Sheikh wa Al-Azhar atoa wito kwa watoa maamuzi ya kimataifa kujifunza ubinadamu kutoka kwa wananchi wao

  • | Sunday, 19 May, 2024
Sheikh wa Al-Azhar atoa wito kwa watoa maamuzi ya kimataifa kujifunza ubinadamu kutoka kwa wananchi wao

     Mheshimiwa Imamu Mkuu, profesa/ Ahmad Al-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar, alisema kuwa kwa hakika ulimwengu umepata kile kinachoweza kuitwa "schizophrenia ya kimataifa" iliyodhihiri kwa wazi baada ya uadui wa kizayuni dhidi ya Gaza kuanza; basi tukaona baadhi ya nchi zikitangaza kutoa misaada ya kibinadamu kwa Gaza, wakati huo huo zinatoa silaha, zana za kijeshi kwa mamlaka ya kizayuni; ili kuendeleza vitendo vyake vya mauaji na ugaidi, akisisitiza kwamba maendeleo katika sekta ya silaha hayaleti ustaarabu.

Sheikh wa Al-Azhar aliongeza, wakati wa kumpokea Bibi Anne Dorte Rijelsen, Balozi wa Denmark mjini Cairo, katika makao makuu ya Al-Azhar, kwamba watoa maamuzi ya kimataifa lazima wawajibikie hekima na akili, na kusikiliza kwa sauti za wananchi wao walioandamana ili kukataa mauaji ya kigaidi yanayofanywa na wazayuni huko Gaza, akisisitiza kwamba maandamano tunayoyaona siku hizi katika miji mingi ya Ulaya na Marekani, yakiwa matatizo yake hayatatatuliwa haraka kadiri iwezekanavyo na kusikilizwa kwa hekima, basi haiwezekani kutabiri nini kinaweza kutokea kwa sababu yake, na kwamba nchi za Magharibi na Marekani zinahitaji kujifunza kutoka kwa hayo na kuwa na yakini kwamba siasa za kutengwa, ukiritimba, kuunga mkono ukoloni, na kuziba masikio zitasababisha hasara kubwa mno, akiwatakia watoaji maamuzi katika nchi za Magharibi kujifunza ubinadamu kutoka kwa wananchi wao; tunaowathamini na kuthamini jukumu lao katika kuunga mkono haki za kipalestina.

Kwa upande wake, Balozi wa Denmark alieleza furaha yake ya kukutana na Imamu Mkuu, na kubainisha kuwa nchi yake imechukua hatua kadhaa za kuunga mkono haki za Wapalestina, na kwamba Denmark imepiga kura ya kuunga mkono Palestina katika azimio kuhusu kustahiki kupata uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa, kama alivyoonyesha kuwa nchi yake ilifungua hospitali huko Gaza kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa majeruhi na waathirika wa uadui wa kizayuni.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.