Al-Azhar Al-Shareif yakaribisha nia ya Misri kuingilia ili kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Mamlaka ya Kizayuni

  • | Monday, 13 May, 2024
Al-Azhar Al-Shareif yakaribisha nia ya Misri kuingilia ili kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Mamlaka ya Kizayuni

     Al-Azhar Al-Shareif inakaribisha hatua iliyotangazwa na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kuhusu nia yake ya kuingilia ili kuunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Mamlaka ya Kizayuni katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu, ikisisitiza uungaji mkono wake kamili kwa uongozi wa kisiasa katika mpango huu ambao unalingana na nafasi ya Misri na historia yake ndefu na yenye heshima ndani ya mfumo wa kuunga mkono kesi ya Palestina na kuondosha fisadi ya madhalimu na maadui, na kunyanyua nafasi ya raia ya Misri katika kuunga mkono kwa kusimama kidete kwa ndugu wao katika Ukanda wa Gaza.

Al-Azhar inatoa wito kwa kila mtu kutumia viwango vya juu vya mashinikizo ya kisiasa, kimataifa na ya wananchi ili kukomesha umwagaji wa damu, kuizingira Mamlaka ya Kizayuni kisiasa na kiuchumi, kuihukumu kwa ajili ya jinai zake za kigaidi ambazo imezoea kuzifanaya kwa zaidi ya miaka 75 dhidi raia wa Palestina, na kukomesha kwa mauaji ya kisasa, ambayo hayakusimamama kwa saa zote za siku, kwa muda wa 220 siku mfululizo.

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.