Ramadhani nchini Senegal

  • | Friday, 22 March, 2024
Ramadhani nchini Senegal

 

     Idadi ya Waislamu nchini Senegal ni 95%, na mwezi wa Ramadhani kwao ni ishara ya kiroho ya maadili mengi kama vile; mshikamano, ukarimu, uvumilivu, ushirikiano n.k. Maadili haya yanapitishwa kutoka kizazi hadi kizazi. Ambapo taasisi za hisani nchini Senegal zinajitahidi kujumuisha maadili haya makuu kwa kuandaa milo ya "Andgoa" katika lugha ya kienyeji ya "Wolof", ambayo ni milo ya kufuturu ambayo inasambazwa katika mji mkuu wa Senegal, "Dakar," kwa maskini, wahitaji, na madereva ambao wapo barabarani wakati wa kufuturu. Mlo huu unazingatiwa ni mojawapo ya mila maarufu zaidi ya ukarimu na mshikamano ambayo ni sifa ya nchi hii katika mwezi huu mtukufu.

Wasenegal pia hufanya desturi nyingine inayojumuisha maadili ya wema na mshikamano kati ya familia na wanajamii, nayo ni desturi ya "sukari kur" katika lugha ya kienyeji, ambayo ina maana ya (sukari ya Ramadhani), ambapo jamaa na familia hupeana sukari kama zawadi ili kuonyesha upendo kati yao katika mwezi huu mtukufu. desturi hii adhimu imekuwa ni wajibu wa wanawake kwa wanawake walioolewa, ambapo kwa njia hiyo wanathibitisha ukubwa wa mapenzi yao ushikamano wao kwa familia ya mume. Pamoja na hayo, desturi hii inaweza kuwakilisha mzigo kwa baadhi ya wanawake walioolewa kutokana na gharama anazozihitaji mwanamke aliyeolewa ili kupata zawadi hii, ambayo wakati mwingine inaweza kufikia mamia ya maelfu ya faranga za Senegali.

Kwa kuzingatia kwamba Senegali inahesabika kuwa miongoni mwa nchi kubwa za Kiafrika ambapo inajumuisha waumini wengi wa Kisufi, basi ibada za kiroho hasa zile zinazohusiana na mila za Kisufi ni nyingi na zinatofautiana katika mwezi huu. Wakati wa mwezi wa Ramadhani unapofika, Wasenegali wanashindana katika kusimamisha sherehe za jioni za Ramadhani zinazojumuisha duru nyingi za tenzi na dhikr. Misikiti haifungi milango yake katika usiku wa Ramadhani, lakini inajaa waabudu, kusoma Kurani Tukufu, na masomo ya kidini. Vijana nchini Senegali wanaacha mila ya kuzungumzana usiku kwa ajili ya kuheshimu utakatifu wa mwezi huu, unawakuta wao wakisikiliza nyimbo za dini, na baadhi yao wanajizoeza kuimba nyimbo za kidini na kusema wito wa sala (Adhani) kulingana na mbinu mahususi ya Kiafrika nchini Senegali.

Kuna tabia nzuri kwa Wasenegali wakati wa kufuturu, ambayo ni kuanza kufuturu kwao kwa maji au kinywaji chochote cha moto. Ambapo wanaamini kwamba kinywaji cha moto kinafaa zaidi kwa tumbo la mfungaji kuliko kinywaji baridi. Hata hivyo kufuturu kunatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine, kwani kila sehemu ina chakula chake kipendacho na ladha inayopendwa. Hayo yanasemwa pia kuhusu suhur ambayo waislamu huko bado wanaendelea katika kuishika, na sala ya Tarawih nchini Senegali haitofautiani na nchi nyingine za Kiafrika, isipokuwa wakati wa sala mitaa na barbara huwa haina watembea kwa miguu. Ambapo Waislamu wote hukimbilia kusali, mfanyabiashara anaacha biashara yake, muuzaji anaacha bidhaa zake, kila mtu anafunga duka lake, na shughuli ya kununua na kuuza inasimama hadi sala itakapomalizika. Kwa njia hii Waislamu wanajitahidi jatika kueneza utamabduni wa kiislamu pande zote za nchi, ambapo makundi ya Masufi wanakuwa na haraka zaidi na desturi zao zinazidi sana wakati wa Ramadhani na maelfu ya vijana hujiunga na wasichana kwenye madarasa yao.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.