Mapendekezo ya Kongamano la Sikiliza Uzungumze

Toleo la tatu Mei 8, 2024

  • | Wednesday, 8 May, 2024
Mapendekezo ya Kongamano la Sikiliza Uzungumze

 

     Kulingana na maoni na mawazo yaliyosemwa katika vikao viwili vya toleo la tatu la kongamano la "Sikiliza na Zungumza", sawa sawa yakiwa kutoka vijana walioshiriki au wataalamu, tunayo furaha ya kutangaza idadi ya mapendekezo yanayotokana na michango hiyo:

  • Kituo cha Al-Azhar kinasisitiza azma yake ya kuwasiliana kwa uwazi na vijana wenye umri mbalimbali, na kufungua njia za mazungumzo nao ili kujua kwa ukaribu kile kinachowahusu vijana hao; hasa kwa kuzingatia changamoto hatari za kisasa, kama kuamiliana na maudhui ya kidini yanayosambazwa na wasio wataalamu; kwa hiyo, hatutaacha wajibu wetu katika kuwasiliana na vijana wa nchi yetu ili kuhifadhi misingi ya kidini na kujadili mawazo yote bila ya mipaka, kwani mawazo yote yenye nia njema ni mada ya majadiliano na utafiti baina yetu.
  • Hisia za kibinadamu ni miongoni mwa pande vipengele bora zaidi ambavyo Allah Aliumba watu navyo, kwani kuwazingtia watu na kubadilishana mapenzi nao ni mojawapo ya mahusiano ya juu zaidi duniani, lakini tumekuta kwamba kipengele hicho kwa mujibu wa tafiti zetu labda kuwasukuma vijana na wasichana wanaangukia kwenye makundi ya kigaidi au uhalifu wa kijamii chini ya majina ya kuvutia, jambo ambalo linalosababisha kuziba mianya yote ambayo makundi ya kigaidi yanaweza kuingia kutoka kwake ili kuendesha hisia za vijana na kuwavutia kwenye safu zao kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi ya kihalifu na kujilipua.
  • Kuzingatia utunzaji wa kinga na chanjo ya mapema kwa watoto na vijana katika hatua mbali mbali za elimu, ili kuingiza maadili ya kidini na kitamaduni na maoni ambayo yanawazuia kufuata fikra kali, na hapa  jukumu la wazazi - hasa mama - lazima kuongeza katika kujua mvuto wa nje unaozunguka hisia za watoto, pamoja na kujua njia sahihi na mbinu za kukabiliana na mvuto mbay katika hisia zao ili kuwazuia kufikiri kujiua au kukana ALLAH.
  • Hali ya kisaikolojia ni kichocheo kikuu katika maisha ya vijana, na katika wakati wa changamoto za kisasa, kukimbilia kwa wataalamu kama madaktari wa akili ili kujua njia sahihi za kukabiliana na shinikizo na hisia mbaya sio anasa kama wengine wanavyofikiria, lakini ni njia ya kuendesha hisia na kuwaelekeza kwenye njia zinazohifadhi maisha yao na kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kuzishinda mashinikizo hayo
  • Habari zilizopokelewa kuhusu halifu zinazofanywa kwa kutumia kile kinachojulikana kama "Mtandao wa Giza" na mbinu zingine za kiteknolojia zinazohusiana na akili bandia, zimeweka changamoto nyingi kwa taasisi za kiserikali, na kutokana na jukumu letu katika kituo cha Al-Azhar cha kilupambana na fikra kali basi tumeanza kutekeleza mfululizo wa warsha zinazoshughulikia matukio mabay ya Intaneti, na warsha hiyo zitaendelea wakati ijayo kwa kushirikiana na wataalamu katikati njia ya usalama wa Intaneti na maelezo ili kubainisha matatizo yanayohusu teknolojia hizo.
  • Hakika njia ya kukabiliana na changamoto zozote ni kujifunza na kukuza fikra makini kwenye vijana wa umri mbalimbali kwa namna ambayo inawazuia kupokea mawazo bila  kufahamu madhara yake, kwani  kutumia akili na kuchunguza mawazo kufuatilia yale yenye manufaa na kukataa yenye madhara ni jambo lisiloweza kudharauliwa; hasa kwa kuongezeka kwa vitisho vinavyotokana na kila kinachohusiana na Intaneti na tuhuma zinazoibua.
  • Sio siri kwamba teknolojia, katika baadhi ya vipindi vyake vya kihistoria, imesukuma ubinadamu kwenye shimo, ambapo makumi ya mamilioni ya watu wameuawa, na mashine ya mauaji bado zinaendelea katika Gaza na kwamba ujumbe wetu ni kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kwamba maendeleo ya kiteknolojia yanaletea manufaa kwa ubinadamu na kufikia usalama, uthabiti, na huduma kwa ubinadamu - na sio kuwa chombo cha mauaji, hujuma na uvamizi - kama tulivyoona na tunavyoona
  • Kituo cha Al-Azhar kinapendekeza kuimarisha ufahamu wa kidijitali unaohusu kudhibiti wakati, kulinda faragha, na kuanzishwa kwa uhusiano mzuri na wa kweli kati ya wanafamilia, na kudhibiti maudhui ya kidijitali yanayotolewa kwa watoto, na tunaashiria hapa kwamba kuna teknolojia na taratibu zinazowezesha familia kufikia hilo; kwa hivyo, tunawatakia baba na mama ili kutekeleza kauli ya Mtume wa ALLAH (S.A W): “Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu atahesabiwa kwa anachokichunga”- ili kuwalinda watoto wao kutokana na athari mbaya iliyoachwa na intaneti na mawazo yake yasiyo sahihi yanayoathiri misingi ya kidini na utambulisho wa kitamaduni na kifikra kwa jamii ya kimisri, na zinazowasukuma watoto hao kwa kuanguka kwa kibinadamu, ambayo yataathiri nchi na utulivu wake.

 

Dkt. Reham Abdallah Salama

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.