Wanadai .. Tunasahihisha

19

  • | Friday, 24 June, 2016

Wazo hili ni kosa kwa dalili ya kuwa Mtume (S.A.W.) amewapa Maswahaba wake haki ya kujitihadi katika enzi maalum katika mazingira, mahusiano, na matukio maalum, wala hakuwakataza kujitahidi na kubuni masuluhisho ya kuyatatua katika kuyatatua matatizo kwa kutegemea msingi wa hakuna Mtawala isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee.
Ikiwa hii ni hali ya Mtume (S.A.W.) na maswahaba wake japokuwa waliishi katika enzi maalum, mahali maalum, mazingira maalum, basi hali yetu inatulazimisha kujitahidi zaidi na kujaribu kufikia ufumbuzi mbali mbli ili kuyatatua matatizo mengi yanayotukumba, na eneo la nchi za kiislamu  likawa pana mno na tumefika karne ishirini na moja ambapo matatizo yameongezeka sana.
Kwa kweli suala la Hakimiya pamoja na matatizo yaliyosababishwa nalo, ambapo limesaidia kuzuka matatizo na migogoro kati ya makundi kama vile Khawarij, Mashia na wakafirishaji wakali wa enzi yetu hiyo waliokosa kufahamu suala hilo, likatumiwa kinyume cha makusudi yake likageuka kutoka “Hakimiya ya Mwenyezi Mungu“ likawa “Hakimiya ya makundi na madhehebu” ambayo yamejifanya naibu ya Mwenyezi Mungu, jambo lililosababisha umwagaji mwingi wa damu na kuzuka fitina.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.