Mwenyezi Mungu (S.W.) Amemchagua Mtume wetu Mohammed (S.A.W.) awe mtume wa mwisho ambaye ni shahidi, mbashiri, mwonyaji na mlinganiaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa idhini yake na kwa mujibu wa mongozo wake (S.W.). Naye Mtume ametimiza majukumu yake ipasavyo akatoa wito na kufikisha ujumbe kwa watu akifungua milango ya ulimwengu kote kwa ujumbe wa Uislamu.
Watu wakaanza kujiunga na dini ya kiislamu makundi makundi kwa kuwa Mwenyezi Mungu Akarahasisha njia za kuenea kwa dini yake katika kila kona duniani. Vizazi vya walinganiaji wa dini hiyo vilifuatana na kusambaa ulimwenguni kote, pamoja na walimu na mashekhi wa vyuoni wanaofundisha taaluma mbalimbali za kidini na zisizo za kidini. Kwa hakika waislamu wamechangia kwa kiasi kikubwa katika ustaarabu uliosaidia kukuza jamii mbalimbali zilizopokea na kutawaliwa na waislamu.
Mifano iko mingi ya wanavyuoni na wataalamu katika nyanja mbalimbali na sayansi tofauti wakiwa wanawajibika mtindo wa Uislamu wa ukati na kati na fikra za wastani. Wataalamu hawa ndio waliotajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili * Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Huku viumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto} Al-Imran: 190-191.
Vile vile, miongoni mwa athari za kiustaarabu za waislamu kuanzishwa kwa Vyuo na Vyuo Vikuu kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa kiislamu kabla havijaanzishwa barani Ulaya kwa karne mbili, ambapo Chuo Kikuu cha kwanza kuanzishwa ni Chuo Kikuu cha Zaytouna nchini Tunisia mwaka 737 B.K. halafu Beitul-Hikma nchini Iraq mwaka 830 B.K., kisha Chuo Kikuu cha Qaraweein kilichoanzishwa mwaka 859 B.K. mjini Fas nchini Morrocco kisha Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilichoanzishwa mwaka 970 B.K. mjini Kairo, nchini Misri.
Wakati huo huo, Chuo Kikuu cha kwanza kuanzishwa barani Ulaya kimeanzishwa mwaka 1090 B.K. mjini Sicilia, kisha Chuo Kikuu cha Padoffa nchini Italy kilichoanzishwa mwaka 1222 B.K. kwa kutegemea vitabu na mitalaa ya waarabu. Pia, vyuo vya masomo ya kiislamu vilikuwa vinafuata mfumo maalumu uliofanana na waliokuwa wakifuata waislamu.
Katika kila enzi tunashuhudia kwamba kuna mvutano baina ya mafunzo ya kimapokeo na mafunzo ya kisasa, mapokeo na usasa ni maneno yanayosikika sana siku hizi, mapokeo yanamaanisha kufuata mafundisho ya kijadi kwa kutegemea misingi ya kisheria kwa dalili na nguzo thabiti na kushikamana na mafunzo haya ama usasa unamaanisha kutumia mbinu mwafaka wa wakati na enzi ya kisasa kwa mujibu wa mahitaji yake na hali ya walinganiwa.
Kwa hiyo, tunaona kwamba wito wa kiislamu ilikusanya mbinu mbili ya kijadi inayoshikamana matini na dalili za Qurani na Sunna wakati ambapo mbinu ya kisasa inayotumia zaidi hoja za kiakili na mantiki ilitumika pia katika mazingira maalumu kufuatana na hali ya watu.
Kwa hivyo, tunaelewa kuwa Uislamu unatumia mbinu zote mbili kwa kiasi tofauti kulingana na hali ya watu wanaolinganiwa. Hata hivyo, mlango wa maendeleo na uboreshaji uko wazi kwa mujibu wa vigezo na masharti na pia mahitaji ya uboreshaji na maendeleo.
Uislamu kwa mujibu wa maumbile yake ni dini inayoafikiana na sunna za maisha isiyopingana na maumbile ya Kibinadamu hata kidogo, kwa hiyo, Uislamu ndiyo dini inayohimiza sana kuleta maendeleo ya mara kwa mara kwa hali ya mambo na jamii kwa ajili ya kufika kiwango cha juu kabisa na kuwa na hali bora zaidi katika pande mbali mbali za maisha. Mtume (S.A.W.) ameelezea dhana ya uboreshaji katika sheria ya Kiislamu, aliposema katika hadithi takatifu: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu Anawatumia ummah huu mwanzoni mwa kila karne, mmoja wao anaye elimu ya Kuendeleza na kufufua mafundisho ya dini yao". Na kwa kuwa Uislamu ni dini ambayo mafundisho yake yanafaa maisha yote, basi uboreshaji unaokusudiwa katika hadithi hii ya Mtume (S.A.W.) ni ule ule uboreshaji wa maisha katika nyanja zake tafauti. Na uboreshaji tunaolenga sio jambo la kiholela, wala haliwi bila ya misingi na vidhibiti maalumu, bali ni uboreshaji unaotegemea uelewa na kutambua hali halisi ya mambo kwa ajili ya kugundua na kubainisha mabaya yake, hivyo kurekebisha hali ilivyo na kuandaa mabadiliko mapya yenye kuleta uboreshaji na kuendeleza maisha kwa kutegemea masuluhisho yaliyobuniwa kwa lengo la kugeuza maisha ya wanadamu iwe bora katika nyanja zake mbalimbali, jambo ambalo huchangia sana kuboresha hali yao kidini na kidunia.
Kwa kuwa dini ni nguzo ya maisha kikamilifu, basi kazi ya Fiqhi inahusiana na kukidhi mahitaji yote ya maisha hayo, na kwenda bega kwa bega na mabadiliko ya maisha, na madamu masuala ya kifiqhi hayana hukumu thabiti; maana yanakubali kubadilika kutokana na mabadiliko ya hali, yale mabadiliko ambayo ni jambo la kawaida kwa mujibu wa jitihada inayotakika katika mambo yanayoruhusiwa kufanyiwa jitihada katika Uislamu kwa lengo la kuwarahisishia watu mambo ya dini yao na kuondoa mashaka, pamoja na yale masuala mapya ambayo maulamaa wa sheria (Fiqhi) ya kiislamu hawakuyajua wala hawakutoa ufafanuzi wake, hivyo jitihada ikawa jambo linalotakiwa ili kupata hukumu ya kisheria inayofaa, kama vile; suala la kunukuu viungo vya mwanadamu kutoka mtu kwa mwingine, upachizaji, mtoto wa maabara na masuala mengine mengi ya matendeano ya kifedha ya kisasa, na kadhalika, hasa baada ya uzinduzi wa teknolojia ya kisasa ya maelezo ya kilektroniki na mawasiliano, na kuenea utumiaji wa intaneti kwa upana zaidi na zaidi, na kuhitilafiana kuhusu usahihi wa kutumia mbinu hizo kupitisha ndoa au talaka au wasia na matendeano mengineyo.
Kwa kweli zama ya kisasa ina mabadiliko makubwa yenye umuhimu kwa maisha ya binadamu, kwa hiyo sheria ya kiislamu (Fiqhi) inabidi kuwenda sambamba na mabadiliko na maendeleo haya kwa kutoa hukumu za kisheria zinazomsaidia mwislamu aafikiane na zama anapoishi, wala hawi mbali na mabadiliko haya. Kwa hivyo, wito wa kuangalia upya baadhi ya masuala na hukumu za kifiqhi siyo kazi mbaya wala hakumaanishi kutoka nje ya misingi na mafundisho ya dini au kukana hukumu zake, bali hali hiyo inamaanisha kuangalia upya hukumu na maelezo ya kifiqhi yaliyotufikia kizazi baada ya kizazi kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine inamaanisha kutafuta masuluhisho ya kiislamu kwa masula mapya yanayojitokeza katika jamii. Kwani kuna masuala mengi yanayohusiana na maisha ya waislamu ambayo yanahitaji kuangaliwa kwa mtazamo wa kisasa na kupangwa upya, jambo linalobidi kuzingatiwa sana na hasa kwa kuzindua na kuongeza tanzu mpya za Fiqhi kama vile, Fiqhi ya kisasa (hali halisi ya kisasa), Fiqhi ya masuala yaliyo muhimu zaidi na Fiqhi ya waislamu walio wachache. Hayo yote yanatubidi kufanya jitihada zaidi na zaidi zinazoambatana na zama na pahalaa, tukiwa na uelewa, wepesi na ufahamu kwa hali halisi ya mambo.