Ramadhani nchini Kongo ya Kidemokrasia

  • | Thursday, 4 April, 2024
Ramadhani nchini Kongo ya Kidemokrasia

 

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Nchi iliyoko Afrika ya Kati, inapakana na Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini kwa upande wa kaskazini, upande wa mashariki: Uganda, Rwanda, Burundi, na Tanzania, upande wa kusini: Zambia na Angola, upande wa magharibi: Jamhuri ya Kongo, na upande wa kusini-magharibi: Bahari ya Atlantiki.

Uislamu ulifika Kongo katika karne ya 19 kupitia wafanyabiashara wa Kiarabu waliokuwa wakitembelea pwani ya Afrika Mashariki, ambapo walifungua njia ya kuenea kwa Uislamu kupitia shughuli zao za kibiashara na uhusiano wao na wakazi wa eneo hilo.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni zinazopatikana: idadi ya Waislamu nchini Kongo ni asilimia 1.3% ya jumla ya wakazi, na ingawa Waislamu ni wachache nchini Kongo, lakini wanaishi maisha yao na kufanya ibada zao kwa uhuru na bila kizuizi au vikwazo, iwe kutoka kwa wasio Waislamu au serikali.

Kwa ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waislamu wote wa  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanalazimika kwa Ibada za Ramadhani, na kukusanyika misikitini kwa ajili ya Swala na kusoma Qur'an, pia wanakusanyika mbele ya misikiti kuanzisha futari ya pamoja, ili hali ya upendo, na umoja itandike. Katika masoko, utawakuta wamiliki wa maduka na mikahawa wakipaza sauti ya Kurani mchana wa Ramadhani.

Moja ya vinywaji vinavyopendwa na Waislamu wa Kongo wakati wa futari ni haibiskasi na tangawizi. Na miongoni mwa milo mikuu ambayo Waislamu wa Kongo hutegemea katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mlo uitwao: “fufu” ambao hutengenezwa kwa unga wa karanga, na “fumbwa” ambao ni mmea maarufu unaofanana na molokhia.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.