Uislamu wakataa Vurugu na Ukabila .. Waheshimu kujiunga kwa jamii fulani

Imeandaliwa na Dkt.; Alaa Salah Abdulwahed

  • | Thursday, 18 April, 2024
Uislamu wakataa Vurugu na Ukabila .. Waheshimu kujiunga kwa jamii fulani

 

      Kwa kweli vurugu, upendeleo na ukabila kwa sura zao zote za kibaguzi au kitaifa au kifikra zinaathiri vibaya na husababisha hatari mkubwa kwa mahusiano yaliyopo baina ya wanajamii na kudhuru hali ya kuishi pamoja kwa amnai baina ya wanajamii hao, kwa kupelekea maangamizi, ugaidi na uharibufu mkubwa. Huenda sura iliyo hatari zidi kuliko kati ya sura za vurugu na ukabila ni ule ukabila wa kitaifa na kidini, ambapo makundi kadhaa wanaifanya na kufuata ukabila na vurugu ya aina hii na kuwachocheza wengine kuifuata kinyume na iliyokuja nayo sheria za mbinguni kuhusu jambo hilo na hasa sheria ya kiislamu, na pia kinyume na maadili ya kibinadamu yanayojengeka upendo na amani. Kwa kweli vurugu na ukabila ni kama moto unaoweza kuharibu na kupasua mahusiano ya kijamii na kuua roho ya kuishi pamoja kwa amani na kueneza unafiki na usambaratisho na kuelekeza nguvu kwenye mizozo na migogoro badala ya maendeleo na ustawi wa jamii na ustaarabu.

Kwa hiyo, ukabila wa kidini ni mojawapo aina hatari zaidi za ukabila katika historia nzima ya kibinadamu, kwani unahusiana na mwingine, fikra zake na imani yake, maana unategemea kutangaza pande za kuhitilafiana na kutofautiana kiitikadi baina ya makundi ya waumini wa dini mbalimbali na madhehebu tafauti za dini moja. Ukabila ulikuwa umeenea sana katika lugha ya Kiarabu, na hasa hasa baada ya ujio wa Uislamu ambao umeangalia maana yake kama ni kuzozana, kusambaratika na kujivunia nasaba, ilhali dini yenyewe inahimiza umoja, undugu na kuhurumiana, ambapo Mwenyezi Mungu (S.W.) Ameziunganisha nyoyo za waja wake waumini kwa kushikimana Uislamu Akawafanya umma mmoja, na kufanya msingi wa kupendelea mmoja bila ya mwingine ndiyo ucha Mungu na matendo mema, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: "Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungeli toavyote viliomo duniani usingeli weza kuziunga nyoyozao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima" Al-Anfaal: 63.

Naye Mtume (S.A.W.) alikuwa kuanzia ujumbe wake akifuata njia ya kuwaunganisha watu na kuipgania vita ukabila na vurugu, ambapo alikuwa anasisitiza daima kwa maneno na vitendo kwamba Uislamu hautambui ukabila wala ubaguzi, kwa hivyo alisistiza katika hadithi yake: "Enyi watu! Kwa kweli Mola wenu Mlezi ni mmoja, na baba yenu ni mmoja, kwa hiyo haijuzu wala haikubaliki kumpendelea mwislamu (mtu) zaidi kuliko mwingine kama vile; kumpendelea mwarabu kuliko mwajami wala kinyume cha hayo, au kumpendelea mweupe kuliko mweusi wala kinyume chake, isipokuwa kwa kigezo kimoja tu ambacho ni Ucha Mumngu" hivyo tunaelewa kuwa Mtume (S.A.W.) alibainisha katika hadithi hii kuwa msingi unaozingatiwa kutafautisha baina ya watu na kuwapa vyeo mbalimbali na kupendeleza baadhi zaidi kuliko wengine ni msingi mmoja tu ambao ni Ucha Mungu, sio kabila wala rangi wala chochote kingine. Kwa hivyo, Mtume alifanya usawa baina ya watu na kuondoa ukabila na ubaguzi ni ukweli thabiti katika hali halisi ya jamii ya kiislamu, akampa Bilal bin Rabah ambaye ni mtumwa mweusi aliyetoka uhabashi maana si mwarabu wala mweupe wala bwana, akampa kazi ya kutangaza adhana na kusimama juu ya Kaa'ba na kuwaita waislamu wanaotoka makabila mbalimbali na koo tafauti waje wakae wamsikilize na kuradidi adhana nyuma yake, bila ya kusikia ghadhabu wala chuki kwa kufanya hivyo, kwani wameamini na kufuata amri yake Mwenyezi Mungu (S.W.): "Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina yandugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe" Al-Hujuraat: 10. Wakati huo huo Mtume (S.A.W.) alikuwa anawafundisha kwamba Mwenyezi Mungu (S.W.) Anazingatia vitendo siyo nasaba aliposema Mtume: "Kwa hakika, yeyote ambaye hakufunikiwa duniani kupata thawabu na maghufira kwa vitendo vyema, hatanufaika kwa nasaba yake hata kidogo".

Hivyo, Bilal kwa kipimo cha Uislamu, ni bora kuliko wengi wa mabwana wa Qureish, kwani yeye aliwatangulia kujiunga Uislamu na kumwamini Mtume (S.A.W.) na cheo alichopewa Bilal katika Uislamu kinatokana na aliyoyafanya kuinusuru dini hiyo na uvumilivu wake kwa mateso makubwa sana kwa sababu ya imani yake. Kutokana na hayo waislamu wakawa wanaamini kuwa wote ni ndugu mbele ya Mwenyezi Mungu (S.W.) na kwamba kigezo cha pekee cha kuwapendeleza baadhi kuliko wengine ni Ucha Mungu siyo kwa kutegemea nasaba wala ukoo wala kabila wala rangi wala utajiri wala madaraka. Inatajwa kuwa Mtume (S.A.W.) ametoka kabila la Qureish na alikuwa anaelewa sifa hasa walizopewa maqureish ambapo mahujaji wote walikuwa wanasimama Arafa lakini maqureish wanasimama Muzdalifah, na mahujaji hawa hawana budi kununua mavazi ya Hijja kutoka maqureish ili kutekeleza ibada ya Tawaf, wasingalifanya hivyo wasingalipata mavazi ya kujisitri wakati wa ibada hiyo, baada ya kuja kwa Uislamu sifa hizo hasa za kuwapendeleza maqureish kuliko makabila mengine zilikataliwa na makabila yote yakawa sawa sawa kwani Kaa'ba ndyio Nyumba Mtukufu ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo watu wote wana sifa sawa na haki sawa wakielekea Nyumba hiyo kuomba rehma na maghufirah ya Mwenyezi Mungu, basi wote wakawa wanatakiwa kusimama Arafa kwa ajili ya kuondoa upendeleo uliokuwepo zama za kabla ya ujio wa Uislamu, waja wote wakawa sawa bila kumbagua yeyote bwana au mtumwa, mtajiri au maskini, mweusi au mweupe.

Ikaja aya Takatifu kuwaagiza maqureish wafanye kama wanavyofanya watu wengine: "Kisha miminikeni kutoka pale wanapo miminikawatu, na muombeni Mwenyezi Mungu msamaha: hakikaMwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu" Al-Baqarah: 199. Kwa hiyo, Uislamu umebainisha kuwa hakuna upendeleo wowote katika ibada kwa kabila kuliko jingine, jambo linalohimiza kuenea msingi wa usawa baina ya watu wote kwani wote ni waja wa Mwenyezi Mungu, wote wanamwabudu peke yake, ikawa bora kuwa sawa sawa bila ya tafauti hata chembe. Pia, Mtume (S.A.W.) alikuwa anawaelekeza waislamu na kuwatanabahisha kuepukana na kujigamba kwa nasaba akisema: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu (S.W.) Amekufuteni desturi mbaya ya kijahahili na kujivunia kwa nasaba, basi mtu ama muumini mcha Mungu au fasiki muovu, nyote ni wana wa Adam na Adam ameumbwa kutokana na udongo, wale wanaojivunia ukoo zao waachane na hayo, huenda watakuwa mkaa wa moto au Mwenyezi Mungu Awaangamize kwa urahisi sana", hali hiyo hiyo kuhusu ukabila na vurugu kwa taifa, ambapo pia waislamu wanakatazwa kujivunia taifa lao, kwa kuwa jambo hilo husababisha uadui na chuki baina ya watu, Mtume (S.A.W.) amesema: "Yeyote anaepigania taifa au ukoo pasipo na haki, akichochea ukabila na vurugu, basi yuko jahiliyya akifa akiwa na hali hii".

Kwa hiyo, haiambatani na imani kuwa mtu apendeleze kaumu wake akiwasaidia kuwadhulumu wengine, lakini wakati huo huo hayo hayamaanishi kuwa Uislamu unapinga au kumzuia mtu atetee taifa lake, ukoo wake na kaumu wake na kusikia fahari nasaba na kabila, bali hayo yanamaanisha kuwa upendo wake na fahari yake isiwe bila ya kutafakuri na kuliwaza kutambua haki kwa kuwasidia jamaa zake kuwadhulumu wanyonge. Hivyo Maswahaba (R.A.) walimfuata Mtume (S.A.W.) katika msimamo wake kuhusu ukabila na vurugu wakitambua kwamba hawatakiwi kusaidia kueneza chuki baina ya makabila na koo mbali mbali, bali kueneza ushirikiano na mashikamano kwa ajili ya kuimarisha nchi na kuleta ustawi na maendeleo katika jamii na kuishi pamoja kwa amani na utulivu, ambapo siyo katika vurugu awe mtu anapenda kaumu wake, lakini vurugu na ukabila wa kweli ni kuwasidia kaumu wake hao kufanya dhuluma, na Uislamu kama ulivyopinga ukabila wa kitaifa unaochukizwa, vile vile ulikataa ukabila na vurugu ya kidini kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): "Hapana kulazimisha katika Dini" Al-Baqarah: 256.                      

       

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.