Uangalifu wa Uislamu kwa Mwanamke kwa mujibu wa Qurani na Sunna

Imeandaliwa na Dkt.; Alaa Salah Abdulwahed

  • | Wednesday, 27 March, 2024
Uangalifu wa Uislamu kwa Mwanamke kwa mujibu wa Qurani na Sunna

     Uislamu ndiyo dini iliyomtukuza mwanamke na kumheshimu sana, ikatangaza kuwa mwanamke katika hali zake zote inatakiwa aheshimiwe na kutukuzwa vizuri, kwa kuwa Mwenyezi Mungu (S.W.) Aliwausia waja wake wanaume wawajali wanawake na kuwasiadia wapate haki zao za kuwa na heshima na uhuru wa kumwezesha atekeleze majukumu yake katika jamii. Wakati huo huo, sheria ya kiislamu imebainisha kuwa wanawake wanatakiwa kusimamiwa kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde} Nisaa: 34.

Kwa hakika aya na hadithi za kuwausia wanaume kuwafanyia wema wanawake ni nyingi mno, ila zote zimekubaliana kuhakikisha kuwa miongoni mwa mafundisho yaliyo na umuhimu mkubwa katika dini yetu na kwamba wanawake wana haki sawa sawa na wanaume na wanatikwa kuwajibikia wajibu mfano wa wanaume. Pia, wanaume na wanawake wanapendelezana kutokana na msini wa uchamungu na kufanya mema, kama Alivyosema Mweyezi Mungu: {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliyemchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu niMwenye kujua, Mwenye khabari} Al-Hujurat: 13.

Inafahamika kwamba mwanamke ana nafasi kubwa katika jamii, mpaka huitwa "Nusu ya Jamii", ambapo mwanamke amepewa nafasi, majukumu na cheo anachoshirikiana na mwanamme kutakeleza wajibu wake, kwani mwanamke anamsaidia mwanamme maishani. Kwa hiyo, Uislamu inamheshimu mwanamke na kumpa nafasi ya juu, kwa kuwa huwa sehemu ya maisha samabamba na mwanamme.

Kwa kuangalia hali ya mwanamke enzi za Jahiliya kabla ya ujio wa Uislamu na hata katika enzi za Warumi na Wayunani tunaona namna watu wa enzi hizi walikuwa wanamzingatia mwanamke kati ya vitu vya anasa na vifaa vinavyotumika nyumbani, kwa hiyo hakuwa na haki yoyote, ambapo mke anayefiwa na mumewe alikuwa halali kwa ukoo wake bila ya kuomba ridhaa yake. Imamu Al-Bukhariy alisimulia kuwa mwanamke wa enzi hizo hakuwa na haki ya kuchagua mumewe na hasa aliyefiwa na mumewe basi ukoo wake walikuwa wanashauriana akitaka mmoja wao kumwoa, au pengine kumwolewa kwa mwingine au kumzuia asioe, maana wao peke yao wanao haki ya kuainisha hatima yake kuliko yeye mwenyewe wala ukoo wake.

Pia, desturi za Waarabu kabla ya Uislamu zilikuwa zinawaruhusu kumshutumu mwanamke ambaye hawamtaki tena kwa zinaa ili aogope fedheha ambayo haipo kabisa na kulipa mahari aliyopewa kwa ajili ya kupata uhuru wake. Mwenyezi Mumgu Amesema kukataza haya: {Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa - isipo kuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake * Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi? * Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?} [An-Nisaa: 19-21].

Uislamu ilipokuja hali ya mwanamke imebadilika, ambapo mwanamke ametukuzwa akapewa haki zake akiwa sawa sawa na mwanamme kuhusu majukumu ya maisha ambapo kwa mtazamo wa Uislamu mwanamke ndiye msaidizi wa mwanamme na mwanamke bora zaidi ni yule anayemsaidia mumewe kuwajibika majukumu ya maisha, kama Mwenyezi Mungu (S.W.) Alivyoeleza sifa za mwanamke bora katika kauli yake: {Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu} [An-Nisaa: 34].

Haya kwa mwanamke ambaye ni mke, ama kuhusu akina mama kweli Uislamu ilimtukuza sana mama ikawaamrisha wanawe wamtii na kuomba radhi yake wala wasimkasirishe na kubainisha kuwa ridhaa ya wazazi na hasa mama ni njia mojawapo njia za kupata radhi ya Mwenyezi Mungu na baraka dunaini na malipo mema Akhera; yaani Pepo. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na tumemuusia mwanaadamu awatendee wema wazazi wake wawili. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu,na akamzaa kwa taabu. Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi thalathini. Hata anapofika utu uzima wake, na akafikilia miaka arubaini, husema: Mola wangu Mlezi! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu} [Al-Ahqaf: 15].

Inabainika kutokana na dua hii iliyotajwa katika aya tuliyoitaja kwa wazazi wawili kisha kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu kuitengeneza dhuriya na kuunganisha hii na kumtaja mama peke yake na kumtilia mkazo ni kwa sababu ya kuonyesha kuwa ana nafasi mkubwa mno na taabu anazozipata kuanzia ujauzito kisha kujifungua kisha unyonyaji kisha malezi na anaendelea kuwalea wanawe hata baada ya wafike utu wao mzima. Hayo yanaashiria kuwa Uislamu imemtukuza mama ikikiri fadhila zake na mchango wake ikijikita pia nafasi yake kuwalea wanawe kwa kujibu wa misingi ya malezi mema iliyopitishwa na Uislamu, jambo linalochangia kukiandaa kizazi cha waislamu wanaolazimika kufuata njia iliyonyooka wakishikilia tabia njema kama walivyolelewa na mama zao.

Pamoja na dini ya kiislamu inavyompa mwanamke heshima na hifadhi ya hali ya juu, wapo wanaojaribu kuchafua dini hiyo adhimu kuwa imemnyima mwanamke uhuru wake na kumfanyia dhulma kwa kumpendeleza mwanamume zaidi kuliko kwake. Lakini ukweli ambao uko wazi kwa yeyote mwenye akili na uelewa kwamba Uislamu ulimpa mwanamke uhuru wake na kumfanya mwandamu mwenye huruma na heshima, ilhali alikuwa hana uhuru wa aina yoyote kabla Uislamu haujakuja.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.