Wanadai .. Tunasahihisha

20

  • | Saturday, 25 June, 2016

Hakuna mtu ye yote anaye haki ya kutawala mambo ya kidini na kuyadhibiti masuala ya kiroho ya mwingine, bali kinyume dini inategemea kushauriana na kuusiana, na kila tunavyoweza kufanya na mtu mwenye kufanya uhalifu ni kumwusia kwa upole na sio hadharani, ambapo akitubu basi itakuwa nzuri zaidi, ama akikataa akaendelea madhambi basi tutakuwa tumeshafanya wajibu zetu kuhusu kumpa shauri na nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (S.W.).
Vile vile mwanadamu huweza kuwa dhaifu na amepatwa na msiba ya kufanya madhambi na hatia, lakini moyo wake ndio safi na hauna shari lo lote umejaa imani kwa Mwenyezi Mungu, kwa hiyo tunakuta katika hadithi tukufu kwamba Mtume (S.A.W.) amesemas: "hakika Mwenyezi Mungu hatazamii sura zenu na mali zenu, bali hutazamia mioyo yenu na kazi zenu" na miongoni mwa semi za kiislamu zinazoashiria maana hiyo yanayosemwa na wanavyuoni wa Al-Azhar wanaposema: "hakika moyo na pahali pa kutazamiwa kutoka Mwenyezi Mungu" basi fanyeni juhudi zenu zote za kusafisha mioyo zenu wenyewe za watu sio kuwakafirisha watu kwa kudai kupitisha hukumu za sheria ya Mwenyezi Mungu.
La maana kuwakumbusha wote kwamba yaliyo halali ni dhahiri na yaliyo haramu ni dhahiri na kwamba kuwakafirisha wingine kwa kutegemea kisingizio cho chote haijuzu kabisa na tukikubali hayo, basi hatutayakubali kutoka makundi yaliyokosea kuongoka kifikira na kiroho.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.