Wanadai .. Tunasahihisha

23

  • | Tuesday, 28 June, 2016

Uislamu ni uhusika unaojumuisha chini yake mielekeo yote ya kibinadamu ambayo haipingi dini hiyo kabisa wala haisaidii kuwalazimisha wafuasi wake kuiacha dini, enyi wadai hayo kwa kutumia dini, hakika Uislamu ni dini isiyohitaji vurugu yenu na ukatili wenu kwa ajili ya kupata ushindi wo wote, bali inahitaji mbinu ya Mtume (S.A.W.) ambayo ni mbinu timamu inayotumiwa katika Al-Azhar Al-Shareif ile taasisi ambayo nyinyi hamjui cho chote kuhusu taasisi hiyo! Kwa kweli Mwenyezi Mungu hakumpa ye yote haki ya kudhibiti mioyo ya watu wala awe kama upanga unaolengea vichwa vya watu hawa bali ni rehema, usamehevu, uadilifu na ubinadamu.
Kwa hakika mwislamu anayeishi kwa utulivu na amani na kufanya ibada za dini yake pasipo na kuvuka uhuru wa mtu ye yote na wala hakafirishi watu au kuwafanyia ukatili, mtu kama huyu haiwezekani kukataliwa na jamii yo yote ila kwa nadra, ama Uislamu ukizingatiwa kwa mujibu wa maoni ya watu hao ni dini ya vurugu, ukatili, mauaji, kulipua na kutolazimika mamlaka na kanuni ya nchi na matumizi ya silaha dhidi ya wasio na hatia basi wajue kwamba ni wajibu ya watawala wa nchi mbali mbali kuwapigania kwa mujibu wa kipimo cha ubinadamu; na kwa mujibu wa mafundisho ya dini na sheria.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.