Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kufuatia Uamuzi wa kusitisha mapigano mjini Gaza

  • | Wednesday, 27 March, 2024
Taarifa ya Al-Azhar Al-Shareif kufuatia Uamuzi wa kusitisha mapigano mjini Gaza

     Al-Azhar yathamini uamuzi wa Baraza la Usalama kusitisha mapigano mjini Gaza na kusisitiza umuhimu wa kufanya juhudi kubwa zaidi ili kumaliza kabisa jinai za mamlaka ya kizayuni

  • Al-Azhar yatoa shukurani zake kwa mataifa na serikali zilizochukua hatua za kupambana na uadui wa kizayuni na kushinikiza jumuiya ya kimataifa kusitisha mapigano huko Gaza.
  • Kwa hakika mashinikizo ya mataifa mbalimbali yaliklazimisha pande zinazounga mkono mamlaka ya kizayuni kutoendelea katika msaada wake na kuunga mkono wake kwa mamlaka hii ya kikatili.
  • Kujizuia kwa Marekani kupiga kura juu ya uamuzi wa kusitisha mapigano na uadui dhidi ya Gaza ni dalili ya umuhimu wa kushinikiza kwa mataifa na serikali.

 

Al-Azhar Al-Shareif yaeleza ridhaa yake kwa uamuzi uliotolewa na Baraza la Usalama wa Kimataifa unaopitisha kusitisha mapigano na uadui wa kizayuni mjini Gaza katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, ikiomba kuendelea kushinikiza kwa mataifa na serikali kufikia kutekeleza uamuzi huu, na kuzuia uadui wa kizayuni uliopita kiasi na kusababisha kuangamizwa kwa maelfu ya mashahidi wa kipalestina na kuenea kwa njaa pamoja na kufanya mauaji mabaya zaidi kwa wasio na hatia.

 

Al-Azhar inasisitiza kuwa uamuzi huu ulichelewa sana kwa sababu ya ukaidi wa baadhi ya mamlaka na serikali za kimataifa zinazoiunga mkono mamlaka ya kizayuni, lakini kushinikiza kwa serikali na mataifa mbalimbali hasa barani Ulaya na Marekani kulizialzimisha serikali hizo kutoendelea katika hali hii ya kuiunga mkono mamlaka dhalimu na utawala wa kizayuni, hivyo, Al-Azhar inaeleza kuwa inataraji kwamba uamuzi huu uwe hatua kwa kufikia uamuzi wa kumaliza uadui na ukaliaji wa kizayuni katika ardhi za Palestina kwa kudumu, na kujiondoa kabisa kutoka ukanda wa Gaza na kuruhusu misaada ya kibinadamu ifike kwa wapalestina.

 

Pia, Al-Azhar Al-Shareif inathamini sana mchango wa serikali, jumuiya, taasisi na mataifa yanayopenda amani na usalama duniani kwa kufanya juhudi kubwa mno kwa ajili ya kutolea uamuzi kama huu, ikitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuendelea kushinikiza mpaka watawala wa mamlaka ya kizayuni washtakiwa mbele ya mahakama ya jinai za kimataifa kwa jinai na mauaji wa kimbari waliyoyafanya katika uadui huu dhidi ya wapalestina, pamoja na kuungana kwa ajili ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa raia wanaoteseka na njaa na hali mbaya katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Gaza na kuvunja kuzingirwa kwao kupitia vivuko na njia tofauti ili kumaliza njaa inayowatesa wananchi kwa sababu ya uadui huu dhalimu.

 

Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu

Kitengo cha Lugha za Kiafrika

Print
Tags:
Rate this article:
2.0

Please login or register to post comments.