Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kufuatia mkutano wa Imamu Mkuu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

  • | Sunday, 24 March, 2024
Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kufuatia mkutano wa Imamu Mkuu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

     Mheshimiwa Imamu Mkuu Profesa; Ahmed Al-Tayeb Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif alikutana siku ya Jumapili tarehe Machi 24, 2024 Bw. Antonio Guateresh katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye Makao Makuu wa Al-Azhar Al-Shareif mjini Kairo, Misri.

Katika mkutano huu pande mbili walitafiti masuala kadhaa na suala nyeti ya ulimwengu hasa suala la uadui wa kizayuni mjini Gaza na namna ya kusitisha maafa haya na mauaji ya kimbari yanayofanywa dhidi ya wapalestina.

Miongoni mwa matukio na maelezo ya mkutano huu yafuatayo:

  • Imamu Mkuu wa Al-Azhar ampe Guateresh tuzo ya Baraza la Wakuu wa Waislamu kwa kutahmini misimamo yake "shujaa" kuhusu wapalestina na kupambana na "islamophopia".
  • Imamu Mkuu: "Lazima tuungane na tushikamane ili kusimamisha mtiririko wa damu zisizo na hatia.".
  • Imamu Mkuu: "Kwa hakika kuendelea kwa hali ya kisasa mjini Gaza kutaeneza uharibifu na vita katika nchi zote duniani".
  • Imamu Mkuu atoa wito wa kusitisha janga hilo, akiashiria kuwa ni wajibu wetu sote, kwani wapalestina katika Ukanda wa Gaza wanateseka sana kwa sababu ya uhaba wa chakula na vinywaji na kuendelea kuenea kwa maradhi mbalimbali.
  • Imamu Mkuu: "Baadhi ya Mayahudi waadilifu watoka barabarani  ili kuomba kusitisha uadui wa kizayuni, na yaliyotolewa na jamii ya kimataifa kuhusu uadui huu ni juhudi finyu hazitoshi hata kidogo.
  • Imamu Mkuu: "Umethibitisha kwa misimamo yako ya kikweli kuwa tamaa na matarjio ya kuwanusuru wanyonge na wanaodhulumiwa yapo kwa kweli"
  • Imamu Mkuu: "Ulimwengu kwa kimya yake upo katika mwelekeo usio sahihi, ambapo maadili ya kibinadamu yalipotezwa na jinai za kikatili zinaendelea"
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: "Sikumbuki kipindi katika historia kilichoshuhudia dhuluma na unyanyasaji kwa kiasi hicho"
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: "Tunaendelea kuunga mkono uadilifu na kulitetea suala la wapalestina wa Gaza, wala hatuogopi kulazimishwa kukaa kimya"
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa: "Al-Azhar ni sauti yenye nguvu na ukweli na upande muhimu wa kuwatetea wapalestina, kwa upande wetu tutaendelea kushinikiza kuwataka jamii ya kimataifa kuhakikisha haki za wapalestina"

 

 

Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu

Kitengo cha Lugha za Kiafrika

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.