Nigeria ina makabila nyingi, kama vile Hausa, Fulata, Burno, Yurba, Wigbo n.k.

Uislamu uliingia Nigeria mapema sana, ambapo nchi hiyo ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya Waislamu duniani kwa jumla na katika Bara la Afrika hasa, ambapo idadi ya waislamu ni zaidi ya asilimia 75 ya wakazi. Waislamu nchini Nigeria wanajikita zaidi katika majimbo ya sehemu ya kaskazini ya nchi hiyo, wakiwakilisha takriban 90% ya idadi ya wakazi wake, ilhali wakiwakilisha takriban 50% huku kusini.

Waislamu wa  Nigeria wanasherehekea sana kufika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Mara tu mwezi mwandamu unapothibitika, basi idadi kubwa ya Waislamu hukusanyika katika sherehe kubwa, wakirandaranda katika mitaa ya miji mikuu, wakibeba dufu na kuimba nyimbo za kuelezea furaha yao kwa kufika mwezi wa saumu.

 

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.