Taarifa ya Al-Azhar kuhusu mkutano wa Imamu Mkuu Sheikh wa Al-Azhar na Papa Tawadros II

  • | Tuesday, 2 April, 2024
Taarifa ya Al-Azhar kuhusu mkutano wa Imamu Mkuu Sheikh wa Al-Azhar na Papa Tawadros II

 

Imamu Mkuu Sheikh wa Al-Azhar: Ninasikia huzuni kwa kukaribia Eid Al-Fitr, wakati ndugu zetu wa Gaza wanateseka na uadui wa kizayuni wa kikatili.

Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa/ Ahmad AlTayyeb Sheikhi wa Al-Azhar, amempokea leo Jumatatu katika makao makuu ya Al-Azhar, Papa Tawadros II, Papa wa Alexandria na Patriaki wa Kanisa la kikatholiki, akiwa na ujumbe wa ngazi ya juu wa viongozi wa Kanisa la Kiorthodoksi, ili kupongeza kwa kukaribia kwa Idi ya Al-Fitr, kwa kuhudhuria kwa kundi la wanavyuoni wa Al-Azhar na viongozi wake.

Papa Tawadros alisema: "Ninafurahi kumpongeza Imamu Mkuu na ndugu zetu Waislamu nchini Misri na ulimwengu wote kwa mnasaba wa kukaribia sikukuu ya Idd Al-Fitr, tunajisikia furaha kila tunapokutana, sawa sawa katika makao makuu ya Al-Azhar au katika Kanisa la Kiorthodoksi, mikutano hiyo inahuisha vifungo vya upendo kati ya Waislamu na Wakristo nchini Misri, na ninatumani kuendelea kwa upendo, uhusiano mwema, maendeleo kwa watu wote na Misri yetu tunaoipenda.”

Kwa upande wake, Mheshimiwa Imamu Mkuu alimkaribisha Papa Tawadros II na ujumbe wa ngazi ya juu uliokuja naye katika makao makuu ya Al-Azhar Al-Sharief, na kutangaza: “karibuni sana katika Al-Azhar, na tunazishukuru hisia zenu njema, na tunathamini ziara hii, ambayo inadhihirisha uhusiano wa urafiki unatukusanya.” sisi Wamisri - Waislamu na Wakristo, na inathibitisha undani wa uhusiano wetu na mshikamano wetu katika kitambaa kimoja cha kitaifa, lakini wakati huo huo tunasikia huzuni kuhusu kukaribia kw Eid ya al-Fitr na ndugu zetu huko Gaza bado wanateseka kutokana na uadui wa Kizayuni unaharibu nyanja zote za uhai huko Gaza, kuua watoto, wazee, wanawake, vijana, kuwashambulia wakimbizi, na kubomoa nyumba, hospitali na shule. Kwa kweli, sioni sababu za kinachotokea Gaza, isipokuwa ni kutengwa kwa sauti ya dini, maadili na kanuni za kibinadamu, na kuzipa masikio mbali na sauti ya dhamira ya kibinadamu.

Pia Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar alizungumzia Idara ya Baytul A'aila ya kimisri na nafasi yake katika kuhifadhi muundo wa kijamii wa Misri, aidha alielezea kuwa ni moja ya matunda ya ushirikiano kati ya Al-Azhar na makanisa ya Misri, na kwamba ina jukumu muhimu katika kuondoa fitina na kukabiliana na kuondoa fikra kali na kuzimaliza, na Misri imevuna matunda ya juhudi za nyumba hiyo, na mipango yake mizuri, na fitna na fikra kali zinazotegemea dini ziliegemezwa, akisisitiza mheshimiwa kuhusu ulazima wa kuzidisha ushirikiano wa mradi huo wa kitaifa na kuimarisha jukumu lake la kijamii ili kuwajumuisha vijana, na kuamsha jukumu la wanawake.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.