Wanadai .. Tunasahihisha

21

  • | Sunday, 26 June, 2016

Kwa kweli tukirudia misingi ya dini yetu tutatambua kwamba Mtume (S.A.W.) amesema akielezea upendo wake kwa Makkah nchi yake ambapo amefukuzwa nje yake na watu wake akalazimishwa kwenda Medinah: "Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu utufanye tuupenda Medinah, kama tulivyopenda Makkah au zaidi….". kwa hiyo Mtume (S.A.W.) aliupenda Makkah ambayo ni nchi yake kwa kiwango cha juu sana, basi madaesha hawa wadaije kwamba kuipenda nchi na kujiunga nayo ni ukafiri wakipuuza hadithi hii ambayo japokuwa ni hadithi sahihi na wanaijua vizuri lakini wamekusudia kuipuuza kama vile wanapuuza hukumu zote za dini hiyo iliyochafushwa nao?!
Pia tunapaswa kufanya kama alivyofanya Mtume (S.A.W.) kwa mujibu wa aliyoyasimulia Imamu Ahmad katika kitabu chake cha Musnad kutoka kwa Faseilah kwamba alisema: nimemsikia babngu akisema: nilimwuliza Mtume (S.A.W.) nikisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je ni ukabila kwamba mtu kuwapenda watu wake hasa? Akasema Mtume (S.A.W.): hapana, lakini ni ukabila kuwamba mtu kuwanusuru watu na jamaa zake hata wakiwa madhalimu" basi mtu kuipenda nchi yake na wananchi wenzake si kitu kibaya, bali ni jambo zuri isipokuwa likapelekea kumsaidia mdhalimu hata akiwa ni miongoni mwa watu wetu.    

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.