Sikiliza na Zungumza..Jukwaa la vijana kwa ulezi wa Al-Azhar Al-Shareif

  • | Saturday, 4 May, 2024
Sikiliza na Zungumza..Jukwaa la vijana kwa ulezi wa Al-Azhar Al-Shareif

 

Jumatano ijayo..Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu chaandaa toleo la tatu la kongamano la Sikiliza na Zungumza (Listen and Talk) kwa vijana wa vyuo vikuu

Kwa mujibu wa mkakati wake wa kiutendaji, Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu siku ya jumatano ijayo terehe nane mwezi wa tano mwaka huu kitaandaa toleo la tatu la kongamano la Sikiliza na Zungumza kwenye Kituo cha Al-Azhar cha Mikutano mjini Kairo, kongamano hilo ambalo toleo lake la kwanza lilifanyika mwaka 2018 linalenga kuimarisha maadili ya mazungumzo, kuheshimu maoni tofauti na kubadilishana mawazo kati ya vijana wa vyuo vikuu, pamoja na kuanzisha njia bora za kuwasiliana nao kwa ajili ya kusikiliza maoni yao na kutambua matarajio yao kwa nchi na mustakbali yao, pia, kusikiliza na kujibu maswali yao yanayohusiana na masuala mbali mbali ya kidini, kijamii au masuala mengineyo hasa yale maswali yaliyotokana na maendeleo ya kisasa ya kiteknolojia kama vile; programu za ubunifu (AI) ambazo zilisababisha kujitokeza changamoto nyingi kwa asasi za nchi na mashirika yake mbali mbali pamoja na watu wanaoishi katika jamii kwa viwango vyake tofauti.

Toleo hili la kongamano la Sikiliza na Zungumza linakusanya vikao viwili; ambapo kikao cha kwanza kinabeba anuani: "Hisia na uhusiano wake kwa Fikra Potofu" watoa mada katika kikao hicho ni: Dkt. Muhab Mujahid, Mtaalamu wa tiba ya kisaikolojia, na Dkt. Osama Raslan, Msimamizi wa Kitengo cha Lugha ya Kiingereza katika Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu, kikako kitaendeshwa na Bw. Mohammed Abouda, Mtafiti katika Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu.

Ama kikao cha pili cha kongamano hilo kitajadili maudhui ya: "Utambulisho katika zama ya Ubunifu" ambapo watoaji mada ni pamoja na Sheikh: Yousry Azzam, Imamu na mwalimu katika wizara ya Waqfu ya Misri, na Mhandisi: Anthony Michael, Mkuu wa Tume ya Teknolojia inayofuata Baraza la Taifa la Ufundi na Elimu, kikao hicho kitaendeshwa na Mwandishi wa Habari Bw. Ahmed Al-Driny.

Inakumbukwa kuwa toleo hili la kongamano la Sikiliza na Zungumza linakuja baada ya kufanikiwa kwa toleo mbili za kwanza na pili kuwakusanya vijana wa vyuo vikuu vya kimisri pamoja na wataalamu na wadau mbali mbali kwa lengo la kubadilishana mawazo na kutambua masuala yanayowahusu vijana na hasa masuala yanayohusiana na fikra zinazotumiwa vibaya na makundi ya kigaidi kuwalaghai vijana na kuwashawishi kujiunga na makundi haya kwa kutumia hamasa za hisia za vijana hawa na kujaribu kuwageuza wawe sababu za kuharibu nchi na kupoteza amani ya kijamii.

Kwa hivyo, mada za toleo la tatu limetokana na mapemdekezo ya toleo la kwanza na la pili, ambapo Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu kilitia maanani kutekeleza mapemdekezo haya hasa tukitambua umuhimu wa kuzingatia hisia na mchango wake katika kumwelekeza mtu na vitendo vyake viwe heri au shari na kuangalia vema pande za  hisia na kisaikolojia kwa vijana, hasa katika za ubunifu wa kiviwanda na programu za kisasa za AI  na mitandao ya kijamii inayojaa fikra zisizoambatana na dini wala maadili ya kibinadamu na tabia njema, jambo linaloweza kuwapelekea kufanya vitendo vibaya, kwa hiyo Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu kinalenga katika toleo hili kujadili maudhui za Hisia na Utambulisho kwa namna isiyo ya kawaida, bali kwa namna inayowafaa vijana zaidi kuliko njia za kawaida kwa ajili ya kupata matokeo yenye faida kubwa zaidi yanayokubalika na wengi wa hadhira lengwa na yanayoweza kutekelezwa kikweli.

 

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Potofu

Kitengo cha Lugha za Kiafrika

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.