Wanadai .. Tunasahihisha

18

  • | Thursday, 23 June, 2016

Hakimiya (Utawala) ni istilahi mpya ambayo imetumika kwa mara ya kwanza na “Abul Aala Al-Maududi katika juhudi za  kupata uhuru kutoka ukoloni wa Uingereza, kisha Pakistan ilipopata uhuru na kutengwa mwaka 1947, yule Al-Maududi ameacha mawazo yake kuhusu Hakimiya akakubali kutawaliwa kwa mujibu wa sheria za nchi na katiba yake bali akajigombea katika uchaguzi.
Sayed Kotb amelitetea wazo lile lile kwa kuitumia vibaya istilahi hiyo na kuielekeza kwenye mawazo yake ya uharibifu akasema kuwa Misri ni nchi isiyo na maendeleo yo yote bali inabaki katika dhuluma za ukafiri kwani inaendesha mambo yake kinyume na Aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu.  
Kwa hakika makundi ya kigaidi tangu enzi ya Sayed Kotb hadi siku hizi za kisasa yanaitumia istilahi hiyo kwa ajili ya kuhalalisha upotofu wake na kujiweka mbali na njia iliyonyooka basi wakawaua wasio na hatia, wakaziharibu staarabu wakidai kuwa hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu pekee, na kwamba ni lazima kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu katika ardhi.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.