Dondoo za Hotuba ya Imamu Mkuu katika shereh ya Usiku wa Al-Qadr

  • | Saturday, 6 April, 2024
Dondoo za Hotuba ya Imamu Mkuu katika shereh ya Usiku wa Al-Qadr

Mheshimiwa Imamu Mkuu Profesa; Ahmed Al-Tayeb Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif alishiriki katika mahafali ya Wizara ya Waqfu kwa mnasaba wa Usiku wa Al-Qadr akiambatana na Mheshimiwa Raisi/ Abdul-Fattah Al-Sisi na viongozi wa nchi pamoja na washindi wa mashindano ya kusoma, kuhifadhi na kuelewa Qurani Takatifu, katika mahafali haya, Imamu Mkuu alitoa hotuba nzito, miongoni mwa yaliyokuja katika hotuba hiyo dondoo zifuatazo:
Imamu Mkuu wa Al-Azhar ampongeza Mheshimiwa Raisi Abdul-Fattah Al-Sisi pamoja na wamisri wote na waarabu na waislamu duniani kote kwa mnasaba wa kusherehekea usiku wa Al-Qadr, ule usiku ambapo Qurani Takatifu iliteremshwa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake Mohammed (S.A.W.) ikawa nuru ya kuwaongoza watu na kuwasaidia watoke kutoka giza kwenda nuru na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka.
Imamu Mkuu: "Nawataka wanazuoni wa Umma waanze kwa haraka taharuki ya kutekeleza umoja wa kitaaluma, ambao utakaowaunganisha maulamaa wa Uislamu mioongoni mwa Sunna, Shiia na Waibadhi na wengineo walio ni watu wa Qibla, waungane kwa nyoyo na hisia zao – kabla ya akili na taaluma zao – kwenye meza moja, kwa lengo la kuweka mipaka na ufafanuzi wa kuainisha yanayopaswa kupitishwa kwa pamoja na yale yanayoweza kuwa na hitilafu, na kuongoka kwa adabu ya maswahaba (R.A.) na Tabiina ile hitilafu iliyochangia kukuza na kuimarisha taaluma za kiislamu na kuzigeuza kuwa vyanzo visivyo na mwisho vya elimu wakiwa na upole na huruma, na kufunga mlango na kukata njia ya kuchocheza hitilafu zetu za kisasa ambazo zilitusababishia mizozo, migogoro, chuki, bughudha nyingi na kutupelekea kwa maadui kama ni mawindo mwepesi”
Imamu Mkuu aeleza kutoridhika kwake kwa kugeuka kwa mahusiano ya umma na staarabu mbalimbali yawe migogoro, vita na mizozo badala ya kuwa mahusiano ya mazungumzo na ushirikiano.
Imamu Mkuu: "Majeshi ya kizayuni wanatumia silaha za kuangamiza halaika kuwalenga raia wasio na hatia wala silaha wala uzoefu wa kupigania vita”
Imamu Mkuu: Afafanua yanayoendelea kutukia huko Gaza kuwa ni jinai ya mauaji ya kimbari zinazofanywa na mamlaka ya kizayni dhidi ya raia wasio na silaha wala hatia yoyote.
Imamu Mkuu: "Jumuiya, taasisi na mashirika ya kimataifa yakawa hayana uwezo wa kubadilisha hali mbaya iliyopo Gaza yakawa kama aliyepatwa na ulemavu wa viungo vyake vyote akawa hana uwezo wa kufanya lolote"
Imamu Mkuu: “Historia itaweka kumbukumbu mateso na maangamizi yanayofanywa kwa wapalestina katika kurasa za kuthibitisha dhuluma na uadui usio na mfano kamwe”

Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.